Meneja
Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi, George Mkanza akifafanua jambo kwa
madiwani wa halmshauri ya mji wa Kahama wakati ziara ya kutembelea Mgodi huo.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya mji wa Kahama Abel Shija(mwenye skafu) pamoja na
waheshimiwa madiwani na wataalamu wa halmashauri hiyo wakifuatilia
kwa makini maelezo kutoka kwa wataalamu wa Mgodi huo.
Afisa
mazingira wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Lusajo Njobelo akifafanua jambo kwa
waheshimiwa madiwani na mbunge wa Kahama mjini Jumanne Kishimba
wakati wa ziara hiyo.
Madiwani
pamoja na wataalamu kutoka halmashauri ya mji wa Kahama wakipiga picha
mbele ya moja ya mitambo inayotumika kusomba mawe mgodini hapo.
Meneja
Uchimbaji wa Mgodi wa Buzwagi Rodney Burgess (wa pili kutoka kulia)
akiwa na baadhi ya madiwani wa halmashauri ya mji wa Kahama.
Wataalamu
wa halmashauri ya mji wa Kahama wakiwa katika kituo cha kupozea umeme,
kituo ambacho kinaelezwa kuwa kitatumika pia kufunga kifaa
maalumu kilichonunuliwa na Mgodi wa Buzwagi ambacho kitawawezesha
wananchi wa Kahama na viunga vyake kuweza kupata umeme wa uhakika.
Afisa
Mawasiliano wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Magesa Magesa akiteta jambo na
Katibu wa Mbunge wa Kahama mjini, Abdul Mpei wakati wa ziara ya
madiwani ambayo pia ilihusisha wataalamu kutoka halmashauri.
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza na madiwani
wa halmashauri ya Kahama wakati wa kuhitimisha ziara yao walipotembelea
Mgodi huo.
Mbunge
wa jimbo la Kahama Mh. Jumanne Kishimba (Kulia) akiwa na mwenyekiti wa ya wilaya ya Kahama, Abeli Shija wakimsikiliza Meneja mkuu wa Mgodi
wa Buzwagi wakati alipokuwa anazungumza na madiwani baada ya ziara yao.
Picha
ya pamoja baina ya madiwani wa Halmashauri ya mji wa Kahama, wataalamu
wa halmashauri hiyo pamoja na maofisa wa Mgodi wa Buzwagi.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini.
Madiwani
wa halmashauri ya mji wa Kahama wameupongeza Mgodi wa Dhahabu wa
Buzwagi ulioko wilayani Kahama mkoani Shinyanga, kwa
namna ambavyo umekuwa ukishiriki katika kutekeleza miradi mbalimbali ya
Maendeleo ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Kahama na
hususuani vijiji vinavyozunguka Mgodi huo.
Pongezi hizo zimetolewa kwa niaba ya madiwani hao na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abeli Shija wakati wa ziara ya
siku moja iliyokuwa imelenga kujionea namna Mgodi huo unavyofanya shughuli zake za uchimbaji.
“Kwa
niaba ya halmashauri ya mji tunawapongezeni sana kwa namna ambavyo
mmekuwa chachu ya mendeleo kwa wilaya yetu na tunafarijika
kwa sababu leo mji wetu uko na barabara nzuri lakini pia wakazi wa
Mwendakulima na maeneo ya jirani wanao uhakika wa kupata huduma nzuri za
afya katika kituo cha afya ambacho mmeshiriki kukijenga, watoto wetu
pia wanaouhakika wa kusoma vizuri kutoka na miundo
mbinu mlioiweka katika baadhi ya shule na hasa ujenzi wa maabara za
kisasa ” alisema Shija.
Mwenyekiti
huyo pia aliuomba uongozi wa Mgodi kuwezesha upatikanaji wa kifaa
kitakachosaidia mji wa Kahama kupata umeme wa uhakika
ambao utaendana na Mahitaji ya shughuli za kiuchumi kwa mji wa Kahama
kutokana na line iliyopo sasa kushindwa kukizi Mahitaji ya wakazi wa mji
wa huo.
Akijibu
ombi hilo Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mhandisi Asa Mwaipopo amesema
mpaka sasa kifaa hicho kimeisha fika na kinachosubiliwa
ni wataalamu waliotengeneza kifaa hicho kutoka ujerumani kuja na
kukifunga.
“Kifaa
kimeisha fika na tunachosubiri kwa sasa ni wataalamu tu kuja na
kukifunga, matumaini yetu ni kuwa kazi hiyo itakapokamilika
wananchi wa Kahama wataondokana na tatizo la umeme usiokuwa wa
uhakika.” Alisema Mwaipopo.
Ziara
hiyo ambayo ilihusisha madiwani wa mji wa Kahama, Mbunge wa Kahama
mjini, Jumanne Kishimba na wataalamu wa halmashauri hiyo,
walipata fursa ya kutembelea maeneo mbali ya Mgodi huo na kuelezewa
namna suala la usalama wa mazingira linavyozingatiwa, ambapo madiwani
hao walishangazwa na namna Mgodi huo ulivyozingatia sheria mbalimbali za
mazingira na uchimbaji na kulifanya eneo hilo
kuwa salama zaidi.
Madiwani hao waliomba mgodi huo kuongeza
ufahamu kwa Jamii kwa kuongeza ziara nyingi zitakazo husisha wananchi wa
kawaida kwa lengo la kuwafahamisha shughuli zinazofanywa na Mgodi hali
ambayo wamesema itasaidia kupunguza taarifa
za uongo ambazo zimekuwa zikisambaa mitaani kutokana na Jamii kutokujua
ukweli.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment