Picha kwa hisani ya enrichmentjournal.ag.org
Ngono: Ni neno linalozungumzia kwa mapana mambo mengi yakiwemo
kutazama picha za ngono, kujichua (masturbation) na mambo mengineyo. Lakini kwa
baadhi ya Waamerika, wingi wa ngono katika utamaduni wao umekuwa mtego, ambao
ni mgumu kuukwepa.
Mwandishi wa habari wa CBN, Gailon Totheroh, anatuambia jinsi uambukizo wa watumwa wa ngono unavyoweza kuwafanya waathirika wakajidhuru na namna Mungu anavyoweza kuleta matumaini mapya.
Utumwa au uraibu wa ngono (sexual addiction) - baadhi wanauita ugonjwa uliojificha. Wengine
wanauita "dhambi isiyozungumza."
Wakati watu wengi huweka taswira ya wanyama waliopagawishwa
na mapenzi, ukweli wa utumwa wa ngono uko tofauti. Wengi wa waathirika siyo
wahalifu kifikra na siyo kwamba wazembe.
Ni nani hawa watumwa wa ngono? Jibu linaweza kukushangaza.
"Utumwa wa ngono huathiri mipango yote ya maisha," anasema Dk.
Douglas Weiss, Mmarekani ambaye ameegemea zaidi katika ushauri wa watumwa wa
ngono. "Nina watu wengi sana, wengine ni wanafunzi wa seminari, madaktari,
maseneta na wanamichezo. Hebu fikiria mwenyewe wengine, wataalamu wa mahesabu
wenye CPA zao, mafundi wa kompyuta - mtu yeyote anaweza kuwa mtumwa wa ngono,
kwa sababu ndiyo njia ambayo tumekuzwa nayo tangu tukiwa watoto na tuliendelea
nayo mpaka kwenye balehe. Siyo inatokea wakati tukiwa na umri wa miaka
40."
Na wengine wanasema kwamba hiyo ndiyo sababu watu
wasishangae kuhusu kashfa za ngono zinazotokea kwenye Ikulu ya nchi hiyo (White
House).
Dolly Kyle Browning, muathirika ambaye alisoma darasa moja
na Bill Clinton, rais mstaafu wa Marekani, katika shule ya juu kabla ya kwenda chuo kikuu. Mwanamke huyo
anasema kwamba walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa miaka 30 na kwamba mnamo
mwaka 1988, aliwahi kuzungumza naye kuhusu uraibu wa ngono.
"Hivyo nikamuuliza, utumwa huu wa ngono umehatarisha
malengo yako ya maisha na yeye alihuzunika sana na huo ndio ulikuwa ukweli, lakini
bila kuliacha hilo lielee, nikamwambia, 'Umeshawahi kufikiria kwamba unaweza
kuwa mtumwa wa ngono?' " anakumbuka Browning. "Naye akaitikia kwa
kutikisa kichwa na kusema, 'Najua mimi ni mtumwa wa ngono na ninajitahidi
kushinda.' "
Katika kadhia yake ya kujisalimisha kwa Paula Jones, Bill
Clinton alikana katu katu kwamba hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
Browning na kutokana na namna alivyojitetea, inaonekana kwamba Wamarekani
hawako tayari kuafiki tuhuma hizo. Lakini Browning anaamini kwamba wastani wa
Wamarekani wengi hawajui utumwa wa ngono unajihusisha kwa namna gani.
"Kama wangepambana na kweli wote, kitu ambacho ni
kugumu kuliko kawaida, mawazo yao yangeasi," anasema mwanamke huyo ambaye
tayari amekwishapatiwa tiba ya utumwa wa ngono. "Hawaelewi chochote,
lakini sasa mwathirika wa ngono anaelewa, na kwa mtu wa kawaida, tabia hii
inaonekana kuwa mbali sana na haisadikiki, hawawezi kusadiki."
Ukweli kwamba waathirika wengi wa utumwa wa ngono ni watu
wenye familia zao, kazi zao na hata ni waumini ama viongozi wa dini unaweza
kuwashangaza watu wengi na kuleta matatizo makubwa kwa wahusika wenyewe na
jamii kwa ujumla.
