Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 4 June 2014

'HAPPY BIRTHDAY' ANGELINA JOLIE, LUKAS PODOLSKI, GALINOMA


ANGELINA JOLIE AZALIWA


Tarehe kama ya leo mwaka 1975, mwigizaji na mshindi wa Tuzo za Academy Agelina Jolie (Voight) azaliwa jijini Los Angeles, California.
Baba yake Jolie, mwigizaji Jon Voight, alikuwa ameteuliwa kuwania tuzo ya Best Actor Oscar kupitia filamu ya Midnight Cowboy (1969); akatwaa tuzo kwa filamu ya Coming Home (1978). Mama yake, Marcheline Bertrand, pia alikuwa mwigizaji; wawili hao walitalikiana wakati Angela akiwa mchanga.
Akiwa msichana mdogo, Angelina alifanya kazi kama mwanamitindo na akashiriki na baba yake kwenye filamu ya mwaka 1982 ya Lookin’ to Get Out. Baadaye akajifunza uigizaji katika kituo cha Lee Strasberg Theatre Institute na Chuo Kikuu cha New York. Baada ya kushiriki sehemu ndogo ya filamu ya Cyborg 2(1993), Jolie akapata mkataba mnono katika filamu maarufu ya Hackers (1995), ambayo ilimshirikisha mwigizaji wa Uingereza Jonny Lee Miller. Jolie na Miller wakaoana mwaka huo baada ya kumaliza kucheza filamu lakini wakatengana mwaka 1997 na baadaye kutalikiana.
Baada ya mfululizo wa filamu, Jolie akateuliwa kuwania tuzo za Emmy na akatwaa tuzo ya Golden Globe baadaya ya kushiriki kama mke wa gavana mkorofi wa Alabama, katika filamu ya luninga ya George Wallace.
Hatimaye, akiwa anang’ara na watu wakimhitaji acheze filamu zao, Jolie akapata mikataba mikubwa na kushiriki filamu kama Playing By Heart (1998), Pushing Tin (1999) na The Bone Collector (1999).
Umahiri wa Jolie akicheza kama Lisa katika filamu ya Girl, Interrupted, ndio hasa uliomwingiza kwenye daraja A la nyota wa Hollywood. Alitwaa tuzo ya Academy katika kitengo cha Best Supporting Actress kwa nafasi aliyocheza, na akazusha maswali mengi baada ya kunyonyana ndimi na kaka yake mkubwa, James Haven, wakati wa sherehe za Tuzo za Oscar mwaka 2000.
Mwezi Mei mwaka huo, Jolie akapamba vichwa ya habari baada ya kufunga ndoa na Billy Bob Thornton, ambaye walicheza naye kwenye filamu ya Pushing Tin (1999), katika sherehe ndogo jijini Las Vegas. Hata hivyo, walitalikiana mwaka 2002 kabla ya kuoana na Brad Pitt baada ya kucheza wote filamu ya Mr & Mrs Smith mwaka 2004. Tetesi zilizidi wakati wakiigiza filamu hiyo kwamba walikuwa na uhusiano, na zilizidi baada ya Brad Pitt kutengana na mkewe Jennifer Aniston Januari 2005.
Mwaka 2003 alimuasili mtoto Maddox wa Cambodia na mwaka 2005 akamuasili Zahara kutoka Ethiopia. Mei 2006 alijifungua mtoto aitwaye Shiloh Nouvel Jolie-Pitt wakati akiwa Namibia.
Jolie alimuasili mtotoo mwingine wa kiume, Pax Thien, kutoka kituo cha watoto yatima nchini Vietnam Machi 2007; na Julai 2008 akajifungua watoto mapacha - Knox Leon na Vivienne Marcheline, akiwa nchini Ufaransa.


