Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 28 June 2016

TATIZO LA MIKOPO KWA WAFANYABIASHARA KUPATIWA UFUMBUZI


Na Immaculate Makilika- MAELEZO, tarehe 28/06/2016 Dar es salaam.

SERIKALI kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeandaa mkakati ya kulipatia ufumbuzi tatizo la ukosefu wa mikopo linalowakabili wafanyabiashara wengi nchini ili kusaidia uanzishwaji wa viwanda.

Hayo yamesemwa na Afisa Biashara wa Wizara hiyo Bw. Baruti Mwaigaga wakati akizungumza katika Viwanja vya Mwl Nyerere wakati wa maonesho ya Sabasaba yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam.

“Kufuatia kuwepo kwa tatizo kubwa la upatikanaji wa mikopo kwa watu wenye nia ya kuanzisha viwanda hapa nchini, Serikali imeandaa utaratibu maalumu wa kutoa taarifa zinazohusu upatikanaji wa mikopo ili kusaidia wananchi, kitu ambacho hakikuwepo awali” alisema Bw. Mwaigaga

Alisema lengo la mkakati huo ni kumrahisishia mwananchi mwenye nia ya kuanzisha kiwanda kupata taarifa sahihi ikiwa ni pamoja na utaratibu mzima wa kupata mkopo ambao unaondoa usumbufu kwa walengwa ikiwa ni utekelezaji wa nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Mikakati mingine ya Serikali katika kukuza sekta ya viwanda nchini ni pamoja na kuanzisha programu ya kuendeleza viwanda vidogo vidogo katika mikoa ya Ruvuma, Pwani, Iringa, Tanga na Manyara.

Naye, Afisa Uchumi kutoka Wizara hiyo Bw. Vicent Turuka alisema katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, Wizara inawaunganisha wafanyabiasha wadogo wadogo na wanunuzi wakuu na kuwapatia masoko ya mazao mfano zao la ufuta lina soko kwa kampuni ya Oramu pamoja na Murza Mills.

Aidha, wananchi wamesisitizwa kutembelea banda la Wizara ya Viwanda na Bishara  pamoja na taasisi zake za BRELA, TBS, TFDA , CBE na SIDO lililopo katika viwanja hivyo vya maonesho ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu namna za kufanya biashara pamoja na kuanzisha viwanda nchini.

No comments:

Post a Comment