Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 14 April 2014

UNAMWAMINI HOUSE GIRL? MTAZAME ANAVYOMFANYA MWANAO

Tunawaamini wadada wa kazi (house girls) kwani wanatusaidia katika shughuli nyingi za familia. U-house girl ni kazi kama zilivyo kazi nyingine, ingawa wapo wanaoona kama kazi isiyofaa ama inayodharauliwa. 
Wapo wanafamilia ambao huwatenda visivyo wadada wa kazi, lakini pia wapo wadada wa kazi ambao wana roho za kinyama kama huyu anayeonekana kwenye clip hii ya video. 
Nyie akinadada wa kazi, tafadhali watendeeni watoto kwa wema, kuwatesa ni dhambi kubwa. Kama hamuelewani na waajiri wenu bora mtafute njia nyingine, lakini watoto hawana hatia yoyote jamani. Wewe uliyemwacha mtoto nyumbani na mdada wa kazi, anza kuchunguza kama mwanao anatendewa haki. 
Lakini vinginevyo, tusiwatese wadada wa kazi, ni binadamu wenye haki kama ilivyo wewe unayedai hata nyongeza ya mshahara kazini kwako. Tukiishi nao kama ndugu, naamini hawawezi kuwa na roho katili.

No comments:

Post a Comment