Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 29 October 2013

ASKARI MWINGINE WA JWTZ AUAWA CONGO, M23 WAKIMBIA

Vikosi vya jeshi la Congo DR vikishangilia huko Rumangabo baada ya kuutwaa mji huo, jana Jumatatu Oktoba 28.

ASKARI mwingine wa JWTZ aliyeko katika vikosi vya kulinda amani nchini DR Congo, anadaiwa kuuawa juzi Jumapili, katika mapambano na waasi wa M23.
Habari kutoka mashariki mwa nchi hiyo zinaelezwa kwamba, askari huyo alikufa wakati akiwalinda raia katika mji wa Kiwanja.
Bado haijajulikana jina la askari huyo, ambaye kifo chake kimeongeza idadi ya askari wa JWTZ waliopoteza maisha katika mapambano hayo.
Hata hivyo, ujumbe maalum wa Umoja wa Mataifa huko Congo DR vimelieleza Baraza la Usalama la UN kwamba harakati za waasi wa M23 zimesambaratika na siyo tishio la kijeshi.
Martin Kobler alisema M23 wametelekeza sehemu nyingi walizokuwa wanashikilia kijeshi huko mashariki na walikuwa wamebanwa kwenye eneo la pembetatu karibu na mpaka wa Rwanda.
Eneo la tano lililokuwa linashikiliwa na waasi hao limetwaliwa na vikosi vya serikali jana Jumatatu.
Waasi hao wamesema uamuzi wao wa kuachia maeneo hayo ni wa muda.
Kobler aliliambia Baraza la Usalama la UN kwa kutumia video: "Inaonekana ni mwisho wa harakati za kijeshi za M23."
Alisema waasi hao wametelekeza sehemu muhimu katika Mlima Hehu jirani na mpaka wa Rwanda.
Baada ya mkutano wa UN, Balozi wa Ufaransa Gerard Araud alisema anatumaini sasa kutakuwa na mazungumzo kati ya waasi na serikali.
Alisema: "Kobler ametujulisha na kimsingi ametuambia kwamba tunashuhudia uwezo wa kijeshi wa M23.
"Kwa hiyo nadhani ni mafanikio na kumekuwepo na makubaliano kwamba sasa tunaweza kurejea kwenye meza ya mazungumzo mjini Kampala."
Mazungumzo ya amani kati ya serikali na M23, yaliyoandaliwa na nchi jirani ya Uganda, yalivunjika wiki iliyopita.
Kumekuwepo na utulivu wa miezi miwili mashariki mwa Congo.
Umati wa watu unadaiwa kuwapokea wanajeshi wa serikali Jumatatu kwenye mji wa Rumangabo, ambako kulikuwa na ngome ya M23.
Serikali imeanza kuweka utawala wake hapo, alisema gavana wa Kivu Kaskazini Julien Palukui.
"Tumeitisha mikutano miwili kujadili namna ya kuwakusanya wananchi... na tunatangaza kurejeshwa kwa huduma za kijamii ndani ya saa 24 zijazo,'' aliongeza.
Rumangabo - mji ambao uko karibu 50km kaskazini mwa Goma, mji mkubwa mashariki mwa Congo DR - ulikuwa na mojawapo ya ngome tatu kubwa za kijeshi kabla ya kutwaliwa na waasi mwaka jana.
Jumapili, Vikosi vya Kulinda Amani nchini DR Congo, Monusco, vilisema askari wa kulinda amani wa Tanzania aliuawa wakati wa mapambano na M23 katika mji wa Kiwanja.
"Askari huyo alikufa wakati akiwalinda watu wa Kiwanja," ilisema taarifa ya Monusco.
Mafanikio ya kuukomboa mji wa Rumangabo yanafuatia kukombolewa kwa maeneo manne - Kiwanja, Rutshuru, Buhumba na Kibumba - tangu mwishoni mwa wiki, jeshi la nchi hiyo limesema.
Maofisa wa M23 nchini Uganda wamesema wapiganaji wao wamerudi nyuma kwa sababu serikali na vikosi vya UN wameanzisha mashambulizi ya nguvu.
Wapiganaji hao sasa wanajipanga upya kabla ya kurejea kwenye mapambano, walisema maofisa hao.
Karibu watu 800,000 wameyakimbia makazi yao huko DR Congo tangu M23 walipoanzisha mapmabano yao Aprili 2012.
CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment