Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 17 April 2014

MT MERU YAKABILIWA NA UKOSEFU WA VIFAA


Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha

HOSPITALI ya Mkoa  wa Arusha, Mount Meru, inakabiliwa na upungufu wa shuka 300 na blanketi 200, kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa kila siku.
Akizungumzia upungufu huo jana hospitalini hapo, wakati akipokea msaada wa shuka nyeupe 100 na blanketi 30 toka kwa Kanisa la Calvary Temple la Kilombero Jijini Arusha,ambalo linaadhimisha miaka 75 tangu lianzishwe, Mganga Mfawidi wa Hospitali hiyo, Dk. Josiah Mlay, alisema upungufu ni mkubwa wa vitu hivyo ukizingatia wanakwenda kipindi cha baridi kali.
Alisema kuwa shuka na blanketi walizonazo kwa sasa nyingi zimechakaa kutokana na kemikali wanazotumia kufulia wakati zinapochafuka wodini, hivyo wanahitaji shuka na blanketi zingine haraka kabla ya msimu wa baridi haujaanza.
"Kwa nyie kutuletea hivi vitu tunashukuru sana na mtabarikiwa, kwani bado tuna upungufu wa itu hivi mkubwa na tunaomba wadau wengine wajitokeze kutusaidia kabla ya msimu wa baridi haujaanza,"alisema.
Dk. Mlay alisema kwa sasa hospitali hiyo inachangamoto kubwa ya ongezeko la wagonjwa na huku mahitaji yao yakipungua, kutokana na wingi wao, hivyo wanahitaji wasamaria wema wajitokeze kuwasaidia.
Mahitaji mengine wanayohitaji hospitalini hapo alitaja kuwa pamoja na vifaa vya maabara navyo ni vichache,hivyo wanaomba msaada kwa wasamaria wema na sio kuiachia serikali ambayo inamajukumu mengi.
Kwa upande wake Emmanuel Mbwiga ambaye ni Mzee wa  Kanisa la Calvary Temple la Kilombero Jijini Arusha, akitoa msaada huo alisema mbali na msaada huo pia kupitia vituo vyao mbalimbali wametoa msaada kwenye vituo vya yatima vya Huruma Kwamurombo,Monduli,Esso.
Pia misaada mingine imetolewa shule za msingi Mwangaza, Olsinyai Sombetini na Ngarenaro, lengo kubwa kusaidia watu wenye shida ili wapate faraja nao katika kuadhimisha kilele cha kanisa hilo kitakachofanyika Kitaifa Mbeya Julai mwaka huu.
Mbwiga alisema vitu walivyotoa maeneo hayo  ni Sabuni, ndoo za mafuta, mchele, nguo, mahindi,daftari,soksi na vitu vingine vingi, ambavyo vyote vina jumla ya Shs. 3 milioni.
Hata hivyo alitoa wito kwa watu wenye mapenzi mema kujitokeza kusaidia hospitali hiyo na maeneo yenye uhitaji kama vitruo vya yatima na shuleni, ili wabarikiwe zaidi.

No comments:

Post a Comment