Ndugu zangu, ni wakati mwingine murua ambao Mungu ametujalia uzima na afya. Hatuna budi kumshukuru Yeye kwa rehema zake kuu zisizo kifani. Nawakaribisha katika ukurasa huu ambapo tutakuwa tukijadiliana masuala mbalimbali yahusuyo uhusiano pamoja na kuyasawiri maisha kwa ujumla.
Wale wasomaji wangu waliobahatika kuvisoma vitabu vyangu vya 'MAHUSIANO, MAPENZI NA MAHABA', 'UTUMWA WA NGONO' na 'SIRI 100 USIZOZIJUA KATIKA MAPENZI' naamini walijifunza mambo mengi yaliyoweza kuwasaidia ama kuanzia uhusiano mzuri au kuimarisha uhusiano waliokuwa nao. Huu ni wakati mwingine mzuri kwenu nyote ikiwa tutashirikiana kwa pamoja katika mijadala na mambo mengine mbalimbali. KARIBUNI SANA!
- Brother Danny
No comments:
Post a Comment