Na Brother Danny
WATU wengi
ni watumwa wa ngono bila wenyewe kujua. Lakini ubongo una kazi gani katika utumwa
wa ngono? Ni njia gani zilizopo katika kupambana na uraibu na kurejea katika
hali ya kawaida pamoja na kujizatiti na kujihakikishia tena kuwa na maisha ya
mapenzi yaliyo bora? Kitu kilicho bora, ninaamini ni kwenda hatua kwa hatua
katika kulielezea tatizo hili.
Utumwa wa Ngono ni nini?
Mapenzi
ya kushurutishwa, yale ya lazima, ambayo mtu analazimika kufanya bila kufuata
taratibu, yaani ile tabia ya kutaka kufanya mapenzi au vitendo vya ngono kila
wakati, kila mahali na mtu yeyote, ni uraibu na utumwa, tena ni tatizo ambalo
linaweza kudhibitiwa. Kwa maana nyingine uraibu wa ngono ni ile tabia ya mtu
kupenda kufanya mapenzi kila wakati, kila mahali, na kutotosheka na mapenzi
ayapatayo.
Watu wa
aina hii wako wengi, wengine hupendelea vitu fulani katika kukidhi kiu zao za
mapenzi, kama vile kupiga punyeto (kujichua: kwa mwanamke na mwanaume na kuna
wanawake ambao siku hizi wanapenda sana kutumia viungo bandia vya kiume ili
kukidhi kiu zao, hasa wasagaji), kutazama picha za ngono, kuchungulia watu
wakifanya mapenzi na mambo mengine kadha wa kadha.
Wapo pia
watu; wanawake kwa wanaume, ambao hata kama wako na wapenzi wao huwa hawafikii
mshindo mpaka ama wakumbuke picha ya ngono waliyopata kuiona au wamfikirie mtu
ambaye wanampenda sana na wangetamani kufanya naye mapenzi.
Watu kama
hawa, bila kuvuta hisia kama hizi katu hawawezi kuridhika, na mara baada ya
kufikia mshindo huwa hawawezi kabisa kuendelea kufanya mapenzi kwa ngwe
nyingine na hujiona kama wanajilazimisha tu!
Mapenzi
bora na yanayonoga ni yale yenye mvuto na hisia. Haya hutoa nafasi ya kufurahia
uhusiano ulio bora zaidi na wenye mvuto yakini. Lakini kwa baadhi ya watu, kuna
msukumo wa lazima ambao huwalazimu kujiingiza katika vitendo vya ngono
vilivyokithiri na visivyofaa.
Utumwa wa
ngono huharibu maisha ya kawaida ya mapenzi ya mhusika. Watu walioraibiwa na
ngono hawawezi kudhibiti au kuahirisha hisia zao za ngono pamoja na matendo
yao. Wataendelea na vitendo vyao viuvo vya ngono, wakihangaika kuzifurahisha
hisia zao za mapenzi kwa gharama yoyote ile, wengine kama siyo kujichua,
huishia hata kubaka watoto, na wanaume wengine hata kama wanazo fedha, unaweza
kuwakuta wakisaka changudoa na hata mashoga, kutegemeana na wapi hisia zake
zinakompeleka.
Wanaume
wengine, japokuwa wako kamili, lakini hisia zao zinaweza zikawapeleka kutaka
kulawitiwa, nao hufanya hivyo, na ndiyo maana unaweza kukuta katika jamii mtu fulani
anaelezwa kwamba ana tabia za kishoga ukakataa, au mwingine ana mumewe lakini
anatamani sana kufanya mapenzi na mwanamke mwenzake, yaani wanasagana!
Kwa watu
wengine walioraibiwa na ngono, suala la kutimiza haja zao za ngono huwa ndilo
linachukua nafasi kubwa katika maisha yao, na ni muhimu kuliko familia,
marafiki, au hata kazi zao.
