Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb)
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es
salaam
WAZIRI wa Fedha na Mipango,
Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa Serikali imeanza kuyafanyia kazi maoni na
malalamiko ya wafanyabiashara na wawekezaji kwa ujumla kuhusu kodi
zinazolalamikwa kwa lengo la kuhuisha ama kubadili kodi zinazoonekana kuwa ni
kero.
Dkt Mpango amesema hayo mara
baada ya kutembelea na kukagua maonesho ya kwanza ya viwanda vya ndani,
yanayofanyika katika Uwanja wa maonesho ya biashara wa Mwalimu J. K. Nyerere,
barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam.
Amewataka wafanyabiashara na
wawekezaji kuwasilisha maoni yao kuanzia mwezi huu wa Desemba wakati ambapo
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, iko katika mchakato wa kuandaa
Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Hata hivyo amewataka watanzania
na wafanyabiashara kwa ujumla kujenga utamaduni wa kulipa kodi ili kuijengea
uwezo serikali wa kuwahudumia katika nyanja mbalimbali za maendeleo na huduma
za jamii
Wakati huo huo, Dkt. Mpango,
amewataka watanzania kujenga tabia na utamaduni wa kuthamini na kununua bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini ili kujenga uchumi wa
ndani badala ya kununua vitu kutoka nje ya nchi ambavyo vingi kwa sasa
vinazidiwa ubora na bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini.
Zaidi ya wafanyabiashara 400
wamejitokeza kushiriki katika maonesho ya kwanza ya viwanda vya ndani
yanayotarajiwa kufungwa leo katika uwanja wa maonesho ya biashara wa mwalimu
J.K Nyerere, barabra ya Kilwa, Dar es salaam, ambapo maonesho hayo yameelezwa
kuwa na mafanikio makubwa.
No comments:
Post a Comment