Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 20 October 2013

TULIVYO WASAHAULIFU... TUMEYASAHAU MAUAJI YA MWANGOSI

Polisi anayedaiwa kumuua Daudi Mwangosi akisubiri kuapa kwa Mlinzi wa Amani.

Daudi Mwangosi enzi ya uhai wake.
Wafuasi wa CHADEMA wakiwa kwenye ofisi cha Nyololo.
Maandamano, Fanya Fujo Uone (FFU) nao wameweka bango lao Nyololo.
Land Cruiser ya Michael Kamuhanda ikiwa mbele ya gari la vijana wake wa FFU, Jumapili Septemba 2, 2012.
Wafuasi wa CHADEMA ndani ya gari.
Vijana wa Kamuhanda wameanza kazi.
"Piga, kong'ota, lipua.. huyu ana kiherehere..." Ndivyo wanavyoelekea kusema askari hawa wakimshambulia Mwangosi huku askari Pasficus (kushoto) akilipua bomu la kivita.
Kazi imekwisha Nani abaki?!. Umebaki mzoga wa aliyekuwa Mwangosi. Lakini OCD wao naye hoi. Tumegeuka wanyama Tanzania.
Dk. Slaa akiweka shada la maua kwenye kaburi na Mwangosi huko Tukuyu.

Sisi Watanzania kweli tu wasahaulifu. Tumesahau kifo cha Mwangosi, tumesahau hata kesi inayoendelea (kama ipo) na hakuna anayejua itatajwa lini.

Nguvu ya kesi ile ilikuwa wakati ule mwaka 2012, lakini sasa tumesahau. Wanahabari, baada ya kupata misukosuko kila kesi hiyo ilipotajwa, sasa hakuna anayeifuatilia. Nguvu yake imekwisha.
Wanasiasa na wanaharakati wamekaa kimya, hakuna anayefuatilia. Wengine wameifanya kesi hiyo ama kifo cha Mwangosi kwa ujumla, kama mtaji wao wa kisiasa. Ni aibu!
Anyway, wacha tusubiri tuone.

Mbega.

No comments:

Post a Comment