Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 31 January 2016

WAZIRI MAKAMBA ATOA MSAADA MABATI 300 KWA WAHANGA AMBAO NYUMBA ZAO ZILIZOEZULIWA NA UPEPO JIMBONI KWAKE.

January Makamba

NA RAISA SAID, BUMBULI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshugulikia Muungano na Mazingira,January Makamba ametoa msada wa mabati 300 kwa wananchi ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha maeneo mbalimbali jimboni humo.


Nyumba hizo zilikuwa 40 ikiwemo  Kanisa  na Msikiti zimeezuliwa mapaa katika kijiji cha Msamaka kilichopo wilayani Bumbuli kufuatia Mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha.

Mvua hiyo imesabisha  kaya  hizo  kukosa  mahali pa kuishi , huku wengi wa  waathirika  wakipewa hifadhi  kwenye  nyumba  za majirani zao.

Akizungumza  na waandishi wa habari hapo Jana Afisa Mtendaji wa kijiji cha Msamaka Mbazi Shemhando alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo January 27 mwaka huku saa kumi jioni.

Alitaja sehemu zilizo athirika zaidi  kuwa  ni Vitongoji vya Kwemchaa, Nazareti,CCM, Kwakorosi pamoja na kitongoji cha Kwamingojo ndio vimeweza kuathirika na maafa hayo.

Hata hivyo aliongeza kuwa waathirika watukio hilo Kwa sasa wamehifadhiwa kwenye nyumba za Jirani wakati utaratibu mwingine wa kuwasaidia ukiendelea kuwekwa.

Akikabidhi msaada huo Makamba alisema kuwa kutokana na tukio hilo anatanguliza msaada huo kwanza wakati akiendelea kutafuta msaada zaidi.

"Nimejikusanya Kwa hiki kidogo ili kiweze kusaidia pale penye uhitaji Kwa haraka wakati tukiendelea na utaratibu  mwingine" alisema Makamba.

Makamba   aliwataka  wananchi  wote  kupanda  miti ili kuepuka  upepo mkali  unaosababishwa  na  mvua  zinazoendelea kunyesha  katika maeneo tofauti

No comments:

Post a Comment