Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa barabara ya lami ambayo
inamaliziwa kujengwa yenye urefu wa mita 600 iliyopo katika Kata ya Mjini,
Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Barabara hiyo imegharimu zaidi ya Sh75
milioni. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja na
kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni mwake.
Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk Emmanuel Nchimbi (aliyevaa miwani) akiwa na Diwani wa Kata ya Mjini ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma, Joseph Fuime (kulia kwa Dk
Nchimbi) wakipita kwa furaha barabara aliyoizindua Dk Nchimbi mjini Songea
mkoani mjini Songea leo. Barabara hiyo yenye kiwango cha lami ina urefu wa mita
600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni, pia mbunge huyo ameweka jiwe la
msingi katika ofisi ya Kata ya Mateka. Dk Nchimbi pia anatarajiwa kuzindua
ujenzi wa mabweni ya sekondari pamoja na nyumba za walimu.
Sehemu
ya mamia ya wananchi wa Kata ya Mjini, Manispaa ya Songea wakiwa tayari kwa
kumsikiliza Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Dk Nchimbi baada ya kuzindua barabara
yenye kiwango cha lami yenye urefu wa mita 600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75
milioni, pia mbunge huyo ameweka jiwe la msingi katika ofisi ya Kata ya Mateka.
Dk Nchimbi katika ziara yake ya siku tano jimboni humo, pia anatarajiwa
kuzindua ujenzi wa mabweni ya sekondari pamoja na nyumba za walimu.
Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk Emmanuel Nchimbi akilifungua jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Kata ya
Mateka iliyopo mjini Songea mkoani Ruvuma. Dk Nchimbi pia alizindua barabara
yenye kiwango cha lami yenye urefu wa mita 600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75
milioni iliyopo katika Kata ya Mjini, Manispaa ya Songea. Dk Nchimbi yupo mjini
Songea katika ziara ya siku tano ya kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo
jimboni humo.
Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na mamia ya wananchi wa Kata ya Mateka, Mjini
Songea baada ya kuizindua barabara yenye kiwango cha lami yenye urefu wa mita
600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni iliyopo katika Kata ya Mjini na
baadaye kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya Kata ya Mateka. Dk Nchimbi katika
ziara yake ya siku tano jimboni humo, pia anatarajiwa kuzindua ujenzi wa
mabweni ya sekondari pamoja na nyumba za walimu.
No comments:
Post a Comment