Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 27 October 2013

BOMU LAUA WAALIKWA 18 WALIOKWENDA HARUSINI



SHAMBULIZI la bomu la pembezoni mwa barabara katika jimbo la Ghazni, kusini mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, limeua watu 18 waliokuwa wanakwenda kuhudhuria sherehe ya harusi, maofisa wameeleza.

Wamesema karibu wote waliokufa ni wanawake na watoto waliokuwa kwenye basi dogo ambalo limeteketezwa.
Wapiganaji wa Taliban wamekanusha kuhusika na shambulio hilo.
Wananchi wa Afghanistan mara nyingi wamekuwa wakiuawa na mabomu ya pembezoni mwa barabara yanayorushwa na wapiganaji wa Taliban ambao wanawalenga wanausalama na maofisa.
Mwezi Juni, NATO walikabidhi ulinzi kwa nchi nzima ya Afghanistan kwa vikosi vya Afghanistan, lakini askari 97,000 wa NATO bado wameendelea kuwepo.
Shmabulio hilo la Jumapili limetokea katika eneo maskini la Pashtun kaskazini mwa jimbo la Ghazni, alisema mtangazaji wa BBC nchini Afghanistan David Loyn.
Basi hilo dogo, likiwa limejaza watu waliokuwa wanakwenda harusini, limeteketezwa kwa bomu.
Wanawake 14, wanaume watatu na mtoto mmoja waliuawa, naibu mkuu wa polisi Kanali Asadullah Ensafi alikaririwa akisema.
Ni watu watano tu kati ya 23 waliokuwa ndani ya basi hilo, wote wakiwa wanawake, wanadaiwa kunusurika. Wawili wako katika hali mbaya.
Wilaya ya Ander, ambako shambulio hilo limetokea, iliwahi kuelezwa na NATO kwamba ni eneo hatari zaidi jimboni Ghazni.
Hata hivyo, msemaji wa Taliban amesema hawahusiki na tukio hilo, na kwamba hawakuwa na operesheni zozote wilayani humo.

No comments:

Post a Comment