Nimeshakutana
na watu wa aina mbalimbali wakati nikifanya uchunguzi wangu, na baadhi ya
wanaume walikuwa na mtazamo tofauti. Yupo mmoja ambaye ana familia yake, lakini
hupendelea kuwahonga baadhi ya vijana ili wakamlawiti, yupo mwingine aliye na
mke mzuri sana, lakini anasema kwamba pamoja na kufanya mapenzi na mkewe,
lakini lazima kwa wiki moja atafute shoga afanye naye mapenzi, mwingine anasema
kwamba, lazima atafute changudoa, na mwingine yeye anasema wazi kwamba,
anapendelea zaidi kufanya ngono na wasichana wa kazi, yaani mayaya (house girls);
awe kwake au kwa jirani yake, ilimradi ni yaya, basi kwake ni halali!
Zaidi
wapo wengine ambao wanasema kwamba, kabla ya kufanya mapenzi na wake zao ni
lazima waingia bafuni wakajichue (kupiga punyeto - masturbation) ndipo
wawaingilie wake zao.
Wanawake
nao wana mambo yao, wapo ambao pamoja na kupatiwa kila kitu na waume zao,
lakini huwa hawatosheki mpaka wafanye ngono na vijana wao wa kazi au vijana
hohehahe na wao ndio hugharamia kila kitu.
Wapo
ambao hupendelea kusagana na wanawake wenzao, na wapo ambao huwa hawatosheki
kabisa na penzi la mume mmoja. Wanataka kujaribu uwezo wa kila mwanaume.
Wengine –
wanaume kwa wanawake – wanasema hawawezi kufanya tendo la ndoa mpaka kwanza
waangalie mkanda wa ‘bluu’ (picha za ngono). Hizi, wanasema, huwasisimua na
kuwapandisha ashki na ndipo hupata fursa ya kuingiliana.
Huu wote
ndio unaoitwa uraibu, ama utumwa wa ngono, ambao nina imani kila mmoja wetu
anao au alipata kuwa nao bila mwenyewe kujiujua.
Ubongo na Utumwa wa Ngono
Ubongo
huitikia na kuongoza elementi kubwa za mfumo wa ndani wa taarifa za kemikali za
mwili wa binadamu. Msisimko wa mahaba huchochea mwenendo mzima wa mfumo mkuu wa
neva, ukiibua mabadiliko kadhaa ya mwili.
Matumainio
ya raha huongeza uzalishaji wa homoni, huongeza kasi ya mapigo ya moyo,
huongeza msukumo wa damu na kuimarisha umakini wa neurone. Sitiari ya
"kemia" baina ya watu wawili hubadilika na kuwa biokemia kwa uhakika,
hasa kemikali ya phenylethylamine
(PEA) inapoonekana kwenye ubongo.
PEA
inahusika na msukumo na nguvu za kumwezesha mtu aangukie mapenzini na kutekwa.
Viwango chipukizi vya kemikali hii huleta matokeo ya ongezeko la raha na
mpagawisho (intensified excitement &
euphoria).
Watumwa
wa ngono hutegemea zaidi hamasa ya kimwili na kisaikolojia inayochangiwa na
'dawa ya mapenzi' ya PEA iliyo ndani ya ubongo.
Fahamu Ulazima wa Ngono
Watu
wengi walioraibiwa katika mapenzi walipatwa kukumbwa na mikasa ya kunyanyaswa
kimapenzi au kutengwa wakati wa utoto. Matokeo yake, wameendeleza hisia za
kutokamilika na kujidharau wenyewe kwamba hawajakamilika.
Wazazi
wao pia wanaweza kuwa waliwahi kuwa watumwa wa ngono na katika kuweka mlinganyo
sawa wa tabia yao iliyokithiri, inawezekana waliwalea watoto wao bila maadili
bora katika suala zima la mapenzi.
Mapenzi
ya lazima mara nyingi huenda sambamba na na hisia za aibu, hatia na kutokuwa na
thamani. Ingawa uzoefu wa mapenzi unaweza kuleta uhuru wa kitambo kifupi
kutokana na hisia za aina hii, lakini bila kutegemea mhusika anaweza kujikuta
akipambana na aibu, lawama na kujitweza mwenyewe. Watumwa wa ngono huwa hawana
nguvu za kupambana na tabia zao.
Aina za Utumwa wa Ngono
Hizi
dalili za athari zilizotokea kwa maisha ya mtumwa wa mapenzi:
Kumilikiwa - kila wakati kutafuta njia mpya za
kukidhi kiu ya mapenzi. Wapo watu ambao kila siku wanabuni njia mpya ya kukidhi
tamaa zake. Kama bosi, kwa mfano, amezoea kufanya mapenzi na sekretari wake au
mfanya kazi wake, anaweza kuiendeleza tabia hiyo hata kufikia kutembea na wake
wa wafanyakazi wake. Ngono ndicho kitu kinachokuwa kimemmiliki wakati wote.
Kulazimishwa - kuendelea kushiriki
katika vitendo vya ngono hata kama vimemletea mhusika madhara na kukosa njia za
kukoma tabia hiyo. Wapo watu ambao wamewahi kufumwa na wake au waume zao wakiwa
na wafanyakazi wao wa ndani wakifanya mapenzi, lakini pamoja na aibu hiyo
waliyoipata bado hawajakoma wanaendelea, na wazazi wengine hufikia hatua ya
kutembea na binti zao au watoto wao wa kiume, hii hutokea katika baadhi ya watu
ambao uraibu huu huwalazimisha kufanya vile hisia zao zinavyowatuma.
Kukata tamaa - kuona hatia au aibu
katika uwezo wa kuidhibiti tabia ya ngono ya mhusika. Ili tabia hii ikome, ni
lazima mhusika akiri kwamba ana tatizo hilo, lakini wengi wa waathirika huona
aibu na hujisikia hatia, hasa kama walipatwa kufumaniwa na baadhi ya wanajamii
wanaelewa vitendo vyao.
Kumaliza Utumwa wa Ngono
Hatua ya
kwanza ya kumaliza tatizo la uraibu wa ngono, kama nilivyosema hapo juu, ni
kulifahamu tatizo husika. Utakapogundua kwamba tabia yako haidhibitiki, ni
wakati muafaka kwako kutafuta tatizo linalosababisha uraibu wako wa ngono.
Matatizo haya yanaweza kuwa ya kifedha, kihisia na kimwili.
Ndiyo,
wapo baadhi ya watu mara wanapokuwa na fedha wanataka kufanya mapenzi na mtu
yeyote yule. Mwanaume mwenye fedha hupenda kutembea na wasichana wazuri wazuri
na anaweza kufikia mahali akatembea hata na wake wa rafiki zake. Mbaya zaidi,
anaweza kuwageukia hata wanafunzi kwa kuwarubuni kwa visenti vyake. Mwanamke
mwenye fedha naye vile vile, anaweza kuwatafuta wanaume anaowataka na
kuwahonga, ilimradi tu apate penzi.
Kama
mtumwa wa ngono, kuna hatua zinazotakiwa kufuatwa ili kukusaidia kupambana na
hisia zako za kutengwa kifikra. Kwa vile msongo wa mawazo wakati mwingine
huchangia vitendo vya mapenzi ya lazima, mbinu za kupambana na msongo wa mawazo
wakati mwingine husaidia.
Nchini
Marekani kuna makundi kadhaa ambayo husaidia waathirika kupambana na madhara
hayo. Taasisi hizo ni kama Sex & Love Addicts Anonymous, Sexaholics
Anonymous & Sex Abusers Anonymous. Mhusika hata hivyo anaweza kupatiwa
msaada na taasisi hizi kupitia mtandaoni au kwa kuwasiliana nao kwa simu.
Mnaweza
kunitumia mchango wenu kwa sms ama kunipigia kupitia kilongalonga – 0715 – 070
109, au barua-pepe: brotherdanny5@gmail.com.
No comments:
Post a Comment