Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani Bi. Melinda Gates akiongea na wadau mbalimbali na kulipongeza shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kwa kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo lengo kubwa ni kuwawezesha wakulima wadogo wadogo wanawake kufanikiwa katika Kilimo cha chakula na umiliki wa ardhi.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akitoa neno la utangulizi wakati wa sherehe hiyo.
Waziri wa Afya,Jinsia,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akilipongeza Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kwa kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo linaonesha changamoto za wazalishaji wa chakula wadogo ikiwemo umiliki wa ardhi.
Mshereheshaji katika Hafla hiyo Maria Sarungi Tsehai akiendelea kutoa muongozo
Dkt. Eve Marie akizungumza kwa kina ni jinsi gani Serikali na Sekta binafsi zinaweza kuwekeza katika wakulima wadogo wadogo hasa wanawake ili kuongeza uzalishaji wa Chakula
Muwezeshaji kutoka Forum CC Faizal Issa akielezea namna wakulima ambavyo wanaweza kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi ambayo kwa sasa yanaathiri kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji katika kilimo.
Mwanamuziki maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva Mwasiti akitumbuiza wakati wa Sherehe hizo
Mama Shujaa wa Chakula Anna Oloishuro akizungumzia jinsi mabadiliko ya tabianchi yanavyo athiri katika kilimo pia kuomba Benki mbalimbali nchini zisaidie wakulima kwa kuwakopesha na kuwapa riba ndogo.
Profesa Marjorie Mbilinyi akizungumzia swala zima za wazalishaji wa chakula wadogo kukosa masoko alisisitiza Sheria mbalimbali zifuatwe ili kukabilina na hali hiyo.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Msichana Initiative Rebeca Gyumi akizungumzia tatizo la ajira kwa vijana Tanzania na kusisitiza ikiwa watawezeshwa katika mambo mbalimbali ikiwemo na umiliki wa Ardhi basi wataweza kufikia malengo yao.
Baadhi ya wageni wakiwa katika sherehe hizo wakifuatilia kwa makini mjadala uliokuwa ukiendelea fuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea
Mwigizaji Maarufu wa Bongo Movie na Balozi wa Oxfam Tanzania Jacob Stephen JB akitaja majina washiriki 19 katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2016 msimu wa tano
Aliyekuwa Mshiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa nne na Rais wa wakulima wadogo wadogo wanawake Afrika Bi. Eva Daud Mageni akitoa neno la Shukurani kwa Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani na kumpa zawadi maalum ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika kuendeleza jitihada za maendeleo Tanzania ikiwemo swala la Kilimo.
Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani akipokea zawadi maalumu kutoka kwa waliokuwa washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Misimu iliyopita
Picha ya Pamoja ya Waziri wa Afya,Jinsia,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu,Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani, Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster,Mabalozi wa Oxfam Tanzania pamoja na Baadhi ya Akina mama watakao Shiriki Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2016
Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwa katika Sherehe hiyo
Mkutano Maalum na waandishi wa Habari ukiendelea
Picha na Fredy Njeje
Waziri wa Afya, Jinsia,
Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na mke wa tajiri namba moja duniani na mwenyekiti
mwenza wa Bill and Melinda Gates Foundation, Melinda Gates kwa pamoja
wamelipongeza Shirika la Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow kwa kufanya Shindano
la Mama Shujaa wa Chakula kama moja ya mbinu za kumkomboa mwanamke mnyonge
kiuchumi.
Wawili hao waliyasema
hayo kwenye mdahalo uliofanyika Juni 29 mwaka huu katika bustani ya Hoteli ya
Serena jijini Dar ambapo walikuwa wageni waalikwa waliopata fursa ya
kuzungumzia jinsi ya kumuwezesha kiuchumi mwanamke mzalishaji na namna ya
kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Akizungumza kwenye
mdahalo huo, Melinda Gates alisema kuwa yeye kupitia Bill and Melinda Gates
Foundation wamelenga kusaidia nchi nyingi hasa za ukanda wa Afrika Mashariki
kama Tanzania katika kubadilisha maisha yao kwa kutengeneza fursa za ajira na
kuwasaidia vitendea kazi.
Aliongeza kuwa kwa nchi
kama ya Tanzania ambayo asilimia 25 ya mapato yake yanatokana na kilimo,
taasisi yao imejikita katika kuwawezesha wakulima wadogowadogo ambao hata hivyo
huwezi kuwaacha wakina mama kwa kuwa ndiyo wanaotoa mchango mkubwa kwenye sekta
hiyo.
Akizungumzia kuhusu Shindano
la Mama Shujaa wa Chakula, Melinda Gates alitoa pongezi zake za dhati kwa
shirika la Oxfam na kuongeza kuwa, ikiwa nchi za Kiafrika hususan Tanzania
itataka kupiga hatua lazima iwawezeshe kiuchumi wanawake kwa kuwa wao ndiyo
wenye uwezo wa kubadilisha maisha yao na hilo ndiyo jambo muhimu zaidi.
Naye Waziri wa Afya,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye
mdahalo huo alisema kuwa; kwa kipindi kirefu amekuwa mfuatiliaji wa mashindano
hayo na kuahidi kuwa sera ya serikali ya awamu ya tano ni kuongeza vipaumbele
kwa mwanamke kwa kutoa mianya kwa taasisi zinazomsaidia mwanamke ikiwemo
shirika la Oxfam kupitia shughuli zake hasas shindano la mama shujaa wa
chakula.
“Nikiri tu kuwa
nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa shindano hili tangu zamani, naahidi kuwapa
ushirikiano mkubwa kwenu kwa kila jambo kwa kuwa mnaisaidia sana serikali,”
alisema Ummy.
Aidha mdahalo huo pia
ulioongozwa na mwanaharakati, Maria Sarungi Tsehai ulihudhuriwa na wanaharakati
wengine wa masuala ya jinsia akiwemo Mkurugenzi wa Msichana Initative, Rebecca
Gyumi, Mwanaharakati wa Mtandao wa Masuala ya Kijinsia, Marjorie Mbilinyi, Mwezeshaji
kutoka Forum CC, Faizal Issa na Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
2011, Anna Oloishuro.
No comments:
Post a Comment