Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha
akitia saini kitabu cha mahudhurio, alipohudhuria kuuaga mwili wa marehemu
Luteni Rajabu Mlima kwenye kambi ya Jeshi la Ulinzia la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
Waziri Nahodha akisalimiana na maafisa na viongozi wa JWTZ
Waombolezaji waliohudhuria kuuaga mwili wa marehemu.
Askari wakiuteremsha mwili wa marehemu baada ya kuwasili.
Askari wameubeba mwili wa marehemu.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akitoa
heshima za mwisho.
Mchumba wa marehemu akimliwaza mwanae ambaye pia ni motto wa marehemu
wakati wa kuuaga mwili kwenye viwanja vya Lugalo. Picha
zote na Hussein Makame, Ofisa Habari Idara ya Habari (MAELEZO).
Na Hussein Makame, MAELEZO
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha
ameongoza mamia ya waombelezaji kuuaga mwili wa Afisa wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) marehemu Luteni Rajabu Mlima aliyefariki Oktoba 27
mwaka huu wakati akitekeleza jukumu la kulinda amani nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Akizungumza na wanahabari katika viwanja vya Kambi ya Lugalo ya JWTZ
jijini Dar es Salaam baada ya kuuuaga mwili wa shujaa huyo, Waziri Nahodha
aliseka kuwa Tanzania haitaacha kutekeleza majukumu yake ya kulinda amani
nchini DRC hadi hapo iatakapohakikisha kwamba nchi hiyo imekuwa na amani.
Hata hivyo, alisema kuwa kufuatia kumpoteza shujaa huyo Serikali
kupitia Wizara yake itaendelea kuwa bega kwa bega na familia ya marehemu katika
kipindi hiki cha majonzi kutokana na kumpoteza mpendwa wao.
Akitoa salamu za rambirambi kutokana na msiba huo, Mnadhimu wa Jeshi
hilo Luteni Genarali Samuel Ndomba alisema kuwa marehemu Luteni Mlima alifariki
baada ya kupigwa risasi wakati akilinda raia wa DRC wasidhuriwe na mapigano
kati ya Jeshi la nchi hiyo na waasi wa M23.
Luteni Generali Ndomba alisema shujaa huyo alifariki saa 5:08 asubuhi
jumapili iliyopita wakati kikundi chao kilipokuwa kikiwalinda raia wa DRC
kwenye mji wa Kiwanja karibu na miliya ya Gavana iliyoko nchini humo.
Aliongeza kuwa marehemu Luteni Mlima alikuwa mmoja wa Maafisa katika
kikundi cha JWTZ nchini DRC ambacho kinashiriki katika operersheni ya kulinda
amani kikiwa ni sehemu ya Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa
(MONUSCO).
“Marehemu wakati wa uhai wake na hasa katika operesheni hii
inayoendelea nchini humo alifanya kazi zake kwa ujasiri na uhodari wa hali ya
juu ambao kwa kiasi kikukbwa umechangia kuleta heshima na sifa ambazo jeshi na
nchi yetu imepata katika nyanja za ulinzi wa amani Afrika.Tutaendelea
kumkumbuka kwa mchango wake kwa Jeshi na Taifa letu” alisema Mnadhimu Mkuu huyo
wa JWTZ.
Aliongeza kuwa “Kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi, Maafisa na watumishi wa
umma natoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na
marafiriki wa karibu kwa masiba huu, tunaungana na familia katika kipindi hiki
cha maombolezo na wakati huo tukiendelea kumuomba Mwenyezi Mungu awape faraja
na ustahamilivu katika ki[phiki kigumu na majonzi.Mwenyezi mungu ailaze mahali
pema roho ya marehemu Luteni Rajabu Ahmed Mlima, Amen”
Naye kaka wa marehemu Dk. Azizi Mlima alisema kuwa kwa niaba ya
familia wanashukuru sana JWTZ na Serikali kwa ujumla kwa kumpokea ndugu yao na
kwa shughuli nzima za mazishi yake hasa ikizingatiwa kwamba amefariki wakati
akitekeleza majukumu ya Kitaifa na Kimataifa ya kuleta amani katika ukanda wa
Maziwa Makuu.
Akizungumza kwa majonzi mchumba wa marehemu Luteni Asia Hussein alisema
amepokea kwa masikitiko msiba huo kwani walikuwa wanatarajia kufunga ndoa mwishoni
wma mwaka huu.
Pamoja na viongozi hao wa Serikali, pia Makatibu Wakuu wa Wuzara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na wizara nyingine, Mabalozi na Maafisa
wastaafu wa Jeshi hilo walihudhuria kuuaga mwili wa marehemu kwenyekambi ya
Lugalo.
Marehemu baada ya kuagwa katika viwanja hivyo alipelekwa nyumbani kwa
familia yake Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambapo familia ilimuaga kabla ya
kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam huku akiwa ameacha mtoto
wa kike mwenye umri wa miaka 10 Zuhrat.
No comments:
Post a Comment