Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 10 December 2016

SUALA LA MCHEZAJI HASSAN RAMADHANI KESSY


Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote kwa njia ya mahojiano, na vielelezo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imebaini mambo yafuatayo ambayo yanapaswa kuchukuliwa hatua za haraka:
  1. 1. Mchezaji Hassan Hamis Ramadhan au Hassan Kessy alikuwa na Mkataba na Klabu ya Simba uliokuwa unaishia tarehe 15/06/2016.
  1. 2. Young Africans SC walikiri mbele ya Kamati kupeleka jina la Mchezaji Hassan Ramadhani Kessy huko Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tarehe 10/06/2016 huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na klabu ya Simba.
  1. 3. TFF kupitia Sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuweza kuielekeza Young Africans SC hatua stahiki za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Klabu ya Simba kama taratibu zinavyoelekeza. Kama hatua hii ingechukuliwa kwa wakati mwafaka mgogoro huu usingekuwa na sura ya sasa na pengine usingekuwepo.
  1. 4. Simba SC walileta machapisho yanayotokana na Mtandao/blog wa mtu waliomtaja kuwa ni Bin Zubeiry ukimwonyesha Mchezaji yuko na viongozi wa Young Africans.
  1. 5. Young Africans SC ilionesha Mkataba iliosainiwa na Hassan Hamis Kessy tarehe 20/6/2016 na hivyo hakukuwa na sababu ya msingi ya kufanya mambo yaliyoainishwa kwenye kipengele cha 2 and cha 4 kabla ya kumalizika kwa mkataba kati mchezaji Haasan Kessy na Klabu ya Simba.
  1. 6. Bila kuathiri hadhi ya Uanachama wengine wa TFF, Klabu ya Simba ni brand kubwa kama ilivyo Klabu ya Young Africans, umakini mkubwa upaswa kutumika katika kushughulikia brand hizi ili kuepuka madhara yasiyokuwa ya lazima.
HATUA:

Kitendo cha Klabu ya Young Africans kupeleka jina la mchezaji wa klabu nyingine CAF huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na mwanachama mwingine wa TFF ni kosa kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kifungu 69[5] ambalo linapaswa kupewa adhabu itakayopelekea wanachama wote kuheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili na sio kuanza kwenda CAF au kwingineko ili kulinda integrity ya soka la Tanzania. 

Klabu ya Young Africans inatozwa faini ya Sh 3,000,000 (Sh milioni tatu) kwa mujibu wa kanuni na fidia kwa klabu ya Simba ya Sh 50,000,000 (Shilingi milioni hamsini).

Ofisa wa TTF aliyehusika ama kwa kushirikiana na Uongozi wa Klabu ya Young Africans au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati apelekwe kwenye mamlaka yake ya nidhamu, yaani, Katibu Mkuu wa TFF ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

No comments:

Post a Comment