Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,
Amani Hassan (kulia) akimuonyesha mwananchi aliyetembelea Banda la Maonyesho la
jeshi hilo jinsi ya kutumia mtungi wa kuzimia moto wa awali, katika maadhimisho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto
na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji, Idd Chanyika (kulia) akitoa
maelezo jinsi ya vifaa vya kinga na tahadhari vinavyotumika kwa Kamishna wa
Utawala na Fedha wa Jeshi hilo, Michael Shija (kushoto), Kamishna wa Oparesheni,
Rogatius Kipali (wapili kushoto) na Naibu Kamishna wa Utawala naFedha, Billy Mwakatage
walipotembelea banda hilo Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini
Dar es Salaam.
Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Amani Hassan (kulia) akimuandikia mmoja ya mwananchi namba ya dharura 114 ambayo hutumika kupokea taarifa ya majanga mbalimbali kutoka kwa jamii.
Kamishna wa Oparesheni, Rogatius Kipali akisisitiza ufanyaji kazi kwa bidii, nidhamu, uadilifu na weledi kwa askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi waUumma inayofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala, jijini Dar es Salaam.
Banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
lililotumika kutoa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto na maokozi
lililopo katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala,
jijini Dar es Salaam. Picha zote na Godfrey Peter, Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji.
No comments:
Post a Comment