*Mwanamke mtumiaji aliyeolewa anaua watoto 12 kila mwaka bila kujielewa
Na Daniel
Mbega
KUPANGA
uzazi kwa njia za kisasa ni kuamua juu ya mpishano wa miaka ya kuzaliwa watoto
na juu ya idadi ya watoto ambo familia inapenda kuwazaa, ambapo njia hizo
hutumia dawa (kemikali) zilizomo katika vidonge vya majira (pills), vitanzi (loops), vipandikizi (norplant
implant), sindano ya Depo Provera,
lunelle, emergency contraceptives, quinacrine, povu, mafuta, vidonge
viyeyukavyo ukeni, kondomu na kutoa mimba.
Afya ya uzazi (reproductive health) humaanisha kuwafanya wanawake wenye ndoa na wasio na ndoa na wasio na ndoa, hata wanafunzi mashuleni, kufurahia ngono bila kuwa na wasiwasi wa kupata mimba na magonjwa ya zinaa, ukiwemo UKIMWI, kwa kutumia njia hizo za kisasa.
Afya ya uzazi (reproductive health) humaanisha kuwafanya wanawake wenye ndoa na wasio na ndoa na wasio na ndoa, hata wanafunzi mashuleni, kufurahia ngono bila kuwa na wasiwasi wa kupata mimba na magonjwa ya zinaa, ukiwemo UKIMWI, kwa kutumia njia hizo za kisasa.
Watafiti
mbalimbali wa mambo ya uzazi nchini Marekani wamebaini kwamba, dawa au chachu
bndia za uzazi wa mpango zinapoingia mwilini huighilibu chachu halisi ya
mwanamke itolewayo katika viungo vya uzazi kwa kuchochewa na tezi la pituitary (pituitary gland) na hivyo hufanya mayai y mwanamke yasikomae;
hupunguza uwezo wa kusafirisha mimba katika mirija ya uzazi; huharibu ngozi
nyororo ya tumbo la uzazi kwa namna kwamba mimba iliyotungwa hushindwa
kujipandikiza; hutoa mimba kutokana na mimba hiyo kushindwa kukaa na kukua
katika tumbo la uzazi; hufanya ute wa mwanamke kuwa mzito sana na hivyo kuzuia
mbegu za kiume (semen) kupita
kuelekea tumbo la uzazi la mwanamke.
Uwepo wa
binadamu mpya hutegemea kuwepo kwa muunganiko halisi na bayana wa mbegu ya
baba, yai la mama na pumzi ya Mungu, na baada ya muunganiko huo uhai unbeba
sifa ya kuwa kitu cha pekee na cha thamani kubwa.
Tunapotafakari
umuhimu na upekee wa uhai wa binadamu, hatuwezi kufumbia macho vitu
vinavyoharibu au kuua uhai huo, kwani sumu zote zinazotumika katika kile
kinachoitwa 'kupanga uzazi kwa njia za kisasa' huondoa uhai na huharibu afya.
Dawa hizo
zinazidi kuingizwa hapa Tanzania na kutekelezwa kwa agizo la Umoja wa Mataifa
wa Mfuko wa Idadi ya Watu Duniani chini ya mwavuli wa Afya ya Uzazi (Reproductive Health), Haki ya Ujinsia (Sexual Rights), Ujinsia (Sexuality) na Uzazi wa Mpango (Family Planning).
Kwa mujibu
wa Dk. Bogomir Kuhar, vita dhidi ya uhai wa watoto kupitia njia za kisasa za
kupanga uzazi husababisha vifo vya watoto kati ya milioni 8.1 na 12.75 kila
mwaka katika mataifa ya Ulaya na Marekani kwa kuwa dawa hizo zina chachu
zinazoua uhai mpya kabla mwanamke hajajua kama ana mimba.
Utafiti
huo unaeleza kwamba, mwanamke anayetumia njia hizo za kisasa ambaye hajaolewa
kwa wastani anaua watoto watatu kila mwaka wakati yule aliyeolewa ambaye
anatumia njia hizo anaua watoto 12 kila mwaka bila mwenyewe kujielewa.
Hii
inatokana na ukweli kwamba, madawa hayo hupoteza mwelekeo wa mzunguko wa siku
za hedhi za mwanamke, ambapo wapo ambao wanaweza kupata siku zao muda mrefu
zaidi bila kuwa na uwiano mzuri wa mwezi hadi mwezi na wengine hutokwa damu
kidogo katika siku zao au wasipate siku zao kabisa.
Wanawake
wanaotumia dawa hizo wanakabiliwa na madhara mengi sana yakiwemo saratani ya
ziwa (breast cancer), ngozi (skin cancer), mji wa uzazi na kokwa (Uterine and Ovary cancer) pamoja na
saratani ya mlango wa uzazi (cervical
cancer); magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, magonjwa ya ini, kiharusi,
kupofuka macho, utasa wa muda au wa kudumu, kupata hedhi bila mpangilio, mimba
nje ya mji wa uzazi, kunyonyoka nywele, kuota nywele kifuani na kuota ndevu.
Katika
hali nyingine, wanawake wanaotumia njia hizo hukosa hamu ya tendo la ndoa na
pindi wanapokutana na wenzi wao huwalazimu kutumia muda mwingi 'kuhamamsishana'
kabla ya kukutana kutokana na uke kuwa mkavu kufuatia ute wa asili kutokuwepo.
Aidha,
baadhi ya wanawake hukonda na wengine hunenepa sana, huku wakieleza kwamba
kunenepa huko kuntokana na dawa hizo 'kuwapenda' wakati ni maradhi ambyo wao
wenyewe hawajui kama wanayo na ndiyo chanzo cha kupata kiharusi na magonjwa ya
moyo kutokana na damu kuganda mwilini badala ya kutoka kila mwezi kama ilivyo
asili yake.
Utafiti
uliofanywa hapa Tanzania na shirika moja lisilo la kiserikali la Pro-Life
kuanzia mwaka 1996 hadi 2001, umeonyesha kwamba wanawake 578 kati ya 600
waliojitokeza kujieleza wenyewe ambao wamekuwa wakitumia vidonge (oral contraceptives) na sindano za Depo Provera (DMPA-Depo medroxyprogesterone acetate) wamekumbwa na matatizo hayo.
Depo Provera ambayo katika miaka ya 1950
ilitengenezwa kama tiba ya saratani ya tumbo la uzazi (Uterine Cancer), hatimaye mwaka 1992 ilithibishwa nchini Marekani
kwa matumizi ya uzazi wa mpango ambapo mwanamke hudungwa miligram 150 kila
baada ya miezi mitatu.
Lakini
mwezi Juni 1993 Idara ya Afya ya Canada ilizuia matumizi ya dawa hiyo kwa
maelezo kuwa siyo salama kwa afya ya watumiaji. Hata hivyo, hadi mwaka 1996
tayari dawa hiyo ilikuwa imetumiwa na wanawake milioni 30 katika zaidi ya nchi
90 duniani na hasa zinazoendelea kama njia ya kupanga uzazi, yaani kudhibiti
ongezeko la watu, hasa baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kufanya majaribio
kwa wanawake wa nchi zinazoendelea kama vile Kenya, Mexico, Thailand na New
Zealand. Wanawake wanaotumia sindano hii hupata hedhi silimia 43 baada ya miezi
12 na asilimia 32 baada ya miezi 24.
Dawa hizo
huwafanya watumiaji washindwe kuwa waaminifu katika maisha ya na hali hii
inawahusu wanawake wote; walioolewa na wasioolewa, kwani mwanamke akijua kuwa
anaweza kufanya mapenzi bila kuwa na hofu ya kupata ujauzito anaanza kujiona
huru na kuvunja heshima inayolinda utakatifu wa tendo la ndoa.
Tumepata
kushuhudia, katika mazingira yasiyokuwa ya kawaida, wanawake ambao waume zao
wameondoka kwa muda mrefu kimasomo au kikazi, wametumia dawa hizi baadhi
wamepata mimba licha ya kuzitumia.
Hali hiyo
imevunja uaminifu wa ndoa na kuleta mafarakano na kwa kiasi kikubwa husababisha
kuvunjika au kuvurugika kwa ndoa nyingi, ambapo utafiti unaonyesha kuwa nchini
Marekani asilimia 50 ya ndoa zinazotumia dawa za uzzi wa mpango huvunjika miaka
michache baadaye kuliko ndoa zisizotumia dawa hizo.
Waasisi n
watetezi wa uzazi wa mpango kwa njia za kisasa, Marie Stopes na Margaret
Sanger, walisema lengo la njia hizo ni kuwaweka wanawake huru kutoka vifungo
vya ndo na hivyo kufurahia ngono bila mipaka.
Kutokana
na mke mtumiaji kukosa hamu ya kujamiiana, basi baada ya muda wanandoa huanza
kujisikia kutoridhishwa; mke anaanza kujisikia kuwa mume wake hampendi
isipokuwa mwili wake tu ambao unatumiwa kwa tamaa ya kuridhisha misukumo ya
mwili, wakati mume naye anaanza kufikiri mke wake hapendi tendo la ndoa kwa
vile anakuwa ''baridi''na kumlazimu kila anapohitaji unyumba kuomba na
kubembeleza. Misigano hiyo ndiyo hupelekea kuwepo kwa talaka au 'kuzaliwa' kwa
nyumba ndogo na mambo mengineyo.
Dawa hizi
husababisha kupungua kwa uwezo wa taifa kuzalisha mali kwa ajili ya maendeleo
na hivyo gurudumu la mzunguko wa umaskini kuzikabili nchi mskini, ikiwemo
Tanzania. Ukweli ni kwamba, nchi zilizotumia dawa hizi kwa muda mrefu, kama
vile nchi nyingi za Ulaya, ikiwemo Italia, Ujerumani, Ugiriki, Ufaransa, na
nyinginezo zimeshuhudia idadi ya watu wao ikipungua kwa kasi kubwa na haziwezi,
bila mikakati ya makusudi, kujizalisha tena.
Ili
kuweza kujizalisha, taifa lolote linatakiwa liwe na ongezeko la watu kwa mwaka
kwa wastani wa watoto 2.1 kwa kila familia, uwezo ambao uko chini kwa nchi
nyingi za Ulaya.
Kulingana
na tarifa iliyomo katika 'Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 1998'
iliyotolewa na Tume ya Mipango, Tanzania ina uwezo wa kujizalisha kwa wastani
wa watoto 2.8 kwa kila familia. Hali hii ikiendelea, tukizingatia vifo vya watu
wengi vitokanavyo na magonjwa hasa janga la UKIMWI, huenda katika muda mfupi
ujao Tanzania itashuhudia upungufu wa watu kuliko ongezeko la watu.
Historia
inatuthibitishia kuwa maendeleo huletwa na uwepo wa watu wengi katika nchi.
Nchi zote za Ulaya, Marekani, Japan, Uchina na India zimeendelea katika kipindi
ambapo idadi ya watu wake ilikuwa kubwa. Ndiyo maana leo nchi za Uingereza
(watu milioni 51), Ujerumani (milioni 82), na Ufaransa (milioni 58)
zinalalamika juu ya upungufu wa watu kuliko kufurahia upungufu huo.
Ukiangalia
nchi hizo ni ndogo kuliko Tanzania, ambayo ina watu milioni 45 kwa mujibu wa
Sensa ya mwaka 2012 na kila eneo la kilometa ya mraba linakaliwa na watu 50 tu
wakati watu wanaokaa katika eneo la kilometa mraba kwa baadhi ya nchi za Ulaya
ni: Uingereza (watu 245), Ujerumani (236), na Ufaransa (107).
Kwa ujumla,
hakuna asiyependa uzazi wa mpango, lakini wananchi wanaweza kuelimishwa kuhusu
uzazi wa mpango wa kutumia njia za asili ambazo mara nyingi hujulikana pia kama
njia za maumbile au Kalenda, ambapo wataalam wetu katika sehemu mbalimbali
wanaweza kutuelimisha badala ya matumizi ya dawa zenye kemikali zinazoweza kuua
na kuharibu au kuudhoofisha mwili wa mtumiaji, hasa mwanamke.<Mwisho>.
No comments:
Post a Comment