Afisa wa polisi akilinda mojawapo ya maeneo
katika jiji la Nairobi ambalo usalama wake unatatiza.
Watu wanne, wakiwemo
maafisa wawili wa polisi, wameuawa jana usiku mjini Nairobi baada ya gari
walilolizuia kulipuka, lilipokuwa likielekea katika kituo cha polisi katika
eneo la Pangani, jijini Nairobi.
Kulipatikana bomu la
pili katika gari hilo baada ya mlipuko huo na wataalamu wa mabomu waliliharibu.
Maafisa wa polisi
wanasema wanajaribu kuitambua miili ya washukiwa hao, usalama umeimarishwa
katika eneo hilo na polisi inaendelea kufanya uchunguzi.
Bosco Mugendi ana
kibanda cha kuuza vitu vidogovidogo karibu na lango la kuingia kwenye iituo cha
polisi cha Pangani kulikotokea mlipuko huo.
"kilie kingine
kilinikuta kwenye kibanda changu ni nyama ya watu ilinirukia halafu mimi
nikatoroka na kutoka nje," Bwana Muigendi alisema.
Mtaalamu wa maswala ya
usalama wa jijini Nairobi, George Musamali, aliambia BBC kuwa maafisa wa polisi
waliokuwa wakisindikiza gari kuelekea kituo hicho cha polisi walikuwa kwenye
gari la washukiwa ambalo lililipuka baadaye.
Chanzo bbcswahili
No comments:
Post a Comment