Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongea
na Bi Sarah Mageni Sanga, mlemavu ambaye Rais alimpa pikipiki ya Bajaji
pamoja na mtaji wa pesa taslimu wa shilingi milioni mbili Oktoba 28,
2009 baada ya kuguswa na mkasa wa maisha ya mkaazi huyo wa kijiji cha
Lupalilo wilaya ya Makete mkoa wa Njombe alipomuona akohojiwa katika TV
na kueleza kuwa maisha yake ni magumu mno baada ya ndugu na jamaa zake
wote kuteketea kwa maradhi ikiwa ni pamoja na UKIMWI. Pichani Bi Sanga
akimshukur Rais kwa msaada huo ambao amesema umebadili kabisa maisha
yake kwani sasa anaishi kama mtu yeyote kijijini hapo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia ubora wa
shati lililotengenezwa na wanafunzio wa Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA
cha Wilaya ya Makete baada ya kukifungua rasmi chuo hicho mwishoni mwa
juma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe
kufungua rasmi Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA cha Wilaya ya Makete
mwishoni mwa juma.
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akiongeana wananchi wa kijiji cha Ivalalila wilayani Makete
baada ya kuweka jiwe la msingi la kituo cha afya cha kijiji hicho
mwishonimwa juma.PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment