Ofisa Uhusiano kutoka Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu (kulia) akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo
pichani) mafanikio yaliyopatikana katika utoaji wa huduma ya afya ikiwa ni
pamoja na kuboresha miundombinu ya afya katika manispaa hiyo, wakati wa mkutano
uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dk. Asha Mahita.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dk.
Asha Mahita (kushoto) akitoa tahadhari kwa wananchi kupitia waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuacha tabia ya kufungua makaro ya maji machafu kipindi
cha mvua ili kuepuka magonjwa ya mlipuko, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa
Manispaa hiyo Bi. Tabu Shaibu. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
No comments:
Post a Comment