Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 29 October 2013

MAKAMANDA WA AL-SHABAAB WAUAWA

 KOMBORA lililorushwa kusini mwa Somalia limewaua makamanda wawili wa kundi la Kiislamu la al-Sahaab, wakazi wa eneo hilo wameiambia BBC.
Bomu hilo limeiteketeza gari ambayo wapiganaji hao walikuwa wakisafiria kati ya miji miwili ya Jilib na Barawe, ambayo inaonekana kuwa ni ngome kuvwa za al-Shabab, walisema.
Marekani ilianzisha mashambulizi yaliyofeli katika mji wa Barawe mapema mwezi huu ili kumkamata kamanda wa al-Shabab, kundi ambalo ndilo mwakilishi mkubwa wa al-Qaeda kwa Afrika Mashariki.
Vyanzo kutoka jeshi la Kenya vimeieleza BBC kwamba vikosi vyao vilikuwa vimeuvamia Jilib, na kwamba lazima kutakuwa na watu walliouawa.
Wakazi wa Jilib, takriban 120km kaskazini mwa bandari ya Kismayo, waliiambia BBC kwamba lilikuwa ni bomu lililoangushwa ambalo liliwaua makamanda wa al-Shabab.
Mmoja kati ya waliokufa alikuwa mtaalam wa milipuko wa al-Shabab, akijulikana kama Anta.
"Mchana wa leo, nimesikia kishindo kikuu na kuona ndege ikipotelea angani, watu wawili wamekufa," mkazi wa eneo hilo Hassan Nur aliiambia Reuters.
"Nimeshuhudia gari aina ya Suzuki ikiteketea, wafuasi wengi wa al-Shabab walikuja kwenye tukio. Nimewaona wakiwa wamebeba maiti mbili," alisema.
CHANZO: BBC



No comments:

Post a Comment