Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 15 April 2014

TUNDU LISSU TENA!


Tundu Antipas Lissu

Dodoma/Dar. Mjumbe wa Bunge la Katiba, Tundu Lissu amesema Tanganyika ilikufa kwa amri iliyotolewa na Mwalimu Julius Nyerere na siyo kwa makubaliano katika hati ya Muungano.
Lissu alitoa kauli hiyo jana alipopata fursa ya kukamilisha dakika 16 za hotuba yake ya ufafanuzi wa maoni ya walio wachache iliyokuwa imekatishwa baada ya matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni ya Taifa (TBC1) kukatika Jumamosi iliyopita.
Huku akinukuu maneno yaliyopo katika vitabu vilivyoandikwa na Profesa Issa Shivji na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa, Lissu alisema Jamhuri ya Muungano ilizaliwa bila uhalali wa kisheria kwa kuwa hayakuwapo makubaliano ya kila upande wa Muungano.
Alisema Aprili 26, 1964 (Siku ya Muungano), Mwalimu Nyerere alitoa amri ya masharti ya mpito ya mwaka 1964 ambayo pamoja na mambo mengine iliifuta Tanganyika. Akichambua kitabu cha ‘50 Years of Independence: A ConcisePolitical History of Tanzania’ (Miaka 50 ya Uhuru: Historia fupi ya Tanzania), kilichoandikwa na Msekwa na kuchapishwa Januari mwaka huu, Lissu alisema:
“Msekwa anasema katika kitabu hicho kuwa amri hiyo ilichapishwa katika Gazeti la Serikali la siku hiyo. Kwanza, iliwabadilisha waliokuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika kuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.”
Alisema hata Mahakama Kuu ya Tanganyika iligeuzwa kuwa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano na nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Tanganyika iligeuzwa kuwa nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano.
Alisema tarehe hiyohiyo, Mwalimu Nyerere alitoa amri ya Katiba ya muda ya mwaka 1964 na ilitangaza kuwa Katiba ya Tanganyika ndiyo iwe Katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano.
“Kifungu cha nne cha amri hii ndicho kilichoipatia Serikali ya Muungano majukumu kuhusu mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano yote na vilevile kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano kwa upande wa Tanganyika,” alisema Lissu huku akishangiliwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo.
Alisema Juni 15, 1964, Mwalimu Nyerere alitoa amri nyingine iliyoitwa ‘Amri ya Masharti ya Mpito’ ambayo ilieleza kwamba mahali popote ambako sheria zilizokuwapo zimetaja jina la ‘Tanganyika’ basi jina hilo lifutwe na badala yake jina la ‘Jamhuri ya Muungano’ liwekwe.
Huku akimnukuu Msekwa, Lissu alisema kigogo huyo wa CCM katika kitabu chake amesema, “Uhai wa Tanganyika ulitolewa kwa njia hiyo ya amri. Athari za jumla za amri hizi ni kwamba eneo la kisiasa ambalo ndiyo ilikuwa Tanganyika lilitolewa uhai wake moja kwa moja kwa amri. Hii ndiyo sababu hata jina la eneo la kijiografia lililojulikana zamani kama Tanganyika ilibidi libadilishwe na kuwa Tanzania Bara.”
Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Lissu aliyoitoa jana, Msekwa alisema: “Kitabu kipo na ukikisoma kwa umakini utagundua kuwa alichokisema Lissu siyo ambacho kimeandikwa. Sasa umhoji kuhusu hayo aliyoyasema, muulize ameyapata wapi?”
Kuhusu Shivji
Akimnukuu Profesa Shivji katika kitabu chake ‘Pan Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika – Zanzibar Union’, Lissu alisema Profesa huyo ameeleza kuwa Muungano huo ulilazimishwa.
“Profesa Shivji amethibitisha kwamba kile kinachoitwa Sheria ya Kuthibitisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964 iliandaliwa na kuandikwa na maofisa wa sheria wa Tanganyika wakiwa Tanganyika,” alisema.
Alisema kuwa Profesa huyo ameeleza sababu ya ukweli wa kisiasa uliokuwapo wakati huo ambao Baraza la Mapinduzi kwa jumla wake halikukaa kuukubali Muungano.
“Profesa Shivji alisema hakuna shaka kwamba Muungano ‘ulilazimishwa.’ Hivyo, maofisa wa kisheria wa kigeni wa Serikali ya Tanganyika (waliokuwa pia marafiki wa Nyerere) walitumia mbinu ya kisheria ya kuchapisha Sheria ya kuthibitisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mwaka 1964,” alisema huku akikatishwa mara kwa mara na wajumbe waliokuwa wakiomba miongozo ya mwenyekiti.
“Profesa ameeleza kuwa, kwa sababu utaratibu huo ulikiukwa, kitendo cha kuunganisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika hakikupata baraka za Baraza la Mapinduzi na kuthibitishwa na kikao halali cha Baraza la Mawaziri la Zanzibar,” alisema Lissu na kuongeza: “Jamhuri ya Muungano ilizaliwa bila uhalali wowote wa kisheria kwa maneno ya Profesa Shivji.”
Alisema hata aliyekuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Salim Said Rashid kati ya Januari 18 na Juni 1964, alitamka kuwa:
“Hakuwahi kupokea maagizo kutoka kwa Rais wa Zanzibar kwa ajili ya kuitisha kikao cha kujadili na kupitisha mkataba wa kuunganisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika,” alisema Lissu.
Alisema katika kitabu hicho, Profesa Shivji alieleza jinsi Rashid alivyoeleza utaratibu wa kisheria uliotakiwa kufuatwa: “... Kwa mujibu wa amri ya mwaka 1964; kila jambo lilitakiwa kujadiliwa na kikao cha Baraza la Mapinduzi na Mwanasheria Mkuu kuarifiwa atayarishe ‘presidential decree’ kwa mujibu wa utaratibu.”
Alisema baadaye yeye (Rashid), akiwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawaziri Zanzibar alitakiwa asaini na kisha Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na baadaye kutolewa katika gazeti la Serikali.
Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa kauli hiyo ya Lissu kuhusu kitabu chake, Profesa Shivji alijibu kwa ujumbe mfupi wa maneno akisema: “Itakuwa vizuri ukisoma wewe mwenyewe.”
Mbowe: Takwimu za Tume zimetengenezwa na vigogo wa Serikali
Akichangia maoni ya walio wachache kutoka Kamati Namba Nane, Freeman Mbowe alisema kitendo cha wajumbe wanaotokana na CCM kubeza takwimu za Tume ya Jaji Joseph Warioba ni kuwakana Watumishi wa Serikali akisema ilikuwa na watumishi wa Serikali 190 wakiwamo wanasheria waandamizi.

No comments:

Post a Comment