ANGELINA JOLIE AZALIWA
Tarehe
kama ya leo mwaka 1975, mwigizaji na mshindi wa Tuzo za Academy Agelina Jolie
(Voight) azaliwa jijini Los Angeles, California.
Baba
yake Jolie, mwigizaji Jon Voight, alikuwa ameteuliwa kuwania tuzo ya Best Actor
Oscar kupitia filamu ya Midnight Cowboy (1969); akatwaa
tuzo kwa filamu ya Coming
Home (1978). Mama
yake, Marcheline Bertrand, pia alikuwa mwigizaji; wawili hao walitalikiana
wakati Angela akiwa mchanga.
Akiwa
msichana mdogo, Angelina alifanya kazi kama mwanamitindo na akashiriki na baba
yake kwenye filamu ya mwaka 1982 ya Lookin’ to Get Out. Baadaye
akajifunza uigizaji katika kituo cha Lee Strasberg Theatre Institute na Chuo
Kikuu cha New
York. Baada ya kushiriki sehemu ndogo ya filamu ya Cyborg 2(1993), Jolie akapata mkataba mnono katika
filamu maarufu ya Hackers (1995), ambayo
ilimshirikisha mwigizaji wa Uingereza Jonny Lee Miller. Jolie na Miller wakaoana
mwaka huo baada ya kumaliza kucheza filamu lakini wakatengana mwaka 1997 na
baadaye kutalikiana.
Baada ya
mfululizo wa filamu, Jolie akateuliwa kuwania tuzo za Emmy na akatwaa tuzo ya Golden
Globe baadaya ya kushiriki kama mke wa gavana mkorofi wa Alabama, katika filamu
ya luninga ya George
Wallace.
Hatimaye,
akiwa anang’ara na watu wakimhitaji acheze filamu zao, Jolie akapata mikataba
mikubwa na kushiriki filamu kama Playing By Heart (1998), Pushing
Tin (1999) na The
Bone Collector (1999).
Umahiri
wa Jolie akicheza kama Lisa katika filamu ya Girl, Interrupted, ndio
hasa uliomwingiza kwenye daraja A la nyota wa Hollywood. Alitwaa tuzo ya
Academy katika kitengo cha Best Supporting Actress kwa nafasi aliyocheza, na
akazusha maswali mengi baada ya kunyonyana ndimi na kaka yake mkubwa, James
Haven, wakati wa sherehe za Tuzo za Oscar mwaka 2000.
Mwezi
Mei mwaka huo, Jolie akapamba vichwa ya habari baada ya kufunga ndoa na Billy
Bob Thornton, ambaye walicheza naye kwenye filamu ya Pushing
Tin (1999), katika
sherehe ndogo jijini Las
Vegas. Hata hivyo, walitalikiana mwaka 2002 kabla ya kuoana na
Brad Pitt baada ya kucheza wote filamu ya Mr
& Mrs Smith mwaka 2004. Tetesi zilizidi wakati wakiigiza filamu hiyo
kwamba walikuwa na uhusiano, na zilizidi baada ya Brad Pitt kutengana na mkewe
Jennifer Aniston Januari 2005.
Mwaka
2003 alimuasili mtoto Maddox wa Cambodia na mwaka 2005 akamuasili Zahara kutoka
Ethiopia. Mei 2006 alijifungua mtoto aitwaye Shiloh Nouvel Jolie-Pitt wakati
akiwa Namibia.
Jolie
alimuasili mtotoo mwingine wa kiume, Pax Thien, kutoka kituo cha watoto yatima
nchini Vietnam Machi 2007; na Julai 2008 akajifungua watoto mapacha - Knox Leon
na Vivienne Marcheline, akiwa nchini Ufaransa.
04/06/1933
STEPHEN JONES GALINOMA
Alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1933 mkoani Iringa. Alikuwa miongoni
mwa wabunge wenye umri mkubwa zaidi hadi kufikia mwaka 2010, lakini akatangaza
mapema kwamba asingegombea katika Jimbo la Kalenga kutokana na umri, hasa baada
ya kuliwakilisha jimbo hilo tangu mwaka 1995. Elimu ya msingi aliipata katika
shule ya Kalenga (1943 hadi 1948 - Darasa la Nne), akajiunga na shule ya
sekondari ya Malangali kati ya mwaka 1949 na 1952 kabla ya kujiunga na mafunzo
ya Cheti katika Masuala ya Umma na Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Princeton,
Marekani (1966 na 1967) na mwaka 1978 akapata mafunzo ya Cheti katika Rasilimali
Watu katika Chuo Kikuu cha Harvard, Marekani.
