Joseph Kony, kiongozi wa
kundi la waasi wa Uganda, L.R.A.
|
Kundi hilo la waasi wa Uganda linafahamika
kwa kushambulia na kufanya wizi wa ngawira katika vijiji na kulazimisha watoto
kujiunga nalo kama wapiganaji.
Jeshi la Uganda linasema
majeshi yake yamemkamata kamanda mmoja wa kundi la waasi la Lord’s
Resistance Army ( L.R.A.) Charles Okello na kuwaachia wengine 10 ambao
walishikiliwa mateka na kundi hilo la waasi.
Haya ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Uganda anayesema kukamatwa kwake kulifuatia kuzingirwa kwa kundi hilo katika maficho yao huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kundi hilo la waasi wa Uganda linafahamika kwa kushambulia na kufanya wizi wa ngawira katika vijiji na kulazimisha watoto kujiunga nalo kama wapiganaji.
Liliundwa kati kati ya miaka ya 1980 na lilipambana na serikali ya Uganda kwa miaka 20 kabla kukimbilia nchi jirani.
Majeshi ya Uganda yamekuwa yakiongoza operesheni za Umoja wa Afrika zinazoungwa mkono na Marekani ili kumkamata kiongozi wa kundi hilo, Joseph Kony na viongozi wengine
CHANZO , VOA SWAHILI
No comments:
Post a Comment