Na Brother Danny
IWE ni utumwa au ni shurutisho, lakini baadhi ya watu
hawawezi kuacha kufanya mapenzi na mara nyingi huwa wanatambua kwamba wana
matatizo mara baada ya kitendo chenyewe, na hapo ndipo Waswahili husema;
"Kijuto msuto kisicho kito!" Hujutia kitendo hicho wakati
wameshakifanya.
Wakati mwanamuziki mkongwe wa miondoko laini wa Marekani, George Michael, alipokamatwa mnamo Aprili 7, 1998 akikabiliwa na shtaka la kulawitiwa kwenye choo cha mbuga ya wanyama huko Beverly Hills, magazeti mengi yaliandika yalivyojua. Gazeti la New York Post la Aprili 9, 1998 liliandika kwa maandishi makubwa ukurasa wa mbele DOWN & OUTED IN BEVERLY HILLS na tangazo lililokuwa ndani ya habari hiyo liliandika kidaku zaidi likisema ZIP ME UP BEFORE YOU GO GO, yaani 'Nifunge zipu kabla ya kuondoka!'. Habari nyingi za kidaku ziliandikwa, kila gazeti likiwa na kichwa tofauti cha habari kuelezea tukio hilo moja, na zaidi kwa sababu Michael siku zote alikuwa msiri kuhusu jinsia yake, akiwa hataki kutoa taarifa thabiti ya jinsia gani aliyokuwa akiipendelea kutokana na vitendo vya kishoga vilivyokuwa vikiripotiwa dhidi yake. Lakini mwanamuziki mwingine mkongwe Boy George ambaye pia ni shoga alimweleza Michael asione aibu. "We are sisters under the skin," yaani "Sisi ni wanawake ndani ya ngozi" aliandika katika barua ya wazi iliyochapishwa kwenye gazeti la The Express la London mara baada ya kukamatwa kwa Michael.
Wakati mwanamuziki mkongwe wa miondoko laini wa Marekani, George Michael, alipokamatwa mnamo Aprili 7, 1998 akikabiliwa na shtaka la kulawitiwa kwenye choo cha mbuga ya wanyama huko Beverly Hills, magazeti mengi yaliandika yalivyojua. Gazeti la New York Post la Aprili 9, 1998 liliandika kwa maandishi makubwa ukurasa wa mbele DOWN & OUTED IN BEVERLY HILLS na tangazo lililokuwa ndani ya habari hiyo liliandika kidaku zaidi likisema ZIP ME UP BEFORE YOU GO GO, yaani 'Nifunge zipu kabla ya kuondoka!'. Habari nyingi za kidaku ziliandikwa, kila gazeti likiwa na kichwa tofauti cha habari kuelezea tukio hilo moja, na zaidi kwa sababu Michael siku zote alikuwa msiri kuhusu jinsia yake, akiwa hataki kutoa taarifa thabiti ya jinsia gani aliyokuwa akiipendelea kutokana na vitendo vya kishoga vilivyokuwa vikiripotiwa dhidi yake. Lakini mwanamuziki mwingine mkongwe Boy George ambaye pia ni shoga alimweleza Michael asione aibu. "We are sisters under the skin," yaani "Sisi ni wanawake ndani ya ngozi" aliandika katika barua ya wazi iliyochapishwa kwenye gazeti la The Express la London mara baada ya kukamatwa kwa Michael.
Mshtuko hata hivyo haukuwa mkubwa eti kwa sababu Michael
alikuwa shoga. Tetesi kuhusu ushoga wa George Michael zilikuwa zimesambaa kwa
miaka kadhaa na katika mahojiano mwaka 1997 alizungumzia kuhusu mapenzi yake
kwa mwanamume mmoja wa Brazil aliyefariki kutokana na matatizo ya ubongo mwaka
1993. Kitu ambacho kila mmoja alikuwa akijiuliza kilikuwa, "Alikuwa
kifanya nini bafuni?" Yeye ni mwanamume tajiri, mwenye kipaji na mvuto.
