Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakikagua chai ikichambuliwa
katika kiwanda cha chai cha Ikanga, Njombe, ikiwa ni sehemu ya
sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe Ijumaa Oktoba 18, 2013.
Rais Jakaya Kikwete akizindua kiwanda kipya cha chai cha Ikanga, Njombe,
ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi rasmi wa
mkoa mpya wa Njombe Ijumaa Oktoba 18, 201312. PICHA NA IKULU
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S
OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O.
BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais Kikwete azindua Kiwanda
cha Chai Mkoani Njombe
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Ijumaa, Oktoba 18, 2013, amezindua rasmi Kiwanda cha Kusindika Chai cha Ikanga,
Tarafa ya Lupembe, Wilaya ya Njombe
katika Mkoa Mpya wa Njombe.
Kiwanda
hicho kinachomilikiwa kwa asilimia 25 na wakulima wa chai wa Lupembe ni
ukombozi mkubwa wa wakulima wa Tarafa ya Lupembe ambao wamekuwa wanakabiliwa na
ukosefu wa sehemu ya kuuza chai yao.
Ufunguzi
wa kiwanda hicho cha Ikanga Tea Factory kinachomilikiwa na Kampuni ya Ikanga
Tea Factory Limited ni utekelezaji wa ahadi ya Mgombea Urais wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati anafanya kampeni ya Urais katika
Tarafa ya Lupembe mwaka 2010. Ni kiwanda kipya zaidi na bora zaidi cha
kusindika chai katika Tanzania.
Ujenzi
wa kiwanda hicho ulianza mwishoni mwa mwaka 2010 baada ya Serikali ya Rais
Kikwete Mei mwaka huo huo kuiomba Kampuni ya Mufindi Tea and Coffee Limited
(MTC) kujenga kiwanda cha kusindika chai ya wakulima ambayo sehemu yake kubwa
ilikuwa inapotea na kuoza kwa sababu ya ukosefu wa kiwanda.
Ili
kufanikisha ujenzi wa kiwanda hicho, MTC iliunda kampuni mpya ya Ikanga Tea Company
Limited Septemba 2010. Kampuni hiyo ni ubia kati ya MTC na wakulima wa chai wa
Lupembe ambao wanamiliki asilimia 25 za hisa za kiwanda hicho kupitia umoja wao
wa Lupembe Tea Farmers Trust.
Uzinduzi
wa leo ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa kiwanda hicho. Chini ya awamu hiyo ya
kwanza yenye uwezo wa kusindika tani 1,800 za chai kwa mwaka kwa kutumia njia
moja ya uzalishaji iliyokamilika Juni
mwaka jana kwa gharama ya Sh. bilioni
3.75. Awamu ya pili ambayo inaendelea kujengwa, itagharimu Sh. bilioni
1.48 na ikikamilika kiwanda kitakuwa na uwezo wa kusindika tani 3,500 na awamu
ya tatu na ya mwisho itagharimu Sh.bilioni 1.5 na kukamilika kwa awamu hiyo kutakiwezesha
kiwanda kusindika tani 5,000 za chai kwa mwaka.
Chini
ya uendeshaji wa Kiwanda hicho, chai yote ya wakulima inanunuliwa kwenye vituo
maalum na kusafirishwa kwenda kiwandani na magari ya Kiwanda. Wakulima pia
wanapewa mbolea kwa mkopo na wakulima wote wa chai inayochukuliwa na kiwanda
hulipwa kila mwezi kwa bei iliyopangwa na Bodi ya Chai Tanzania.
Miongoni
mwa mipango ya Kampuni ya Chai ya Ikanga ni kununua angalau hekta 600 za ardhi
ili nayo ianze kulima chai ili kuongeza kiwango cha chai kinachozalishwa katika
eneo la Lupembe na ukamilishaji wa shule kwa ajili ya watoto wa wakulima wa
eneo la Lupembe.
Rais
Kikwete amezindua Kiwanda hicho ikiwa ni shughuli ya kwanza katika shughuli
nyingi ambazo atazifanya wakati wa ziara yake ya siku sita katika Mkoa wa
Njombe kuzindua na kukagua shughuli za maendeleo. Miongoni mwa shughuli hizo
itakuwa ni kuuzindua rasmi Mkoa wa Njombe.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
18 Oktoba, 2013
No comments:
Post a Comment