Aliajiriwa kama Karani wa Serikali (1952 hadi 1959 - ya Kikoloni wakati
huo), Ofisa wa Serikali wa Wilaya na Hakimu (1959 hadi 1960), Kamishna wa
Wilaya (1961 hadi 1962), Katibu Tawala wa Jimbo la Kusini (1963 hadi 1964),
Katibu Mkuu Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais (1964 hadi 1968), Katibu Tawala wa
Mkoa (1968 hadi 1972), Mkurugenzi (1972 hadi 1976), Mwenyekiti wa SCOPO (1978
hadi 1980), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi (1980 hadi 1991).
Alifariki dunia Januari 26,2012.
RUSSELL BRAND
Leo hii Juni 4, mcheza filamu huyu mzaliwa wa England mwaka 1975
anatimiza miaka 39. Huyu ni mwigizaji wa vichekesho ambaye alijipatia umaarufu
mkubwa kwa staili yake ya uchekeshaji katika vipindi vya tamthilia vya luninga
kama Forgetting Sarah Marshall na Get Him to the Greek. Pia
alishiriki katika tamthiliya za Despicable Me 2, Bedtime Stories, na Penelope.
Alisomea uigizaji katika Kituo cha Drama Centre
London, ambako alifukuzwa wakati yuko mwaka wa mwisho.
Alianza rasmi shughuli hiyo akiwa mwandishi wa
video kwa ajili ya kituo cha MTV.
Kutoka na tabia ya utukutu na utumiaji wa vileo na dawa za kulevya,
akahudhuria mikutano ya mijadala ya ngono, dawa za kulevya na ulevi na akatumia
Kundalini Yoga ili kujitibu na uraibu uliokuwa umemtinga.
Alimuoa mwimbaji Katy Perry mwaka 2010, lakini ndoa yao ilidumu kwa
miezi 14 tu.
Kwenye mchezo wa vichekesho wa Get Him to the Greek, alicheza pamoja na
Jonah Hill.
MOLLIE KING
Mwanamuziki wa Kiingereza kutoka kundi la The Saturdays aliyezaliwa
tarehe kama ya leo mwaka 1987 ambaye leo hii anatimiza miaka 27. Pia anajishughulisha
ama kumilikia kampuni yake ya mitindo iitwayo Loved by
Mollie.
Kabla ya kuwa maarufu alisomea saikolojia na
biashara, japokuwa amekuwa akisumbuliwa na dyslexia.
Wakati akiwa na miaka 19 nusuru atwae taji la
urembo la Miss Guildford.
Baada ya kupata umaarufu, bendi yake ya The
Saturdays ilipata mikataba ya kupiga picha za kampuni za Veet na T-Mobile.
Amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwimbaji kiongozi wa bendi hiyo
Lawson, lakini pia amekuwa na uhusiano na Andy Brown, pamoja
na John Mayer.
Tanu Februari 2013, alianza uhusiano wa kimapenzi
na Jordan Omley.
LUKAS PODOLSKI
Mshambiliaji
mahiri wa Arsenal ya England aliyojiunga nayo mwaka 2012 baada ya kuzichezea
klabu za Bayern Munich na FC Koln. Alizaliwa Poland tarehe kama ya leo mwaka
1985 ambapo leo ametimiza miaka 29.
Pamoja
na kwamba ni Mpoland, lakini alianza kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani tangu
mwaka 2004 na wakati wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2006 nchini Ujerumani,
alitwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo zaidi wa mashindano.
Alianza kucheza soka yake ya utotoni mwaka 1991 (akiwa na miaka sita
tu) alipojiunga na klabu ya FC 07 Bergheim. Alikuwa
na uwezo wa kuchezea nchi zote Ujerumani na Poland, lakini akachagua Ujerumani.
