Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 15 June 2016

Hatimaye Nyumba ya Kisasa ya ‘Shinda Nyumba’ Yakamilika

1 Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdalkah Mrisho, akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) walipotembelea nyumba hiyo.
2Wanahabari wakizungumza na Mrisho kwenye nyumba hiyo.
3Mrisho akiwaonyesha masinki ya jikoni.
4Haya ni masofa murua yaliyo ndani yake.
5Mrisho akiangalia kabati dogo.
6Muonekano wa sehemu ya ubavuni.
7Mandhari ya barazani.
8Sura ya mbele ya nyumba husika.
9Moja ya mafeni yaliyomo ndani.
10Sinki la jikoni.
11Moja ya taa za ukutani.
12
Sinki la sehemu ya kulia chakula.
13Moja ya sehemu za mbele.

HATIMAYE ule mchakato wa mchezo wa bahati nasibu ya Jishindie Nyumba kwa kusoma magazeti ya Global Publishers, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na Championi umefikia hatua za lala-salama ambapo nyumba husika imeshakamilika kwa kila kitu.
Nyumba hiyo iliyopo Mbezi Salasala Jijini Dar leo Jumatano ilitembelewa na vyombo mbalimbali vya habari katika msafara ulioongozwa na Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.
Akiwatembeza wanahabari kwenye nyumba hiyo, Mrisho aliwaonyesha mandhari ya ndani na nje ya nyumba hiyo ambayo iko sehemu yenye upepo mwanana unaovuma kutoka eneo la Kunduchi Beach.
Wanahabari hao walishuhudia samani za kisasa zilizomo kwenye nyumba hiyo kama vile masinki ya kunawia, taa za urembo, meza kubwa, televisheni, masofa, feni za juu na mengineyo.
Mrisho alisema nyumba hiyo iko tayari kukabidhiwa mshindi atakayepatikana katika droo inayotarajiwa kufanyika Juni 30 mwaka huu kwenye viwanja vya Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Mrisho aliwataka watu mbalimbali kununua magazeti ya Global Publishers na kukata kuponi kisha kuzifikisha kwenye ofisi hizo zilizopo Bamaga- Mwenge jijini au wampatie muuza magazeti yeyote.
Haya, ndugu msomaji, hata wewe waweza kugeuka baba au mama mwenye nyumba! Kazi kwako, nyumba ndiyo hiyooo….!!!
PICHA RICHARD BUKOS / GPL

No comments:

Post a Comment