Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kulia) akizungumza na Rais wa Comoro Mhe.Azali Assouman walipokutana kwenye
uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye
mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya
Umrah nchini Saudi Arabia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa
tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Comoro
Mhe.Azali Assouman na ujumbe wake walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Dar es
Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya
kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya Umrah nchini Saudi Arabia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu Ikulu jijini Dar es Salaam
ambapo Balozi wa Japan Nchini alisema nchi yake imeridhishwa na kasi ya
Serikali ya Rais Mhe. Magufuli na kuahidi kuendelea kuisaidia Tanzania
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu mara
baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
......................................................
Rais
wa Comoro AzaliI Assouman amesema serikali yake itaendelea kudumisha uhusiano
na ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania
na Comoro katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya na biashara.
Rais
huyo wa Comoro ametoa kauli hiyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya
Rais John Pombe Magufuli akiwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari yake ya Mecca – Saudi
Arabia kwa ajili ya ibada ya UMRAH.
Rais
Azali Assouman pia amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano
zinazolenga kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za kijamii na
kusisitiza kuwa serikali yake itaendelea kujifunza kutoka Tanzania ili kutatua
changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Komoro.
Akitoa
ujumbe wa Rais JOHN MAGUFULI kwa Rais wa
Comoro Azali assouman, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amemhakikishia
Rais wa Comoro kuwa Tanzania itadumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo MBILI
hasa kwenye sekta za elimu, afya na biashara kwa ajili ya manufaa ya nchi hizo
MBILI.
Makamu wa Rais pia amemtakia Rais wa Comoro kheri
katika safari yake ya Mecca– Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Umrah.
Wakati
huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana
na kufanya mazungumzo na Balozi wa JAPAN hapa nchini Masaharu Yoshida na kumweleza
kuwa serikali itaendelea kuweka na kuboresha mazingira bora kwa ajili ya
wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali Duniani ikiwemo wawekezaji kutoka
nchini JAPAN.
Makamu
wa Rais amesema serikali ya JAPAN imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo kwa Tanzania
katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo Tanzania Bara na Visiwa hasa
kwenye sekta ya elimu, afya na maji na kusema jambo hilo ni zuri na lakuigwa na
washirika wengine wa maendeleo.
Kwa
upande wake Balozi wa Japan hapa nchini MASAHARU YOSHINDA amemhakikishia Makamu
wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN kuwa nchi yake itaendelea kufadhili ipasavyo miradi ya maendeleo hapa nchini ili
kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za kijamii.
No comments:
Post a Comment