04/06/1933
STEPHEN JONES GALINOMA


Alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1933 mkoani Iringa. Alikuwa miongoni mwa wabunge wenye umri mkubwa zaidi hadi kufikia mwaka 2010, lakini akatangaza mapema kwamba asingegombea katika Jimbo la Kalenga kutokana na umri, hasa baada ya kuliwakilisha jimbo hilo tangu mwaka 1995. Elimu ya msingi aliipata katika shule ya Kalenga (1943 hadi 1948 - Darasa la Nne), akajiunga na shule ya sekondari ya Malangali kati ya mwaka 1949 na 1952 kabla ya kujiunga na mafunzo ya Cheti katika Masuala ya Umma na Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Princeton, Marekani (1966 na 1967) na mwaka 1978 akapata mafunzo ya Cheti katika Rasilimali Watu katika Chuo Kikuu cha Harvard, Marekani.
Aliajiriwa kama Karani wa Serikali (1952 hadi 1959 - ya Kikoloni wakati huo), Ofisa wa Serikali wa Wilaya na Hakimu (1959 hadi 1960), Kamishna wa Wilaya (1961 hadi 1962), Katibu Tawala wa Jimbo la Kusini (1963 hadi 1964), Katibu Mkuu Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais (1964 hadi 1968), Katibu Tawala wa Mkoa (1968 hadi 1972), Mkurugenzi (1972 hadi 1976), Mwenyekiti wa SCOPO (1978 hadi 1980), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi (1980 hadi 1991).
Alifariki dunia Januari 26,2012.


RUSSELL BRAND


Leo hii Juni 4, mcheza filamu huyu mzaliwa wa England mwaka 1975 anatimiza miaka 39. Huyu ni mwigizaji wa vichekesho ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kwa staili yake ya uchekeshaji katika vipindi vya tamthilia vya luninga kama Forgetting Sarah Marshall na Get Him to the Greek. Pia alishiriki katika tamthiliya za Despicable Me 2, Bedtime Stories, na Penelope.
Alisomea uigizaji katika Kituo cha Drama Centre London, ambako alifukuzwa wakati yuko mwaka wa mwisho.
Alianza rasmi shughuli hiyo akiwa mwandishi wa video kwa ajili ya kituo cha MTV.
Kutoka na tabia ya utukutu na utumiaji wa vileo na dawa za kulevya, akahudhuria mikutano ya mijadala ya ngono, dawa za kulevya na ulevi na akatumia Kundalini Yoga ili kujitibu na uraibu uliokuwa umemtinga.
Alimuoa mwimbaji Katy Perry mwaka 2010, lakini ndoa yao ilidumu kwa miezi 14 tu.
Kwenye mchezo wa vichekesho wa Get Him to the Greek, alicheza pamoja na Jonah Hill.


MOLLIE KING


Mwanamuziki wa Kiingereza kutoka kundi la The Saturdays aliyezaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1987 ambaye leo hii anatimiza miaka 27. Pia anajishughulisha ama kumilikia kampuni yake ya mitindo iitwayo Loved by Mollie.
Kabla ya kuwa maarufu alisomea saikolojia na biashara, japokuwa amekuwa akisumbuliwa na dyslexia.
Wakati akiwa na miaka 19 nusuru atwae taji la urembo la Miss Guildford.
Baada ya kupata umaarufu, bendi yake ya The Saturdays ilipata mikataba ya kupiga picha za kampuni za Veet na T-Mobile.
Amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwimbaji kiongozi wa bendi hiyo Lawson, lakini pia amekuwa na uhusiano na Andy Brown, pamoja na John Mayer.
Tanu Februari 2013, alianza uhusiano wa kimapenzi na Jordan Omley.


LUKAS PODOLSKI


Mshambiliaji mahiri wa Arsenal ya England aliyojiunga nayo mwaka 2012 baada ya kuzichezea klabu za Bayern Munich na FC Koln. Alizaliwa Poland tarehe kama ya leo mwaka 1985 ambapo leo ametimiza miaka 29.
Pamoja na kwamba ni Mpoland, lakini alianza kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani tangu mwaka 2004 na wakati wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2006 nchini Ujerumani, alitwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo zaidi wa mashindano.
Alianza kucheza soka yake ya utotoni mwaka 1991 (akiwa na miaka sita tu) alipojiunga na klabu ya FC 07 Bergheim. Alikuwa na uwezo wa kuchezea nchi zote Ujerumani na Poland, lakini akachagua Ujerumani.
Mwaka 2011 alimuoa Monika Puchalski.


