Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki Balozi Augustine Maiga akitoa maelezo kwa wadau waliohudhuria mkutano wa Utawala wa Sheria na Utawala Bora (hawapo pichani) uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Maiga akiongea jambo na Balozi wa Italia Nchini Mhe. Luigi Scotto baada ya kumaliza mkutano wa Utawala wa Sheria na Utawala Bora uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
Wadau
wa Mkutano wa Utawala wa Sheria kutoka nchi mbalimbali duniani wakifatilia kwa
makini mkutano wa Utawala wa Sheria na Utawala Bora ili kufikia agenda ya mwaka 2030 na 2063 ya
malengo ya millennia uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
Picha
na Ally Daud- Maelezo
Na
Immaculate Makilika- MAELEZO
Dar es
Salaam
BARA la Afrika limetakiwa kuimarisha Utawala wa Sheria kupitia
vyombo vya dola ikiwemo mahakama na polisi ili kuisaidia mfumo huo kutetea maslahi ya wanyonge.
Hayo yamesemwa jana jijini Dar es
Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga wakati alipokuwa akifunga Mkutano wa siku
mbili wa Kimataifa kuhusu Utawala wa
Sheria na Utawala bora.
“Lazima Afrika iimarishe vyombo
vyake vinavyosimamia Utawala wa sheria na Utawala bora kama Polisi na Mahakama
pamoja na kuwa na msimamo wa Bara katika kuzungumzia masuala mbalimbali”
alisema Balozi Mahiga.
Balozi Maiga alisisitiza kuwa
rushwa imekua adui mkubwa katika Utawala wa Sheria, hivyo ni lazima suala hilo
lipatiwe ufumbuzi ili haki iweze kutendeka kwa watu wote.
Aidha, Balozi Maiga amemshukuru Balozi
wa Italia nchini Mhe. Luigi Scott kwa kufanikisha mkutano huo pamoja na Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Sheria (IDLO) Bibi. Irene Khani
kwa uamuzi wa wake wa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
“Mkutano huu ni wa kihistoria
utasaidia kuleta mageuzi katika Taasisi ama Vyombo vinavyosimamia masuala ya
Sera na Sheria ambayo yatachochea maendeleo mazuri katika nchi za Afrika”
alisema Balozi Mahiga.
Mkutano huo unaomalizika leo
ulikua na kauli mbiu isemayo “Kufikia agenda ya 2030 na agenda ya 2063: Utawala
wa Sheria kwa Maendeleo Endelevu ya Afrika”, umehusisha wadau mbalimbali
wakiwemo Mawaziri, kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Mabalozi kutoka ndani na
nje ya Afrika pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya kutetea Haki za Binadamu
ulimwenguni.
No comments:
Post a Comment