Kama alikuwa akifanya kile ambacho alituhumiwa nacho, kama alikuwa akijaribu
kufanya mapenzi na mtu katika chumba cha kupumzika watu wote, ni kwa nini
akachagua choo kuwa ndiyo mahali muafaka pa kufanyia mapenzi? Watu wachache
walishangaa kwa sauti, Hivi George Michael ni mtumwa wa ngono?
Wakati Michael alipozungumza kupitia kituo cha luninga cha
CNN siku chache baada ya kukamatwa kwake, pia alimaanisha, bila kueleza
kinaganaga, kwamba yeye ana tatizo. "Nadhani ni hatari ya hali yenyewe
ndiyo iliyosababisha nikafanya vile, kwa sababu hakika ilikuwa kama
shurutisho," Michael alimweleza mwandishi Jim Moret. Mapema katika
mahojiano hayo Michael alikuwa amesema, "Siwezi kusema pia kwamba hiyo
ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kutokea. Unajua, nimejiweka katika nafasi hiyo
kabla. Ninachoweza kufanya ni kuomba samahani tu. Ninaweza kujaribu kufikiria
kwa nini nilifanya vile, kuielewa jinsia yangu kwa undani kidogo, lakini, bila
kutarajia, upande wangu mmoja unaamini kwamba baadhi ya shurutisho hizi ni
kwamba ningeweza kufumaniwa... Najiona mpumbavu na mzembe na dhaifu kwa
kuruhusu jinsia na tamaa yangu ya mapenzi ikafichuka namna hii."
Wakati ni rahisi kujua nini kinachoendelea katika fikra za
Michael, maneno yake yanafanana na yale yanayotumiwa na watumwa wengi wa ngono
kuelezea baadhi ya vitendo vyao vibaya na namna walivyojisikia wakati
walipofumaniwa.
Mwitikio kutokana na tukio la Michael ulizusha mdahalo wa
mara kwa mara miongoni mwa mshoga na wasagaji kuhusiana na tafsiri tofauti za
utumwa wa ngono na uhuru wa ngono. Kama ungezungumza na wataalamu na watu
wanaotambua uraibu basi wangekwambia kwamba Michael ni mtumwa wa ngono. Kama
ungezungumza na Keith Griffith, mmiliki wa tovuti ya Cruising for Sex, mtandao
ambao ulielezea mbuga ya huko Beverly Hills kwamba ina "vyumba vingi vya
wanawake, basi ungeiona hasira yake. "wali ambalo nategemea polisi
wangeulizwa," alisema Griffith baada ya tukio hilo, "ni kwa nini
wanapoteza fedha nyingi za kodi katika shughuli kama hii."
Griffith na mashoga wengine, kama wanachama wa Sex Panic!-kundi linalozungumzi mapenzi
huru lililoanziishwa mwaka 1997- wanaona kwamba mapenzi kwenye umma ndilo
suluhisho la karne kwa karne za ukomeshaji wa mapenzi. Lakini mashoga na
wasagaji wengi wanasema kwamba mapenzi katika sehemu za umma ni tofauti na
uraibu, na kwamba bafu na klabu za mapenzi, hasa zile za usiku ambako watu
wanaweza kufanya mapenzi hadharani, hasa katika nchi zilizoendelea, hazistahili
kupigwa marufuku kwa sababu kufanya hivyo ni uonevu.
