Na
Brother Danny
JOHN alijiingiza
katika tabia za utumwa wa ngono wa aina tatu: 1) kupiga punyeto kila wakati, 2)
kutazama picha za ngono, na 3) majumba ya kufanyia massage. Alikuwa pia ni
mlevi kupindukia. Kutokana na ushauri aliopewa na Joe Zychick, mtaalamu wa
mambo ya saikolojia wa Marekani, alijifunza kwamba haijalishi kama alikuwa
akinywa bia, mvinyo au pombe kali, iwe alikunywa nyumbani, baa, wakati wa
wikiendi au wakati wowote. Alitakiwa kupambana na kuyashinda majaribu yote ya
ulevi.
Tofauti na pombe - tabia za utumwa wa ngono haziko sawa. Watu wengi wanapambana na uraibu wa ngono kama vile ulevi kwa sababu, kwa nchi ya Marekani, Programu ya Hatua-12 ndiyo maarufu. Lakini kwa bahati nzuri kuna tiba ambayo ni nzuri zaidi. Ngoja tuangalie kwa undani na tupate tafsiri ya uraibu ambao unaweza kutumiwa kwenye ulevi na ngono kwa pamoja, na uraibu mwingine: Uraibu ni "shughuli" au "kitu" ambacho mtu hukitumia "kuepuka" kupambana na mawazo au hisia "zisizoburudisha" ambazo zinapaswa kukabiliwa.
Tofauti na pombe - tabia za utumwa wa ngono haziko sawa. Watu wengi wanapambana na uraibu wa ngono kama vile ulevi kwa sababu, kwa nchi ya Marekani, Programu ya Hatua-12 ndiyo maarufu. Lakini kwa bahati nzuri kuna tiba ambayo ni nzuri zaidi. Ngoja tuangalie kwa undani na tupate tafsiri ya uraibu ambao unaweza kutumiwa kwenye ulevi na ngono kwa pamoja, na uraibu mwingine: Uraibu ni "shughuli" au "kitu" ambacho mtu hukitumia "kuepuka" kupambana na mawazo au hisia "zisizoburudisha" ambazo zinapaswa kukabiliwa.
John
alikuwa ameraibiwa na ulevi kwa sababu: badala ya kupambana na hali nzito ya
kijamii, yeye alikunywa sana ili kupunguza fadhaa. Vijinasaba vyake
havikumshawishi afanye hivyo, wala wazazi wake, wala jamii, au hata mpangilio
mbovu wa kemikali. John aliamua kwa hiari yake kufanya hivyo. Badala ya
kutafuta suluhu, yeye aliyasahau kwa kwenda kunywa pombe. Ulikuwa ni uamuzi
wake. John alipokosa kujiamini katika mazingira fulani, alitumia kileo kwa
kuyaondoa mawazo hayo kwa muda. Hakuna mtu aliyemuelekezea bunduki kichwani
mwake; ulikuwa ni uamuzi wake wa hiari. Si yeye tu, wapo watu wengi ambao
wakiwa na matatizo husema, "Ngoja nikanywe pombe nipoteze mawazo"
bila kujua kwamba ulevi ukiondoka tatizo hilo itaendelea kubaki pale pale bila
ufumbuzi tena utakuwa umeongeza jingine kwa fedha ulizotumia.
John
alijikuta akiwa mtumwa wa ngono kwa njia hiyo hiyo. Kushindwa, ghadhabu, hatia,
upweke - mawazo yoyote yasiyoleta faraja - aliamini yangeweza kuondoka kwa
kufanya vitendo vya ngono. Alichagua kufanya vitendo hivyo vya ngono kama tiba
yake. Uchaguzi siyo maradhi hata hivyo, ni uamuzi kati ya chaguzi mbili. John
alichagua kujiingiza kwenye ngono badala ya kukabiliana na maisha halisi.
Hakuna mtu anayeweza kupata raha halisi kutoka kwenye uraibu. Atapata masahibu
kama ya John: faraja ipatikanayo ni ya muda mfupi sana.
Kuna
hatua tatu za mtu kuingia kwenye uraibu: Katika hatua ya mwanzo kabisa, mhusika
huwa anaamini kabisa kwamba uraibu wake unampa raha na faraja ya pekee; Katika
hatua ya kati, mhusika huanza kujiuliza kama uraibu huo ni mzuri au mbaya,
yaani unaleta raha inayotakiwa ama la, na; Katika hatua ya mwisho, mhusika
hutambua kwamba uraibu huo husababisha maumivu kuliko raha, akini bado
ataendelea kushikiliwa na utumwa huo.
Emile,
mke wa John aliwahi kumuuliza mshauri, "John anafahamu kwamba hakupaswa
kuanza vitendo vyake hivyo. Kwa nini anaendelea kuvifanya? Kwa nini
asikome?"
Kama
umeraibiwa, nina imani umeshawahi kujiuliza mwenyewe swali hilo mara nyingi
sana. Jibu lake ni kwamba: Kama kukabiliana na uraibu hakukufanywa kwa usahihi,
hakika utaendelea kuwa mtumwa kwa maisha yako yote, hata kama unajua kwamba
tabia hiyo ni hatari. Watu hawajioni kama hawana matumaini katika kukabiliana
na uraibu mpaka pale watakaposhindwa kuziacha tabia zao. Kama unajiona kwamba
huna matumaini, hebu tutumie kushindwa kwako kama njia nzuri ya kujifunza.
Tazama historia yako ya nyuma utagundua kwamba ulishindwa kukabiliana na uraibu
wako kwa sababu utaratibu ulioutumia uliegemea katika kujirudia kwa tatizo.
Watu wengi hawatambui kwamba wanayarudia matatizo yao, na ninadhani hata wewe
hujui.
Utakuta mtu
amefumaniwa na mke au mumewe aifanya mapenzi na mtu mwingine, au akipiga
punyeto, au akitazama picha na mikanda ya ngono, badala ya kusema tabia hii
sasa basi, na uiacha kabisa kama alivyoahidi wakati alipofumaniwa, siku chache
baaaye atarejea vitendo hivyo hivyo!
Kama wewe
si mtumwa, na una wasiwasi wa ukweli wa mwenzi wako katika kutaka kuacha tabia
yake, muulize maswai yafuatayo: "Kama utapata njia halisi na ya kweli
katika kuachana na tatizo lako, unaweza kuitumia?" "Kama utatakiwa
kufanya kazi kwa bidii, na hiyo ikawa rahisi zaidi kuwa huru kutokana na uraibu
wako, unaweza kufanya hivyo?" Kama mpenzi wako atajibu "ndiyo"
katika masali yote, usikate tamaa. Mungu anamsaidia yule anayejisaidia!
Ngano za uraibu
Tunaishi
katika ulimwengu uliogubikwa na vyombo vya habari. Utapagawisha sana na mawazo
ya uraibu kwa muda mrefu sana, unachotakiwa kufanya ni kuwa makini ili kwamba
harakati zako za kupambana na uraibu wa ngono zisiharibiwe na mambo mengine.
Hebu ngoja tujadili baadhi ya yale yaliyo maarufu: Hakuna kitu kinachoitwa
uraibu chanya kwa sababu uraibu wote unabomoa.
Ngano: Baadhi ya vitu husababisha uraibu: Hii kwa hakika ndiyo
ngano kubwa kuliko zote. Kwa ujumla, utumiaji wako wa kitu fulani
'unaweza' kukufanya ukawa mtumwa. Kwa
mfano; Baada ya kufanyiwa upasuaji wagonjwa wengi huwa wanaruhusiwa kutumia
dawa aina ya morphine. Morphine iko katika mfumo wa heroin, na ina nguvu sana.
Lakini watu wengi ambao wanatumia dawa ya morphine baada ya upasuaji huwa siyo
waraibu. Makumi kwa mamilioni ya watu wanavuta bangi. Wewe unaweza kuwa mmoja
wao. Lakini wapo wachache ambao huitumia katika kiwango ambacho huwadhuru,
unakuwa uraibu. Watu wengi wameshawahi kunywa pombe, wewe unaweza kuwa mmoja
wao, lakini wachache ndio hugeuka kuwa 'walevi-mbwa'. Mamilioni ya watu
wameshawahi kutumia cocaine, crack na dawa nyingine za kulevya.
Tofauti
baina ya mtu aliyeathiriwa na asiyeathiriwa haihusiani na kitu hicho. Tofauti
ipo katika uchaguzi wa kila mmoja kuhusu matumizi ya kitu chenyewe. Angalia
maisha yako. Ulifanya uchaguzi katika matumizi mabaya ya vitu. Vitu haviwezi
vikakuleteza ukafanya vitendo vya uraibu kuliko: Vitabu vinakufanya wewe usome;
Gari zinakufanya wewe uendeshe; Mai yanakufanya uwe na kiu.
Ngano: Uraibu ni kushindwa kiroho: Maadili na uraibu ni
vitu viwili tofauti. Kwa mfano, kumnyanyasa mtoto ni suala la kimaadili na
kiroho kuliko uraibu. Mtu mwenye uraibu wa kula sana hana tatizo la kiroho,
bali ni tatizo kama matatizo mengine.
Ngano: Uraibu unarithiwa: Baadhi ya
"wanazuoni" wanaai kwamba kuna jeni (genes) fulani ya ulevi ambayo
huwafanya watu kuwa walevi wa maisha, tena jeni hizi zinaweza kurithishwa kwa
vizazi vyao. Ukweli unaonyesha kwamba huu ni uongo wa mchana kweupe. Wapo
mamilioni ya watu ambao wazazi wao ni ni walevi wa kupindukia lakini wao hawajawahi
hata kuonja kileo au dawa za kulevya maishani mwao. Wapo mamilioni ya watu
ambao ni walevi mbwa na watumiaji wa awa za kulevya (mateja) lakini wzzi wao
hawajawahi uvigusa vitu hivyo. Hii ni hekaya tu ambayo haina maana yoyote ile
na kama utaisikia huko mitaani ipinge kwa nguvu zote.
Ngano: Uraibu unasababishwa na matangazo ya
ajabu na hatari.
Kwa mfano: Matangazo ya pombe na sigara huwaanya watu walewe na wavute sigara.
Mitandao ya ngono na majarida ya ngono huwafanya watu wawe wazinzi. Filamu
zinawafanya watu watumie dawa za kulevya.
Malumbano
haya yanakufanya ujione kwamba wewe huna uamuzi wa hiari, kwamba wewe ni
matokeo ya soko la vyombo vya habari. Lakini siyo kweli hata kidogo. Hebu ngoja
tuangalie mambo machache: Makumi kwa mamilioni ya watu walikuwa wameathirika na
uvutaji wa sigara na ulevi katika uliokuwa Umoja wa Kisovieti (USSR) na wakati
huo hakukuwa na matangazo yaliyoruhusiwa, yaani serikali ilikuwa imepiga
marufuku matangazo wakati huo wa Ujamaa na Kujitegemea.
Wapo
mamilioni ya watu walioathirika na tabina na vitendo vya ngono ingawa huwa
hawatazami picha za ngono. Wanapenda kitu hlisi au wanatumia fikra zao tu.
Matumizi ya dawa za kulevya yalikuwa yamesambaa hata kabla Hollywood haijaanza
kuonyesha athari za matumizi hayo. Uraibu hausababishwi na sehemu ya soko;
unatokana na uchaguzi wa mtu anayetaka kuyakimbia maisha halisi na kwenda
katika maisha ya kufikirika.
Kwa kuwa
tumeziona hekaya hizi, sasa na tuangalie dalili halisi za utumwa wa ngono.
Dalili za Utumwa
Dalili: Tabia huongezeka wakati muda ukisonga
mbele
Mtu
huanza kujihusisha na utumwa kwa kutumia kitu au shughuli fulani kuyakimbia
masumbufu ya maisha. Kukimbia huku hushindikana kwa sababu utoro huwa
haufanikiwi - na mara zote huharibu matatizo ya maisha. Kisha - na hili ndilo
kosa kubwa zaidi - mtu huyu huamua kujikita zaidi kwenye utumwa huu badala ya
kupambana n tatizo linalomfanya atoroke.
Mzunguko
huu wa utoro-kushindwa-utoro zaidi ndio husababisha tabia za uraibu kuongezeka
kila wakati. Haihusiani chochote na mlingano wa kikemikali au mazingira.
Mhusika huamua kuchagua kutoroka hata kama majiribio ya utoro siku zote
hushindikana. Hatimaye, baada ya muda, waathirika wote hufikia kiwango cha
utumwa uliokithiri na hakiongezeki; hubaki hapo hapo tu.
Jinsi ya kumsaidia mwathirika
Baadhi ya
watu walioathirika hujaribu kukana matatizo yao kama alivyofanya William, mtu
wa makamo na mmoja wa watu waliokuwa wakipewa ushauri naaha na rafiki yangu
Joe. Yeye alisema: "Sijaongeza tabia zangu za uraibu kwa miaka 10, kwa
hiyo sina uraibu."
Kama
unataka kumsaidia ama kumfahamu mtu kama William, muulize swali hili:
"Tabia yako imewahi kupungua katika miaka michache ya kwanza?" Kwa
vyovyote vile atajibu "Ndiyo." Mara mtu wa aina hiyo atakaposema
kwamba tabia yale imepungua au haijaongezeka, usiende mbali sana. Badala yake,
angalia dalili nyingine, kwa sababu tabia nyingine hupungua kulingana na muda
pia. Mtu aliyeathirika kutokana na tabia yake ya kujichua, kama William, hawezi
kupiga punyeto kila mara katika umri wa miaka 35 ya sasa kama alivyokuwa na
umri wa miaka 19. Wanaokula kupita kiasi hupunguza kasi yao kadiri wanavyokua,
lakini bado wataendelea kutumia chakula zaidi. Katika hatua ya mwisho, walevi
wengi hunywa kidogo lakini bado watakunywa katika mtindo ule ule wa utumwa.
Kama tabia inaendelea kadiri muda unavyosonga mbele ni dalili tu, siyo
uthibitisho wa mwisho. Ni kidokezo kikubwa kama kitachanganywa na matatizo
mengine.
Dalili: Tabia inambomoa mtu binafsi
Uraibu
unaegemea zaidi katika matumizi mabaya ya kitu au vitendo vibaya. Matumizi
mabaya ya kitu chochote kile au kitendo chochote kibaya huleteleza matatizo
makubwa zaidi.
Jinsi ya kumkabili mwathirika
Baadhi ya
wathirika wa uraibu huwa wanasema, "Simuumizi mtu yeyote; mimi napata raha
isiyo na madhara." Inaweza kuwa kweli, kwamba kujichua kwako kunakupa raha
bila kumuumiza mtu yeyote, lakini hebu fikiria kama una mke au mpenzi na wewe
ukaendelea na vitendo vyako hivyo, je, unaweza kumpatia mapenzi ya kweli na ya
dhati? Unaweza kuyafurahia mapenzi halisi na yale ya kufikirika uliyoyazoea?
Kifupi hapana, kwa sababu wataalamu wanasema kwamba, kama mtu ameshazoea
kujichua basi akikutana na mwanamke au mwanaume halisi uwezo wake wa kufanya
mapenzi huwa mdogo na mara afikiapo mshindo huchoka na kukosa raha ya kuendelea
na tendo hilo. Aidha, ili afikie mshindo, huwa na kawaida ya kufikiria ni
wakati gani mzuri aliowahi kuufurahia katika vitendo vyake.
Kama
unataka kumkabili mtu aliye na uraibu na anayekana kwamba vitendo vyake viko
sahihi kwa sababu hamuumizi mtu, pitia mambo yaliyoko chini taratibu ukiwa
naye. Usizitumia pointi hizi kwa ajili ya kumshambulia. Tazama orodha kama
nafasi ya kuperuzi na kutambua ukweli wa mambo: Vitendo vya uraibu huchuku muda
mrefu na kugharimu fedha nyingi; Waathirika wengi hawaelewi jinsi wanavyopoteza
muda na fedha nyingi katika vitendo vyao. Wengine wanajua na kutegemea kwamba
wanaweza kuacha vitendo hivyo vinavyowapotezea muda na fedha zao.
Kwa mtu
mwenye uraibu: Kama hujui kiasi gani cha muda na fedha unachotumia kwenye
uraibu wako, sasa ni wakati mzuri kunza kufikiria hilo.
Kwa
mwenza wako:
Kama unajaribu kumkabili mtu mwenye uraibu, mwambie akuandikie kwenye karatasi
kila kitu anachotumia au kugharamia katika tbia hiyo na kuchunguza muda
anaoutumia katika hilo. Mambo haya peke yake yanaweza akamshtua na kumfanya
mwenzi wako akiri kuhusu uraibu wake.
Huharibu
afya ya mwili wa mtu. Uraibu mara nyingi hufanyika mpaka kiwango cha kuchoshwa
kwa mwili. Watu wengi wenye matatizo haya huwa hawaelewi uchovu mwingi wa mwili
unaosababishwa na tabia za uraibu mpaka watakapoiacha tabia hiyo.
Kwa mtu
mwenye uraibu:
Wakati mwingine utakapojisikia kuchoka sana mwili, fikiria kuhusu mara ya
mwisho ulipofanya vitendo vya uraibu. Ilichangia kutokana na uchovu huo? Ndicho
kilikuwa chanzo kikubwa cha uchovu?
Kwa
mwenza wako:
Waathirika wengi wanaokana matatizo yao watapinga na kudai kwamba uraibu wao
hupunguza msongo wa mawazo na kuwaongezea nguvu. Huu unaweza kuwa utetezi mgumu
kuushinda. Hata hivyo, waathirika wote huwa wanachoka mara wanapomaliza vitendo
vyao vya uraibu. Mulize mwenza wako, "Unajisikiaje mara unapomaliza
kitendo chako (kama kujichua, kuvuta sigara, bangi, dawa za kulevya, kutazama
picha za ngono, kuzini, n.k.)?" Inawezekana hicho ndicho kitu pekee
unachokihitaji.
Kama
atakataa kwamba huwa hafanyi vitendo hivyo, basi hii inaonyesha kwamba tatizo
ni kubwa zaidi. Badala ya kumfanya akiri kuhusu uraibu wake, muulize,
"Unataka kusema kwamba huwezi kuongeza nguvu na kukabiliana na msongo wa
mawazo katika njia za kawaida? Haitakuwa vizuri kwako kutegemea fikra zako
mwenyewe badala ya vitu vingine vya kufikirika, kula sana, kufanya ngono kwa
lazima?" Hiyo inaweza kumsaidia kuelewa kwamba kweli yeye ni mtu tegemezi.
Dalili: Tabia hiyo huleta athari kwa wengine
Baadhi ya
kadhia hizi zinaweza kuwa zimezoeleka miongoni mwa jamii yetu: Henry alivunja
ahadi na marafiki, familia, na wafanyakazi wenzake kutokana na vitendo vya
uraibu; Watoto wa Maria kwa bahati mbaya walijikuta wakimfumania mama yao
akitazama mikanda ya video ya ngono usiku wa manane huku akiwa anajiingiza
vidole sehemu za siri; Familia ya Eric ilikuwa inaishi kwa mlo wa kubahatisha
kutokana na yeye kutumia fedha nyingi kwa makahaba na wanawake wengine; Badala
ya ndoa ya upendo na mahaba ambayo Doreen aliitegemea, alikumbana na mateso makubwa
kutoka kwa mumewe Damas ambaye aliweza kukaa miezi kadhaa bila kuanya naye
tendo la ndoa, hali iliyomlzimisha dada huyo atafute bwana wa pembeni kukidhi
haja zake za mwili; Sylvia alitekeseka sana moyoni kwa miaka mingi kwa sababu
mumewe Jonathan alihusudu sana na kutumia muda mwingi katika kupiga punyeto na
kutazama picha za ngono kuliko alivyofanya naye mapenzi; Sally hakufanya
mapenzi kwa miaka mitano na hakuelewa kwamba hali hiyo ilitokana na uraibu wa
ngono wa mumewe, yeye alifikiri kwamba tatizo liko kwake; Tatizo jingine la
kutisha, Hamisi alipata ugonjwa wa zinaa kutokana na tabia ya uzinzi ya mumewe;
Kwenda matembezini na mumewe yalikua kama mateso makubwa kwa Mwasiti kwa sababu
mumewe Juma alikuwa akiwakodolea macho wanawake kana kwamba anataka kuwavua
nguo; Hassan aliwanyanyasa sana akina dada waliokwenda kuomba kazi ofisini
kwake na kukataa kufanya naye mapenzi kama moja kigezo cha kuajiriwa naye; n.k.
Kwa
ujumla yapo mambo mengi sana ndani ya jamii yetu ambayo yanatokea siku hadi
siku, na yote ukiyatazama utaona kwamba ni uraibu tu. Hivi sasa dunia
imegubikwa na maradhi mabaya ya UKIMWI, na ukiangalia kwa undani watu wengi
wanapata maradhi haya wakiwa nani ya ndoa, tena wameishi kwa miaka mingi sana.
Sasa jiulize, wamepataje maradhi hayo kama siyo mmoja wao kutokuwa mwaminifu?
Jibu nadhani kila mmoja wetu analo kichwani mwake, au siyo?
Katika
matukio mengine, mtu anaweza kuonekana mnyama ndani ya jamii kwa utumwa wake wa
ngono kiasi cha kubaka watoto kama Maumba alivyofanya, au kuhusudu kuchungulia
watu wakifanya mapenzi kama Ally alivyofanya, au mpendna mashoga kama David
afanyavyo. Lakini matatizo haya siyo mengi kama yale mengine.
Watu
wengi wenye uraibu, kama ni wastaarabu na wanawajali wenzao na uhusiano wao,
watakiri kuhusu madhara waliyowasababishia wengine. Kama unakabiliana na
mwathirika ambaye hayuko tayari kukiri madhara aliyowasababishia wengine,
usikae kimya na badala yake jitahidi mpaka akiri, lakini katika hili lazima
ujindae na wakati mgumu zaidi. Unapaswa kukusanya taarifa zako pamoja kabla ya
kumkabili. Angalia katika kila upenyo ambao mwenzi wako anaweza kuutumia.
Ninaamini mpaka hapa unajua mambo ya msingi unayopaswa kumweleza. Tazama namna
ambavyo wewe utakwenda kuitikia, kama utashindwa kuja na maelezo yanayofaa,
basi mweleze, "Sawa, huu ndio ukweli wenyewe kuhusu matatizo yako. Siwezi
kubishana na wewe kuhusu hili, unaweza kufanya au kuacha." Kwa watu ambao
ni wagumu kukubali, nafasi pekee ambayo unaweza kuitumia ni kuwaambia, anya
hivi au acha.
Dalili: Tabia hii hubadili hisia
Watu
wanapotumia dawa za kulevya kwa ajili ya kujisikia vizuri (wengine hujiona kama
wanaelea angani) au wanapokunywa pombe kwa minajiri ya kupoteza mawazo,
wanajaribu kubadili hisia zinazowakera badala ya kukabiliana na tatizo husika.
Wengine wanatumia dawa mbalimbali za hospitali, mapenzi, na ama kula sana
katika namna ile ile ya kutoroka matatizo.
Watu
walioathirika sana na tabia hii watakiri kwamba wanatumia tabia hii kubadili
hisia zao. Lakini baadhi wanaweza kusema pia, "Kwani kuna ubaya
gani?" Swali hili litakuwa na tafsiri za aina mbili kwa sababu mtu huyo
anaweza kumaanisha: Kwani haifai kimaadili kubadili hisia zako? Na/au Kwani
itaniumiza kama nitazigeuza hisia zangu?
Njia
nzuri zaidi ya kujibu swali hilo "Kwani kuna ubaya gani?" ni,
"Siyo vibaya kimaadili wala siyo dhambi kukiri. Ni kwamba haifai kwako.
Hakika inaweza kukuumiza tabia hiyo. Mara nyingi ni vizuri kwako kukabiliana na
hisia zako badala ya kuzikimbia."
Kuna
baadhi ya waathirika ambao siyo rahisi kukiri kwamba wanakuwa na tabia hiyo kwa
ajili ya kubadili hisia zao. Hili ni swali unalopaswa kuwauliza: "Kama
wewe siyo mtumwa, basi kwa nini (unalewa, unakula kupita kiasi, unazini na
kuhusudu ngono, nk.) kila unapokuwa na msongo wa mawazo, upweke, hati, hofu,
kushindwa, kutwezwa au hisia nyingine zisizo njema?" Kama watakana, basi
wakumbushe nyakati ambazo ulishawahi kuwaona wakiwa katika tabia hizo katika
harakati zao za kutoroka kukabiliana na maisha halisi.
Dalili: Mwathirika hujaribu kuacha
Mkanganyiko,
hatia, fadhaa, hofu, aibu, na mambo mengine huambatana na uraibu kwa sababu ni
njia za asili za kumweleza mwathirika, "Kabiliana na tatizo lako au
ukitaka endelea kujiona mnyonge mpaka ufanye matendo hayo." Katika hatua
ya mwisho ya uraibu ambapo itaonekana kwamba uraibu lilikuwa ni kosa kubwa
sana, waathirika wengi hutumia sehemu kubwa ya maisha yao yaliyosalia: Kujaribu
kuacha; au, Kudhani kwamba wanaweza kuacha; au Kujiandaa kwa jaribio lao
linalofuata la kuacha.
Nini cha pekee kuhusu utumwa wa ngono?
Hatukuzaliwa
na tamaa za asili za kulewa pombe, kutumia uraibu wa dawa za kulevya na
mihadarati au kuharibu fikara zetu na matibabu ya dawa za hospitali. Tumezaliwa
na tamaa njema za asili kuhusu mapenzi, kazi na chakula.
Uraibu
ambao shina lake ni msukumo wa kiasili unapaswa kutibiwa tofauti n uraibu
unaotokana na mambo yasiyo rasmi. Sababu zake ni hizi: Msukumo wa kiasili
unapaswa kutekelezwa. Kama utajaribu kuliondoa tatizo la uraibu unaotokana na
tamaa za asili, utakuwa unapambana na asili. Kuishi maisha bila ya kufanya
mapenzi wala kazi humfanya mtu achanganyikiwe, afadhaike na ahuzunike. Kama
utaacha kula kabisa hakika utakufa. Na ingawa baadhi ya watu wanasema kwamba
kuka bila kufanya mapenzi hakuna madhara, mimi napingana nao, kwa sababu watu
wengi ambao wameamua kuishi maisha ya useja na ukapera wana matatizo mengi ya
kisaikolojia.
Dalili 10 kwamba wewe ni mtumwa wa ngono
1. Unafanya mapenzi na zaidi ya mtu mmoja kwa
mwezi.
2. Unajichua kila mara (mara 3 hadi 25 kwa
wiki).
3. Unawageuza wapenzi wako kama chombo tu
badala ya "kufanya nao mapenzi."
4. Una zaidi ya mikanda 10 ya video za ngono au
majarida ya ngono nyumbani kwako.
5. Unafanya mapenzi ya kufikirika.
6. "Unazunguka," lakini unaweza
kusema 'watu wanakutazama....'
7. Unafanya mapenzi katika sehemu za hatari.
8. Unaendelea kupigania "mapenzi
makubwa"
9. Unafikiria na/ama kuzungumzia sana ngono.
10. Unadhani kwamba unaweza kuwa bingwa wa
ngono.
No comments:
Post a Comment