Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 14 April 2014

BOMU JINGINE ARUSHA



Watu kadhaa wamejeruhiwa kutokana na mlipuko unaodhaniwa kuwa ni wa bomu katika baa maarufu ya Arusha Night Park katika eneo la Mianzini katika jiji la Arusha.
Tukio hilo lilitokea jana saa mbili usiku wakati mamia ya watu wakiwa katika baa hiyo wakiangalia  mechi ya soka ya Ligi Kuu ya England kati ya Chelsea na Swansea. Chelsea ilishinda 1-0.
Mmoja wa wamiliki wa baa hiyo, AngeloMwoleka pia alithibitisha kutokea mlipuko huo na kueleza kujeruhiwa watu kadhaa.
“Ni kweli kuna mlipuko umetoka na watu kujeruhiwa, mimi sikuwepo ila nipo njiani nakwenda eneo la tukio, “alisema.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, John Lymo alisema watu saba waliumia vibaya kutokana na bomu hilo na walipelekwa katika Hospitali ya Mkoa Arusha ya Mount Meru.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus (pichani), alisema: “Hivi sasa tunaendelea na uokoaji na uchunguzi umeanza.”
Tukio hilo limekuja wakati bado jiji la Arusha likiwa na kumbukumbu ya kushambuliwa kwa mabomu kwa Kanisa la Mtakatifu JosephMfanyakazi lililopo eneo la Olasiti  na jingine Uwanja wa Soweto wakati Chadema walipokuwa wakifunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani. Katika matukio yote hayo, watu sita waliuawa na wengi kujeruhiwa.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment