Kutokana na kudaiwa deni la zaidi ya milioni 100 kanisa la Sinza
Christian Center latupiwa nje vyombo
vyake na dalali aliyepewa tenda hiyo bwana Joshua aliyeteuliwa na Mahakama na
mmiliki jengo hilo Bwana Prosper Rwendera.
Akizungumza na Dar es Salaam Yetu Blog mke wa mmiliki wa jengo hilo Bi. Patricia Prosper alisema; “huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa jengo letu."
Akizungumza na Dar es Salaam Yetu Blog mke wa mmiliki wa jengo hilo Bi. Patricia Prosper alisema; “huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa jengo letu."
Alipotafutwa msemaji wa Kanisa ambaye ni Askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo, hakupatikana kuzungumzia
sakata hilo na hata waumini wa kanisa hilo walipotafutwa walikataa kwa madai hawana mamlaka ya kuzungumzia lolote kuhusiana na sakata hilo.
Hili ni eneo la Kanisa Hilo.
Viti vyote vikiwa vimetolewa nje
Vyombo vya Muziki vikiwa nje
Magari yakiwa yanatolewa nje
Vitu vikiwa nje ya Jengo hilo ambapo mpaka sasa kuna sinto fahamu vinapelekwa wapi
Vikombe nje
Wametoa vitu vyote
Baadhi ya Magari yaliyotolewa katika Jengo hilo ambapo hapo awali ilikuwa ni Kanisa
Kushoto kwa mbali ni Mke wa mmiliki wa Jengo hilo Bi. Patricia Prosper akiendelea na majukumu huku pembeni vijana wakipata maelekezo ya kuendelea kutoa vitu.
Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa
No comments:
Post a Comment