HALMASHAURI ya wilaya ya Arusha DC, imeziagiza shule za msingi katika halmashauri hiyo kufundisha masomo kwa njia ya picha ili kuongeza ufahamu na uelewa zaidi wanachofundishwa wanafunzi badala ya kuendelea na nadharia pekee .
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Arusha DC, Fidelis Lumato, alipokuwa akifungua mafunzo maalumu ya siku mbili ya ufundishaji wa masomo kutumia picha kwa shule za msingi ambayo yanaendeshwa na taasisi ya kimataifa ya elimu kwa njia ya picha (LTP).
Lumato, amesema zamani walimu walikuwa wakifundisha kwa kutumia vielelezo lakini sasa wanapaswa kubadilika na kufundisha kwa kutumia picha ambao mbinu hiyo inamuongezea maarifa zaidi na mwanafunzi hawezi kusahau akiona picha ya kitu alichojifunza .
Amesema kufundisha kwa kutunmia picha inaongeza uelewa na kukumbuka zaidi kwa kuwa picha zinaonyesha hali halisi ,na kuongeza kuwa ili mwalimu aweze kufundisha vizuri zaidi lazima kitabu kiwe na picha.
Mfumo huu wa kufundisha kutumia picha unasaidia kuboresha elimu katika shule na hivyo kuwezesha kufanya vizuri katika matokeo makubwa sasa RBN.
Kuhusu ufaulu wa wanafunzi katika shule za msingi amesema mwaka 2013 halmashauri hiyo ilifaulisha kwa asilimia 52% tu na malengo yalikuwa ni 62 % na mwaka huu imajipanga kufaulisha kwa asilimia 73 % na hiyo inatokana na kuimarisha ukaguzi na uboreshaji wa mazingira ya walimu.
Kuhusu vitabu vya kufundishia mkurugenzi huyo wa halmashauri ya wilaya ya Arusha DC, amesema kuwa halmashauri haina upungufu wa vitabu shuleni .
Kuhusu ujenzi wa maabara kwenye shule za sekondari, amesema kuwa halmashauri hiyo inazo shule za sekondari 26 na kati ya hizo zenye maabara ni shule sita tu.
Amesema kuwa kulingana na maelekezo ya serikali ifikapo Novemba mwaka huu kila shule ya sekondari lazima iwe na maabara hivyo akawaagiza waratibu elimu kata kukaa na kamati za maendeleo ya kata zao kuhakikisha ujenzi wa maabara unakamilika.
Amesema katika kuhakikisha hilo linatekelezeka halmashauri imetenga katika bajeti yake shilingi milioni 120 kwa ajili ya kukanmilisha ujenzi wa maabara utakaofanywa kwa nguvu za wananchi lengo ni kupata wataalamu wa sayansi.
Kuhusu matatizo yanayowakabili walimu hasa waliopo kwenye mazingira magumu, mkurugenzi huyo amesema halmashauri imejipanga kuyapatia ufumbuzi lengo ni kuwawezesha walimu kufanya kazi kwenye mazingira rafiki yanayovutia na hivyo kuongeza morari ya utendaji wao.
Naye mratibu wa Taasisi hiyo, Mwalimu Shaib Ibarahim Pele, amesema kuwa amesema taalumu hiyo ya ufundishaji wanafunzi kupitia picha kwa kutumia njia ya kusoma picha kwa makini na na kuziandikia habari na hadithi,au taarifa inamsaidia mwanafunzi kuelewa upesi anachofundishwa na hivyo kumfanya awe mbunifu.
Anmesema katika taaluma hiyo mwalimu na mwanafunzi watatumia vifaa kama vile picha za kuchora, kamera ,magazeti ambazo watazitumia kujieleza kwa kuziandikia maelezo
Pia mfumo huo unalenga kumpunguzia mwalimu majukumu na badala yake mwalimu atapata wasaa wa kupitia kazi za mwanafunzi kwa umakini , haraka na wepesi zaidi.
Awali mratibu wa mafunzo hayo, Evaresta Swai, ambae ni afisa elimu Vielelezo na Takwimu wa halmashauri ya Arusha DC, amesema kuwa mafunzo hayo yanafanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza imehusisha walimu 66 am,bao ni mabingwa wa masomo ya Hisabati, Uraia, Kiswahili na Kingereza, Sanyansi na History, kutoka shule za msingi kutoka kata 11 ,wakiwemo waratibu wa elimu kata, wakaguzi ,afisa utamaduni, tume ya walimu TSDC, na chama cha walimu CWT.
No comments:
Post a Comment