TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA
MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
[ DIWANI ATHUMANI - ACP
]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
“PRESS RELEASE” TAREHE 22. 10. 2013.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SARE ZA
ASKARI WANYAMA PORI NA PINGU.
MNAMO TAREHE 18.10.2013 MAJIRA YA SAA
13:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA BITIMANYANGA, KATA YA MAFYEKO, TARAFA YA
KIPEMBAWE WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA/MSAKO KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WANYAMAPORI WALIMKAMATA SAMWEL S/O
VITALIS @ MANDE , MIAKA 34, MNYATURU, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA BITIMANYANGA
AKIWA NA SARE PAIR MOJA “KOMBATI” ZA ASKARI WA WANYAMAPORI PAMOJA
NA PINGU MOJA. MBINU NI KUTUMIA VIFAA HIVYO KATIKA UWINDAJI HARAMU.
TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI MALI ZA SERIKALI ISIVYO HALALI
KWANI NI KOSA LA JINAI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA
JUU YA MTU/WATU AU KIKUNDI KINACHOMILIKI MALI ZA SERIKALI /WAWINDAJI
HARAMU AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA
ICHUKUE MKONDO WAKE.
MNAMO TAREHE 21.10.2013 MAJIRA YA SAA
12:00HRS HUKO KATIKA MTAA WA MANGA – MWANJELWA , KATA YA MANGA , TARAFA
YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO
WALIWAKAMATA 1. ITIKA D/O KIMANGA,, MIAKA 41, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA
MWANJELWA 2. YASIWA S/O SHELISHELI, MIAKA 37, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA MANGA,
3. MATESO S/O SHELISHELI, MIAKA 33, MNYIHA,MKULIMA, MKAZI WA CHUNYA NA 4.
EMANUEL S/O SILAVWE, MIAKA 33, MNYAMWANGA, MKULIMA, MKAZI WA MANGA WAKIWA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA NANE [08]. WATUHUMIWA NI WAUZAJI
NA WATUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI
WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA
YA MTUMIAJI.
WILAYA YA MOMBA – KUPATIKANA NA
BHANGI.
MNAMO TAREHE 21.10.2013 MAJIRA YA SAA
05:00HRS HUKO KATIKA MTAA WA MJINI , KATA YA TUNDUMA , TARAFA YA
TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA/MSAKO WALIMKAMATA 1. EDMUND S/O KANFWA,, MIAKA 41, KYUSA, MKULIMA,
MKAZI WA MWANJELWA NA 2. TAIFA S/O MWAMAHONJE, MIAKA 22, MMALILA, MKULIMA
WOTE WAKAZI WA MIGOMBANI – TUNDUMA WAKIWA NA BHANGI KETE 18 SAWA NA UZITO WA
GRAM 90. WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA WAVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA
KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI.
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment