Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia ya wananchi
kabla ya kuzindua Mashindano maarufu ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya
Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha
wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya
Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa
kufanyika mwezi ujao mwakani. Picha zote na Felix Mwagara.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akikata utepe kuashiria uzinduzi
wa Chama cha Kuweka na Kukopa (Vicoba-Together) katika sherehe iliyofanyika
Skuli ya Chekechea, Miembeni, Zanzibar. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Unguja.
Masauni alikichangia chama hicho shilingi milioni tatu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimkabidhi Mkurugenzi
wa Redio ya Coconut mjini Unguja, Zanzibar, Ally Dai, jezi kwa ajili ya
Mashindano maarufu ya Nage Mapinduzi Cup ambayo yamezinduliwa na kiongozi huyo katika
Viwanja vya Matumbaku mjini humo. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana
yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya
Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa kofia) akiyapokea
Maandamano ya timu 38 za Mashindano ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya
Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha
wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya
Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa
kufanyika mwezi ujao mwakani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wanachama wa Chama
cha Kuweka na Kukopa cha Vicoba-Together (hawapo pichani) kabla ya kuzindua
kikundi hicho katika sherehe iliyofanyika Skuli ya Chekechea, Miembeni,
Zanzibar. Kushoto ni Katibu wa Vicoba Together, Mwashum Mohammed Mustafa. Kulia
ni Katibu wa Jimbo la Kikwajuni, Kassim Ally Juma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizikagua timu ya Kikwajuni na
Baa kutoka Jimbo la Mtoni kabla ya kuanza Mashindano ya Nage Mapinduzi Cup
katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano
hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo
yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya
Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
Mchezaji wa Timu ya Kikwajuni, mjini Unguja, Zanzibar
akijaza chupa mchanga wakati wa Mashindano ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja
vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha
wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya
Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa
kufanyika mwezi ujao mwakani. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni alizindua
Mashindano hayo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (katikati waliokaa) akiwa katika
picha ya pamoja na wanachama wa Chama
cha Kuweka na Kukopa cha Vicoba Together. Masauni alikichangia chama hicho
shilingi milioni tatu. Picha zote na Felix Mwagara
*****************************************************************
No comments:
Post a Comment