Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo
toka kwa Meneja mradi wa Maganga Matatitu Resource Development limited
Bw.
Lawrence Manyama kuhusu mlima huo uliosheheni mashapu ya chuma
alipotembelea eneo lenye utajiri wa chuma la Liganga wilaya ya Ludewa
mkoani Njombe leo
Oktoba 22, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wawekezaji
wa kampuni ya Sichuan Hongda ya China ambao ni wawekezaji katika eneo lenye
utajiri wa chuma la Liganga wilaya ya
Ludewa mkoani Njombe leo Oktoba 22, 2013. Kampuni hiyo inatarajiwa kujenga
kiwanda cha kufua chuma mapema mwakani kitachajiri watu 32,000 kitakapokamilika.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionesha kilele cha
Central Liganga hill ambacho ni mojawapo ya sehemu ambazo kampuni ya Sichuan
Hongda ya China itachimba mashapu ya chuma na kuyafua katika kiwanda kikubwa cha kufua chuma kitachoajiri
watu 32, 000 katika eneo hilo lenye utajiri wa chuma la Liganga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe leo
Oktoba 22, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na
wananchi alipoowasili katika uwanja wa mikutano wa Ludewa ambako alihutubia
mkutano wa hadhara. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment