Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 27 October 2013

VIGOGO WA CCM WAPATA SHAHADA CHUO KIKUU HURIA


Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Idara ya Itikadi na Uenezi CCM, Makao Makuu, Daniel Chongolo, akipongezana na Mjumbe wa NEC ya CCM, Asha Abdallah Juma baada ya wote kutunukiwa shahada zao katika mahafali ya 25 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), yaliyofanyika Oktoba 27, 2013 Bungo, Kibaha mkoa wa Pwani.  Chongolo ametunukiwa shahada ya kwanza ya Mawasiliano ya Umma na Asha shahada ya pili ya Biashara. Katikati ni Kada wa CCM, Rachel Kyala ambaye pia ametunukiwa shahada ya Mawasiliano ya Umma.(Picha na Bashir Nkoromo)
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk. Asha-Rose Migiro, akimpongeza Kada wa CCM, Asha Abdallah Juma, baada ya kumtunuku shahada ya pili ya Biashara, katika mahafali ya 25 ya chuo hicho, yaliyofanyika jana, Oktoba 27, 2013, Makao Makuu ya OUT, Bungo, Kibaha mkoa wa Pwani. Kushoto ni Makamu Mkuu  wa Chuo hicho, Profesa Tolly Mbwette. Asha ambaye sasa ni Mjumbe wa NEC CCM, amewahi kuwa Waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na pia Katibu wa NEC, Oganaizesheni. (Picha na Bashir Nkoromo).

No comments:

Post a Comment