GEORGE III


Mfamle huyu wa Uingereza na Ireland wakati wa karne ya 18 alizaliwa Juni 4, 1738 huko England. Ndiye mfalme pekee wa karne hiyo ambaye maisha yake na utawala wake ulikuwa mrefu zaidi yaw engine waliomtangulia katika Ufalme wa Uingereza.
Ingawa aliipiga na kuishinda Ufaransa katika Vita ya Miaka Saba, lakini akajikuta akipoteza koloni la Uingereza la Marekani katika Vita ya Mapinduzi ya Marekani.
Alikuwa mfalme wa kwanza wa Uingereza kusoma sayansi kwa ustadi na mbali ya masomo ya kemia na fizikia, masomo mengine yalikuwa elimu ya nyota (astronomy), hisabati, Kifaransa, Kilatino, historia, muziki, jiografia, biashara, kilimo na sheria ya katiba.
Alikuwa mfalme wa kwanza wa Uingereza kutoka House of Hanover kuzungumza Kiingereza kama lugha yake ya kwanza.
Mdogo wake alikuwa Prince Edward, Duke wa York na Albany.


BRADLEY WALSH



Mwigizaji wa luninga aliyezaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1960 nchini England. Ametimiza miaka 54. Kwa sasa anawakilisha nafasi ya Ronnie Brooks kwenye vipindi vya luninga vya, Law & Order: UK akicheza pamoja na Jamie Bamber. Awali alicheza katika tamthiliya ya Kiingereza ya Night and Day.
Alianzia kucheza soka ya Kimarekani, lakini akaamua kukimbilia kwenye televisheni na kupata umaarufu akiwa mtangazaji wa kipindi cha The National Lottery. Aliwahi kuongoza kipindi cha Wheel of Fortune.
Alifunga ndoa na Donna Derby mwaka 1997 na wana mtoto mmoja wa kiume. Katika kipindi cha luninga cha Coronation Street aliigiza kama Danny akiwa sanjari na mwigizaji Ryan Thomas.


KEITH DAVID


Mwigizaji wa filamu aliyezaliwa mjini New York tarehe kama ya leo mwaka 1956. Ni mwigizaji mwenye sauti nzito ambaye amekuwa akiigiza kama mwenza. Alifahamika zaidi kwa ushiriki wake wa filamu ya Platoon ya mwaka 1986 na filamu ya Crash ya mwaka 2004.
Aliigia kama Imam katika filamu ya kubuni ya Pitch Black.
Alianza kuigiza akiwa na miaka 23 katika filamu ya Disco Godfather ya mwaka 1979. Mwaka 1982 aliigiza na Kurt Russell katika filamu ya kutisha ya The King.
Alitwaa tuzo mbili za Primetime Emmy Awards kwa kuigiza sauti kwenye filamu ya The War ya mwaka 2007 na ile ya Unforgivable Blackness: The Rise and Fall of Jack Johnson.
Alimuoa na baadaye kumtaliki mwigizaji Margit Edwards Williams.


ROSALIND RUSSELL


Mwanamama huyu mwigizaji aliyezaliwa Connecticut tarehe kama ya leo mwaka 1907, alifariki dunia Novemba 28, 1976 akiwa na miaka 69.
Alikuwa mwigizaji mahiri aliyeshiriki katika flamu za vichekesho kama Auntie Mame na filamu ya mwaka 1940 ya His Girl Friday. Mwaka 1939 alishiriki katika filamu ya The Women akiwa na Joan Crawford.
Alitwaa Tuzo ya Tony kwa uigizaji wake mzuri kwenye filamu ya Wonderful Town.
Kabla hajawa maarufu alikuwa amepanga kuwa mchekeshaji wa jukwaani.
Aliteuliwa na kushinda Tuzo tano za Golden Globe.
Aliolewa na Frederick Brisson mwaka 1941, na wawili hao walijaliwa mtoto wa kiume aitwaye Lance mwaka 1943.



No comments:

Post a Comment