Kama lilivyo wazo lenyewe, uraibu wa mapenzi uliingia na
mzigo wa siasa. Matukio ya miaka ya 1960 na 190, wakati wanaume mashoga na
wanawake wasagaji waipoanza kuibuka kwa mara ya kwanza katika idadi kubwa na
wakati watu wengi walikuwa wakipiga vita mapinduzi ya mapenzi, yalisababisha
kutoweka kwa maradhi mengine ya mapenzi kifikra kama, ushoga na
nymphomania-kutoka kwenye 'biblia ya afya ya akili', ambacho ndicho kitabu cha Diagnostic & Statistical Manual of
Mental Disorders, maarufu kama DSM. Matatizo mengine yaliyojitokeza kwa
kuwa na nguvu kidogo za kufanya mapenzi au kutokuwa nazo kabisa, kama uhanithi
(impotence) na mshindo usiokomaa (premature ejaculation), yaliongezwa.
Lakini baadaye, kutokana na kuibuka kwa maradhi ya zinaa kama herpes, kaswende
(syphilis) na baadaye UKIMWI,
kulikuwa na mtazamo tofauti kuhusu mfumo wa maisha wa mapenzi huru na rahisi -
mfumo wa maisha ambao mashoga na wasagaji waliamua kuutumia zaidi na kihistoria
ndio wanaouona kama ni sehemu yao hasa. Watu walikuwa wakifanya mapenzi kwa
kiwango kikubwa na mambo mengi mabaya yakawakumba.
"Katika miaka ya 1970 tabia za mapenzi hazikuwakilisha
patholojia, yaani sayansi ya magonjwa," anasema mwanasosholojia John
Gangnon wa State University of New York huko Stony Brook. "Lakini katika
miaka ya 1990, kwa sababu ya maradhi ya UKIMWI, kuwa na idadi kubwa ya wapenzi
(inachukuliwa) siyo vizuri. Hii kwangu naiona kama siyo sahihi."
Lakini bado, utumwa wa ngono umeendelea kushikilia kasi.
Waathirika wa ngono hawaachi kufanya mapenzi; hawakomi kuyatafuta, hawakomi
kufikiria wala kufanya chochote katika maisha yao ili tu kukidhi kiu yao.
"Mapenzi ndicho kitu pekee ambacho kilikuwa muhimu
kwangu," anasema Ken, ambaye amekuwa akitibiwa uraibu wa ngono kwa miaka
kumi. "Ilikua kama kujaribu kula sukari peke yake. Inaweza kujaza tumbo
lako, lakini unashinda na njaa." Ataalamu wanasema kwamba, waathirika
wataendelea na tabia zao hata pale wanapokabiliana na matatizo mengi, kama
kupoteza familia zao, kazi, uhuru wao, kufumaniwa wakifanya mapenzi au wakipiga
punyeto na hata kupoteza maisha yao. Hawawezi kujidhibiti na wanajiona wako
dhaifu. "Nilikuwa nateseka kwa njaa," anasema Ken, "na nilikuwa
katika hatari ya kujiua."
Kama nilivyosema hapo awali, sababu zinazochangia uraibu wa
ngono ni nyingi sana, lakini kikubwa ninachotaka kusema ni kwamba,
"Mapenzi ndicho kitu pekee wanachokitaka." Kwa mtu ambaye ameraibiwa
katika mapenzi, kauli hii huwa ubeti maarufu vichwani mwao. Hatimaye huwa kama
ukweli. Utumwa wa mapenzi ni nini na kwa nini baadhi ya wanaume na wanawake
wanaraibiwa katika mapenzi? Tatizo hili linawezaje kujulikana na namna gani
wale walioathirika wanavyoweza kusaidiwa?
Utumwa
wa Kisaikolojia
Utumwa wa mapenzi ni uraibu wa kisaikolojia, matokeo ya
matamanio yasiyofikiwa ya utotoni. Watoto ambao mahitaji yao hubakia ykiwa
hayatambuliki wanaweza kurekebisha kwa kujifunza udhibiti matarajio yao.
Utaratibu huu wa udhibiti unaweza kuchukua muundo wa mawazo mabaya kama,
"Mahitaji yangu hayahesabiki," "Kuwa karibu kunaweza kuumiza
" na "Nastahili kupendwa." Mawazo kama haya hayatoshelezi
mahitaji ya utotoni, kuyaacha kutawafanya wakumbane nao baadaye maishani mwao.
