Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee, Flora Lauwo akipungia mkono alipokuwa akitambulishwa bungeni Dodoma.
Flora Lauwo akitafakari jambo alipokuwa akifuatilia mwenendo wa mijadala ya Bunge mjini Dodoma.
Flora Lauwo (kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula katika viwanja vya Bunge, Dodoma
Serikali
imetakiwa kuziangalia kwa jicho la tatu ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano
wa kuanza kutoa ruzuku kwa taasisi za watu binafsi zinazofanya kazi ya kufuatilia na kubaini matatizo
yanayowakumba wananchi kama afanyavyo, Flora Lauwo Mkurugenzi wa Taasisi ya
Nitetee.
Licha ya
serikali kutambua mchango unaotolewa na taasisi hizo, jamii nayo imeaswa kujitokeza kuwasaidia watu
ambao wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia ,maradhi na wale
wanaohitaji msaada wa kupata elimu .
Kufatia
serikali kutambua mchango huo baadhi ya wadau kutoka sekta binafsi wanajitokeza
na kubainisha changamoto zinazowakumba.
Yapo malengo
yanayowekwa na wadau hao ili kutimiza ndoto za kuwasaidia watanzania
“Lakini wapo
Wajanja ambao wamekuwa wakinufaisha na misaada wanayopewa na wafadhili badala
ya kuwasaidia walengwa,” alisema Lauwo.
Taasisi ya
nitetee inajishughulisha na utatuzi wa matatizo yanayozikumba familia zinazoishi katika mazingira magumu
ambapo mpaka sasa imeshazifikia kaya 36 pamoja na kuwapeleka watoto 20 shule.
No comments:
Post a Comment