Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 28 October 2013

PROMOSHENI YA MAWAKALA YAZIDI KUCHANJA

Meneja wa Vodacom Tanzania,Chunya Mkoa wa Mbeya Bw. Elisha Tengeni (kushoto)akimkabidhi wakala wa M-pesa wa hiyo,Bw.Damas Mtewele hundi yake yenye thamani ya shilingi 100,000 aliyojishindia katika Promosheni ya "Mkwanja kwa Wakala"yenye lengo la kuboresha maisha ya mawakala wa kampuni ya Vodacom.Kampuni hiyo  imetenga fedha taslimu kwa mawakala 810 wa M-pesa ambao wamejivunia kiasi cha  Shilingi Milioni 81 ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini Mchango wao kwa jamii ya watanzania na kampuni hiyo,hadi sasa kati ya Wakala 270 wamepatikana katika droo iliyochezeshwa leo ikiwa ni wiki ya tatu tangu kuanza kwa promosheni hiyo.
 
Meneja wa Vodacom Tanzania,Chunya Mkoa wa Mbeya Bw. Elisha Tengeni(kushoto)akimkabidhi wakala wa M-pesa wa Wilaya hiyo Bw.Jerry Bryan, hundi yenye thamani ya shilingi 100,000 aliyojishindia katika Promosheni ya "Mkwanja kwa Wakala" yenye lengo la kuboresha maisha ya mawakala wa kampuni ya Vodacom.Kampuni hiyo  imetenga fedha taslimu kwa mawakala 810 wa M-pesa ambao wamejivunia kiasi cha  Shilingi Milioni 81 ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini Mchango wao kwa jamii ya watanzania na kampuni hiyo,hadi sasa kati ya Wakala 270 wamepatikana katika droo iliyochezeshwa leo ikiwa ni wiki ya tatu tangu kuanza kwa promosheni hiyo.
Wakala wa M-pesa wa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya Bw.Jerry Bryan, akiwa ameshikilia hundi yenye thamani ya shilingi 100,000 mara baada ya kukabidhiwa na Meneja wa kanda hiyo Elisha Tengeni(hayupo pichani)katika Promosheni ya "Mkwanja kwa Wakala" yenye lengo la kuboresha maisha ya mawakala wa kampuni ya Vodacom.Kampuni hiyo  imetoa fedha taslimu kwa mawakala 810 wa M-pesa ambao wamejivunia kiasi cha  Shilingi Milioni 81 ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini Mchango wao kwa jamii ya watanzania na kampuni hiyo,hadi sasa kati ya Wakala 270 wamepatikana katika droo iliyochezeshwa leo ikiwa ni wiki ya tatu tangu kuanza kwa promosheni hiyo.
Meneja wa Vodacom Tanzania,Chunya Mkoa wa Mbeya Bw. Elisha Tengeni (kushoto) akimkabidhi wakala wa M-pesa wa wilaya hiyo,Bw.Peter Maliva hundi yenye thamani ya shilingi 100,000 aliyojishindia katika Promosheni ya "Mkwanja kwa Wakala"yenye lengo la kuboresha maisha ya mawakala wa kampuni ya Vodacom.Kampuni hiyo  imetenga fedha taslimu kwa mawakala 810 wa M-pesa ambao wamejivunia kiasi cha  Shilingi Milioni 81 ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini Mchango wao kwa jamii ya watanzania na kampuni hiyo,hadi sasa kati ya Wakala 270 wamepatikana katika droo iliyochezeshwa leo ikiwa ni wiki ya tatu tangu kuanza kwa promosheni hiyo.


MTWARA - Katika harakati za kuhakikisha inaboresha maisha ya mawakala wake kampuni ya Vodacom imetoa fedha taslimu kwa mawakala 810 wa M-pesa ambao wamejivunia kiasi cha  Shilingi Milioni 81 ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini Mchango wao kwa jamii ya watanzania na kampuni hiyo.
 hadi sasa katika promosheni ya Mkwanja kwa Wakala kati yao 270 wamepatikana katika droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es salaam ikiwa ni wiki ya tatu tangu kuanza kwa promosheni hiyo.

Kupitia Promosheni yake ya Mkwanja kwa Wakala ambayo haimhitaji wakala kutoa kiasi chochote kushiliki zaidi ya kufanya maamisho matano ya fedha tayari imekuwa na mafanikio na kupigiwa chapuo  na mawakala hao kuwa sehemu ya kuboresha maisha yao.
 "Tunao mawakala zaidi ya 55,000 nchi nzima na hivyo kuifanya huduma yetu hii ya M-pesa kuongoza na  kuleta unafuu mkubwa kwenye maisha ya watu, mafanikio yetu yanatokana na kazi nzuri na kubwa inayofanywa na mtandao huu wa mawakala."Alisema Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano wa Vodacom Joseline Kamuhanda muda mfupi baada ya kuchezeshwa kwa droo leo.
"M-pesa imeendelea kuwa huduma inayoongoza sio tu kwa idadi kubwa ya mawakala wanaofanya huduma hiyo kupatikana kwa urahisi na uhakika zaidi bali pia kuyaleta maisha ya watanzania viganjani mwao kwani kwa sasa wanauwezo wakufanya miamala kwa makampuni zaidi ya 300 kwa kiasi tu cha kupiga *150*00# kutoka simu zao za viganjani"Aliongeza Kamuhanda
Kamuhanda amesema ni matumaini yao kwamba mawakala wameendelea kufurahia promosheni hiyo ambayo pia hutoa cheti cha utambuzi wa huduma bora kwa wakala mmoja katika mkoa wa kibiashara wa Vodacom.
Kamuhanda amesema mafanikio ya M-pesa hapa nchini sio jambo linalotokea kwa kubahatisha bali ni kazi nzuri inayofanywa na Vodacom na washirika wake wakiwemo mawakala wadogo na wakubwa ambao kwa pamoja wameweza kuwahudumia wateja zaidi ya Milioni Tano wa M-pesa.
"Kupitia mawakala wetu kila mmoja amekuwa akifurahia jinsia huduma ya M-pesa ilivyoleta mageuzi makubwa kwenye maisha yake hakuna anaepanga foleni benki, au kusafiri umbali mrefu kutuma pesa kwa ndugu au jamaa au kwenda kulipia ada, tiketi ya safari ya ndege, kodi TRA au huduma nyengine mbalimbali kwani kwa sasa yote haya yanawezeshwa kwa njia ya M-pesa."
Kamuhanda amewataka mawakala kuendelea kufurahia na kutajirika na promosheni hiyo ya Mkwanja kwa Wakala ambayo inaendelea kwa wiki tano zaidi na kwamba jumla ya Shilingi 216 Milioni zimetengwa kwenda kwa mawakala kama zawadi ya ushindi ya fedha taslimu.
Kamuhanda amema M-pesa itaendelea kuongoza na kuwa huduma yenye usalama, kuaminika, kuaminiwa zaidi na uhakika wa kupatikana kwa urahisi wakati wowote mahali popote kutokana na kazi kubwa ya ubunifu inayofanywa na Vodacom ili kuipa huduma hiyo ya M-pesa uwezo mpna wa kuhudumia mambo mengi zaidi kukidhi mahitaji ya wateja ya sasa na ya baadae.

No comments:

Post a Comment