Mwaka 2011 alimuoa Monika Puchalski.
GEORGE III
Mfamle huyu wa Uingereza na Ireland
wakati wa karne ya 18 alizaliwa Juni 4, 1738 huko England. Ndiye mfalme pekee
wa karne hiyo ambaye maisha yake na utawala wake ulikuwa mrefu zaidi yaw engine
waliomtangulia katika Ufalme wa Uingereza.
Ingawa aliipiga na
kuishinda Ufaransa katika Vita ya Miaka Saba, lakini akajikuta akipoteza koloni
la Uingereza la Marekani katika Vita ya Mapinduzi ya Marekani.
Alikuwa mfalme wa kwanza wa Uingereza
kusoma sayansi kwa ustadi na mbali ya masomo ya kemia na fizikia, masomo mengine yalikuwa elimu ya nyota (astronomy), hisabati,
Kifaransa, Kilatino, historia, muziki, jiografia, biashara, kilimo na sheria ya
katiba.
Alikuwa mfalme wa kwanza wa Uingereza
kutoka House of Hanover kuzungumza Kiingereza kama lugha
yake ya kwanza.
Mdogo wake alikuwa Prince Edward, Duke
wa York na Albany.
BRADLEY WALSH
Mwigizaji
wa luninga aliyezaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1960 nchini England. Ametimiza miaka
54. Kwa sasa anawakilisha nafasi ya Ronnie Brooks kwenye vipindi vya luninga
vya, Law & Order: UK akicheza pamoja
na Jamie Bamber. Awali alicheza katika tamthiliya ya Kiingereza ya Night and
Day.
Alianzia kucheza soka ya Kimarekani, lakini
akaamua kukimbilia kwenye televisheni na kupata umaarufu akiwa mtangazaji wa
kipindi cha The National Lottery. Aliwahi kuongoza kipindi cha Wheel of
Fortune.
Alifunga ndoa na Donna Derby mwaka 1997 na wana mtoto mmoja wa kiume. Katika
kipindi cha luninga cha Coronation Street aliigiza kama Danny akiwa sanjari na
mwigizaji Ryan Thomas.
KEITH DAVID
Mwigizaji wa filamu aliyezaliwa mjini New York tarehe kama ya leo mwaka
1956. Ni mwigizaji mwenye sauti nzito ambaye amekuwa akiigiza kama mwenza. Alifahamika
zaidi kwa ushiriki wake wa filamu ya Platoon ya mwaka 1986 na filamu ya Crash
ya mwaka 2004.
Aliigia kama Imam katika filamu ya kubuni ya Pitch Black.
Alianza kuigiza akiwa na miaka 23 katika filamu ya Disco Godfather ya
mwaka 1979. Mwaka 1982 aliigiza na Kurt Russell katika filamu ya kutisha ya The
King.
Alitwaa tuzo mbili za Primetime Emmy Awards kwa
kuigiza sauti kwenye filamu ya The War ya mwaka 2007 na ile ya Unforgivable
Blackness: The Rise and Fall of Jack Johnson.
Alimuoa na baadaye kumtaliki mwigizaji Margit
Edwards Williams.
ROSALIND RUSSELL
Mwanamama
huyu mwigizaji aliyezaliwa Connecticut tarehe kama ya leo mwaka 1907, alifariki
dunia Novemba 28, 1976 akiwa na miaka 69.
Alikuwa mwigizaji mahiri aliyeshiriki
katika flamu za vichekesho kama Auntie Mame na filamu ya mwaka 1940 ya His Girl Friday. Mwaka 1939 alishiriki katika filamu ya
The Women akiwa na Joan Crawford.
Alitwaa Tuzo ya
Tony kwa uigizaji wake mzuri kwenye filamu ya Wonderful Town.
Kabla hajawa maarufu alikuwa amepanga
kuwa mchekeshaji wa jukwaani.
Aliteuliwa na kushinda Tuzo tano za Golden Globe.
Aliolewa na Frederick
Brisson mwaka 1941, na wawili hao walijaliwa mtoto wa kiume aitwaye Lance mwaka
1943.
No comments:
Post a Comment