Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 27 January 2016

BONNY MWAITEGE: TAMASHA LA PASAKA TULIPE UZITO WAKE


Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injil, Bonny Mwaitege ametoa wito kwa Watanzania kuilipa uzito wa aina yake Tamasha la Pasaka kwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria tukio hilo adhimu duniani.Mwaitege alisema Tamasha la Pasaka lina ujumbe wa Mungu hivyo Watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi na kumkimbilia Mungu katika tamasha hilo.
"Watanzania tunatakiwa tujitokeze kwa wingi kwa sababu Yesu alikufa na kufufuka, hivyo kuna kuna ujumbe mkubwa  kutoka kwa Mungu ambao utawaokoa Watanzania wote," alisema Mwaitege.  
Mwaitege alisema kupitia tamasha hilo jamii inaondokana na machafu ambayo yanamchukiza Mungu.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema tamasha la mwaka huu wamejipanga vilivyo kufanikisha matakwa ya jamii kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za injili na viongozi wa dini watakaohudhuria tamasha hilo.
Msama alisema tamasha la mwaka huu wamepanga litaanza Machi 26 hadi 28 hapa nchini, hivyo Watanzania wajiandae na tamasha hilo.
"Watanzania watarajie tamasha bora ambalo litafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii, hivyo wajiandae," alisema Msama.

No comments:

Post a Comment