Kama watu wazima, wapenzi walioraibiwa huendelea kubakia tegemezi kwa wengine
kuwahudumia, kuwalinda na kusuluhisha matatizo yao.
Walioraibiwa kimapenzi huwa wana matumaini ya ajabu na hofu
zisizokwisha. Kuhofia kukataliwa, maumivu, kuhofia mambo wasiyoyazoea na
kutokuwa na mani na uwezo wao - au hata haki zao - kuelezea mapenzi, husubiri,
huomba na hutumainia mapenzi, pengine ndio uzoefu wao mdogo kabisa.
Kwa waathirika, mapenzi: Yanadhoofisha na yana tamaa;
Yanafichwa; Yanaepuka madhara au mabadiliko; Hukosa urafiki wa ndani na wa
kweli: Ni tegemezi na yana madhara; na Hutaka yule anayependwa ndiye aonyeshe
upendo wa dhati.
Madhara
ya Utumwa wa Mapenzi
Penzi ililoraibiwa limegubikwa na tamaa ya kuiona dnia yote
kama iko kwa mpenzi mmoja tu. Ukuaji na maendeleo yao yakiwa yamehribiwa mapema
katika maisha yao, wapenzi walioraibiwa hung'ang'ana katika utambulisho wa
wapenzi wao. Kama mpenzi wake ana mali nyingi au ni maarufu, basi kila mahali
atakapokuwa atapenda kujitambulisha kama sehemu ya huyo mpenzi wake. Nakumbuka
dada mmoja mwandishi wa habari ambaye sipendi kumtaja jina, wakati uhusiano
wake ulipokuwa katika hatua za awali na mchezaji mmoja wa klabu moja kongwe ya
soka Tanzania, alikuwa akipenda kujitambulisha kama "Mama Fulani",
yaani jina lake la ubini alikuwa akiliweka la yule mchezaji! Waandishi wenzake
wengi, hasa wasichana wenzake, walikuwa wakimshangaa, akini yeye aliona fahari
kubwa kujiita Mama Fulani. Huu ni utumwa wa mapenzi bila yeye mwenyewe kujijua.
Watu wa namna hii hupenda kupata sifa kwa migongo ya wapenzi wao, na wakati
mwingine watu hawa hupenda kulazimisha wapatiwe upendeleo fulani kutokana na
umaarufu, utajiri au uwezo na mafankio ya mpenzi wake.
Kutokana na hofu ya mabadiliko, wapenzi walioraibiwa
watatunisha maendeleo ya nafsi zao, wakitafuta ulinzi wakiamini kwamba hawawezi
kutofautishwa kutoka kwa wapenzi wao. Wakati mwingine hofu ya mabadiliko ni
kubwa kiasi kwamba maendeleo na uwezo binafsi, haja na tamaa zao nyingine
huyeyuka.
Haja ya kuwa na ulinzi na utegemezi huleteleza matatizo ya
kihisia. Wapenzi ambao ameraibiwa wanahadaika kwamba kufanya mambo kwa
kuwafurahisha wapenzi wao kutawafanya wapendwe. Mfano kupendelea kumnunulia
mpenzi wako zawadi, kadi a maua, na hata kumsifia kila wakati au kumgana kila
mahali. Hali hii ni mbaya sana na watu wengi wamekuwa wakifanya hivi bila
kutambua kwamba kuna madhara, na tena ni utumwa ambao mtu amejipa bila mwenyewe
kutambua.
Kama utagundua kwamba uko katika uhusiano wa aina hii,
unapaswa kutafuta msaada wa kitaalamu haraka sana, vinginevyo unaweza
kuharibikiwa zaidi.
Tukutane wakati mwingine. Niandikie kupitia: brotherdanny5@gmail.com au +255 715
070 109
No comments:
Post a Comment