Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 22 January 2016

MCHEZAJI NYOTA WA UGANDA KUHAMIA UBELGIJI

Miya
Image copyrightANDREW ORYADA
Image captionMiya alifungia Uganda bao moja dhidi ya Mali CHAN
Mshambuliaji wa Uganda Farouk Miya, anayechezea taifa hilo michuano ya CHAN inayoendelea Rwanda, anatarajiwa kujiunga na klabu ya Standard Liege ya Ubelgiji.

Kwa sasa amekuwa akichezea klabu ya Vipers Sports Club.
Klabu hizo mbili zimekubaliana uhamisho wake dola za Kimarekani 400,000 na mkataba unatarajiwa kutiwa saini baada ya michuano ya kombe la taifa bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani.
Miya, 19, aliwafungia Uganda penalti na akasaidia ufungaji wa bao la pili mechi yao ya kwanza CHAN ambayo walitoka sare ya 2-2 na Mali.
Hata hivyo, hataweza kucheza Jumamosi dhidi ya Zambia kama tahadhari baada yake kutatizwa na bega.
Msimu uliopita, Miya alifunga mabao 11 na kusaidia ufungaji wa mengine saba huku akisaidia Vipers kushinda taji la ligi kuu ya Uganda.
Amekuwa katika klabu ya Vipers kwa miaka miwili.

No comments:

Post a Comment