Kipa Hanningtony Kalyesubula
Orodha ya wachezaji ambao walikuwa kwenye kikosi cha Mbeya City fc msimu uliopita na mikataba yao kufikia tamati baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara Mei 22 tayari imetolewa ikiwataja nyota saba kutokuwepo tena kikosini msimu ujao.
Muda mfupi uliopita, Katibu Mkuu wa City Emmanuel Kimbe amesema kuwa, wachezaji saba wanaotajwa kwenye orodha hii ni wazi mikataba yao imemalizika na klabu haitafanya tena mazungumzo yoyote na tayari wamesha taarifiwa juu ya hilo.
“Mikataba yao imemalizika, tumekwisha wataarifu kuwa hatutakuwa na mazungumzo mapya, hili soka kutoka timu moja kwenda nyingine ni jambo la kawaida hivyo tunawatakia kila la heri kwenye maisha mapya ya soka watakayo kutana nayo” alisema.
Kwenye orodha hiyo yupo mlinda mlango Haningtony Kalyesubula, walinzi ni Yusuph Abdalah Sisalo, Deo Julius, Hamad Kibopile, Yohana Morris, Richard Peter Chundu na mshambualiaji Temmi Felix.
Katika hatua nyingine Kimbe amesema kuwa klabu bado inafanya mazungumzo na baadhi ya nyota ambao mikataba yao imemalizika lakini bado wanayo nafasi ya kuendelea kukitumikia kikosi cha City kwa mujibu wa mapendekezo ya kocha Kinnah Phiri, huku pia mazungumzo ya wachezaji wengine ambao bado wana mikataba lakini hawapati nafasi ya kucheza yakiendelea ili kuona ni jinsi gani wanaweza kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao.
No comments:
Post a Comment