Fikiria, unaweza kumkuta baba mzima mwenye familia yake na
fedha zake akitangatanga na watoto wadogo, tena wale wa shule, huku akimwacha
mama watoto wake akiwa hajui lolote. Mama mzima mwenye fedha na maisha ya hali
ya juu, anamwacha mumewe na kutafuta vijana ili wakidhi kiu yake ya mapenzi,
kwa madai kwamba mumewe amechoka na akifika mshindo mmoja yuko taabani kabisa!
Vijana wanakwenda kujiunga na kwaya kanisani kwa sababu tu ya kumpata binti
fulani, na wengine hufikia hata hatua mbaya zaidi kwa kuamua kutangaza
wameokoka ili wawe karibu tu na msichana mwenye msimamo anayemcha Mungu kwa
bidii. Mapadre wanasema kwamba hawaruhusiwi kuoa, lakini kutokana na utumwa wa
ngono unaowasakama utakuta ama wanafanya mapenzi na watawa wa kike au kutafuta
wanawake wa pembeni, na tayari kuna mashauri mengi hapa Tanzania ya aina hiyo.
Wapo wachungaji wengi wa Kondoo wa Bwana ambao wamekwishashikwa ugoni ama
wakiwa na wake za watu au wake zao kuwafumania na wahudumu wa kanisa. Wapo
mashekhe ambao pamoja na kuwa na wake wanne kama dini ya Kiislamu
inavyoelekeza, lakini utakuta wana vimada zaidi ya sita mitaani!
"Ni ule upande wenye giza," anasema Weiss.
"Ni upande ule wa kuzifurahisha tamaa zao za mwili ambazo zimetengana na
fikra zao za kawaida, mpaka watakapokamatwa au kufumaniwa au kitu fulani kilete
dunia hizi mbili pamoja na kuleta mgongano."
Kwa upande wa Jerry, utumwa wake wa ngono ulitokana na mambo
mengi: makahaba, picha za ngono, klabu za usiku ambako wanawake wanacheza uchi
na kupendelea kuchukua wanawake tofauti kila siku, ambao kwa Kiingereza
wanaitwa (one-night stands). Lakini utumwa wa ngono haumaanishi kwamba mpaka
ufanye mapenzi na mtu mwingine. Unaweza kuwa unajichua mwenyewe, kutazama picha
na sinema za ngono na mambo mengine.
Baraza la Taifa la Utumwa wa Ngono la Marekani (National
Council on Sexual Addiction) linaielezea hali hiyo kama tabia za mapenzi
zinazozidi na kuhamasisha zaidi.
"Kwamba mtu hatimaye huanzisha uhusiano na tabia hiyo
na wataifanya tabia hiyo katika kuleta madhara makubwa," anasema Dk.
Deborah Corley wa Sante Center mjini Dallas.
Mwathirika "ataendelea kufanya ngono nje" pamoja
na uwezekano wa kuipoteza familia yake au kupoteza kazi. Waathirika mara nyingi
hupoteza maelfu ya fedha katika vitendo vyao, wakiziacha familia zao zikiteseka
kwa kukosa msaada wa kifedha. Nyumba ndogo, kama wenyewe wanavyoita, hutaka
kutimiziwa haja zao haraka sana bila kujali hali ya kipato ya mwanamume husika,
na matumizi yao mara nyingi ni makubwa kuliko ya nyumbani kwako. Waathirika
mara nyingi hupenda kutumia fedha ili kununua mapenzi na kuwaonyesha hao vimada
kwamba wanawajali, lakini wakisahau kwamba huko nyumbani moto unawaka na paka
kalala mekoni! Aibu na hatia huchukua nafasi haraka katika raha zao na baadaye
huanza kujilaumu kwa vitendo hivyo, ambavyo hata hivyo huwa ni vigumu kwao
kuviacha.
"Aibu, hatia ya kufanya mambo niliyokuwa nikiyafanya
vilikuwa havielezeki," anasema Jerry. "Njia pekee ambayo niliifahamu
katika kukabiliana na aibu, hatia na maumivu ni kuendelea kufanya vitendo
hivyo."
"Ukitambua kwamba ni kitu ambacho hupaswi
kukifanya," anasema Browning. "Ukitambua kwamba siyo vizuri kwako -
ni kitu ambacho hakika ni vigumu kukiacha. Najua inaonekana kama uendawazimu,
hakika ni uendawazimu."
Uga wa saikolojia umekuwa mgumu kukubali kwamba utumwa wa
ngono ni uraibu kama ilivyo kwa pombe na dawa za kulevya, lakini wataalamu
wanasema unaweza kubomoa maisha ya watu katika njia na kiwango kile kile kama
pombe na dawa za kulevya.
"Utumwa wa ngono siyo ni kiasi gani au mara ngapi mtu
anafanya mapenzi," anasema Weiss. "Utumwa wa ngono ni kuhusu mtu
fulani kutumia mapenzi ili kukidhi haja zake za kiakili. Wanatumia kama
kimbilio - kupambana na msongo wa mawazo. Wanatumia kupambana na maumivu
yaliyopita. Wanatumia ili wapendwe - wakubalike. Wanakimbilia kwenye ulimwengu
wa kufikirika badala ya ulimwengu halisi. Ni kama kuwa katika ukuta wa kioo.
Naweza kuuona ulimwengu, lakini huwezi kuugusa na wala wenyewe hauwezi
kukugusa. Na hivi ndivyo ulivyo utumwa huu."
"Unataka kuafikia watu, lakini huwezi," anasema
Terry, ambaye zamani alikuwa mwathirika. "Unakuwa umekwama na unajiona
kama maisha yako yamepotea na ubomolewa."
Ni kitu gani kinachosababisha utumwa huu? Kama uraibu
mwingine, wanasaikolojia wengine wanaamini kwamba ubongo wa baadhi ya watu
umeachiliwa huru kwa ajili ya uraibu, iwe pombe, dawa za kulevya chakula au
ngono.
Tatizo jingine kubwa ni unyanyasaji wa kimapenzi, ambao
tutauona huko mbele. Asilimia 82 ya waraibu wa ngono wameshawahi kunyanyaswa
kimapenzi wakati wakiwa watoto. Deborah Corley, mkurugenzi wa The Sante Center
mjini Dallas, Texas, anasema waathirika wanaweza kuwa wanajaribu kutanzua
mkanganyiko unaozunguka manyanyaso hayo.
Tiba za uraibu wa ngono, kama ni nilivyoelezea hapo awali,
zipo za aina nyingi. Kuna Programu ya Hatua-12 kama Sexaholics Anonymous au Freedom
Groups ya Doug Weiss ambazo zinawasaidia waathirika kupambana na tatizo
hilo na kuishi maisha ya uponaji na matumaini.
Baaa ya kujaribu kwa miaka kadhaa uacha baadhi ya utumwa
wake, Dolly Kyle Browning alipata msaada wa kiroho mwaka 1998.
"Niliamka asubuhi moja na kusema, 'Hii inatosha: unatakiwa
kuamua.' Utaendelea kuishi maisha ya kumpendeza Mungu au utaendelea kufanya
mambo yale yale? Punguza," anakumbuka. "Ndiyo, natakiwa kuwa na bwana
mmoja na, unafikiria kuolewa. Bado siyo sahihi."
Na Dolly, kama walivyo watu wengi wenye tatizo kama lake,
walikuja kutambua kuhusu Mungu. "Nilitambua kwamba Alikuwepo muda wote.
Nilikuwa ninafanya mambo mengine tofauti."
"Ni kama ukombozi wa kudumu," anasema Terry.
"Nina matumaini makubwa sana, hata pamoja na hofu ambayo nimekuwa
nikipambana nayo. Ninaona Mungu akiendelea kunivuta nitoke na hakika naona kama
kuna matumaini makubwa ya baadaye nikiwa Naye."
Tutaendelea na mjadala…
Niandikie: brotherdanny5@gmail.com
No comments:
Post a Comment