Mwenyekiti wa chama cha waandishi
wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard kulia akitoa msimamo wa
wanahabari dhidi ya gazeti la Rai na mbunge Msigwa leo ,kushoto ni
katibu mtendaji wa IPC Francis Godwin.
Wanahabari Clement Sanga kushoto akiwa
na mwakilishi wa New habari {2006} Ltd wachapishaji wa magazeti ya
Mtanzania , Rai na Bingwa mkoa wa Iringa Mercy Mwalusamba wakati wa
kikao cha cha wanahabari mkoa wa Iringa leo kujadili habari
zilizoandikwa na gazeti la rai jumapili .
Wanahabari wakifuatilia kwa makini kikao hicho
Na Francis Godwin Blog
WANAHABARI
mkoani Iringa wamekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la
Rai toleo Namba 1067 la Jumapili, Oktoba 27, 2013 kuwa wanahabari hao wamehongwa viongozi wa CCM mkoani humo ili wasiandike habari ya msaidizi wa Mbunge wa Isimani, Wiliam Lukuvi, Bw. Thom Malenga
kukamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na ujangili.
Katika kikao chao kilichofanyika leo katika ofisi za Klabu
ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC) mbali ya kukanusha
habari hizo kuwa zimeandikwa kwa lengo la kuchafua tasnia ya habari
mkoani humo, wamelitaka gazeti la Rai na Mbunge wa
Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kuwataja waandishi waliohongwa kabla ya wanahabari hao hawajachukua hatua zaidi.
"Gazeti la Rai Jumapili halijatutendea haki, limetuvunjia heshima kwa wadau wa habari mkoani Iringa na nje ya mkoa... tunachotaka Rai kuwataja waandishi waliohongwa ili tuchukuliane hatua... wasipofanya hivyo ndani ya siku 14 kuanzia leo Jumanne tutawafikisha Baraza
la Habari Tanzania (MCT)," walisema katika tamko lao lililotolea na Mwenyekiti wa IPC, Frank Leonard.
Walisema gazeti la Rai limewachafua vibaya kutokana na jinsi lilivyoandika habari hiyo huku likishindwa kuwapa hata fursa ya kuwahoji ili kuweka uzani sawa.
Leonard
alisema siyo kweli kwamba wanahabari Iringa walishindwa kuandika
habari ya kukamatwa kwa Malenga bali kwa kuwa wao ni
makini na hawakutaka kukurupuka hivyo walitaka
kabla ya kuandika kuweza kumpata msemaji wa kikosi hicho cha kupambana
na ujangili ili kulizungumzia hilo kabla ya kuandika jambo ambalo wao kama wanahabari walikuwa wakilisikia
mitaani bila kuwa na uhakika.
Uandishi wa habari mzuri ni pamoja na kuzingatia maadili ya uandishi na sio
kuandika bila ya kuwa na uhakika wa kile unachokiandika.
Hata hivyo alisema
kwa kuwa mbunge Msigwa amenukuliwa katika gazeti hilo kama ndio
msemaji wa jambo hilo wao kama wanahabari watamwandikia barua mbunge
huyo ili kusaidia kuwataja wanahabari waliohongwa pesa vinginevyo
wao kama wanahabari wa mkoa wa Iringa hawatamvumilia Mbunge Msigwa
katika hilo.
Pia alisema kuwa suala hilo kwa sasa ameachiwa mwanasheria wa IPC ili
kulifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwaandikia barua Rai na Mbunge Msigwa kuwataka kuthibitisha
ukweli wa kilichoandikwa dhidi ya wanahabari Mkoa wa Iringa.
CHANZO: francis godwin blog
(Imehaririwa na Admin wa blog hii)
No comments:
Post a Comment