Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alifunga mabao 2 katika kipindi cha kwanza baada ya bao la kusawazisha lake Joel Matip, huku Fred na Fernandinho wakihakikishia timu hiyo nafasi katika mkondo wa pili wa timu 16 bora kama washindi wa kundi A.
Matokeo duni dhidi ya Croatia na Mexico yameibua wasiwasi kuhusu Brazil - na hofu inasalia katika safu yao ya ulinzi - lakini Neymar akiwepo, chochote chaweza kutokea.Kushiriki kwa Brazil katika robo fainali kunategemea mechi yao dhidi ya Chile katika robo fainali, na Brazil watakwenda katika mechi hiyo itakayochezewa jijini Belo Horizonte siku ya Jumamosi wakiwa na imani mpya ya kunyakua taji hilo.
Mshambulizi huyo wa Barcelona alirejea na bao dhidi ya Japan katika mechi ya ufunguzi katika mechi ya kwanza ya Kombe la Mashirika la mwaka uliopita, ambayo iliisaidia Brazil kuanza kwa ushindi ili kunyakua taji hilo, na kocha Luiz Felipe Scolari atatumai kuwa matokeo haya yatakuwa na athari sawa.
Brazil ilikuwa karibu kupata bao la kwanza mkwaju wake Paulinho ulipozuiliwa baada ya Hulk kumpigia pasi iliyokuwa imetoka kwake Neymar, lakini tamaa yao ya kushambulia ikawafanya kusahau safu ya ulinzi, ambayo Cameroon ilonekana kutaka kutumia.
Marcelo aliokoa mkwaju ambao angefunga Vincent Aboubakar kabla ya David Luiz kulazimika kuondoa mkwaju aliokuwa ameupiga Eric Choupo Moting katika eneo la lango.
Hata hivyo, Brazil walionekana wasiokata tamaa, Luiz Gustavo alipata mpira katika ubavu wa kushoto na kumpigia pasi Neymar ambaye alimpiku Charles Itandje na kufunga bao.
Ilikuwa njia nzuri ya kuandikisha bao la 100 katika Kombe la Dunia - na mchezaji yuyo huyo alikaribia kufunga bao la pili ambalo Itandje aliondoa.
Uwanja uliokuwa umejaa kelele ulinyamaza kimya wakati Cameroon walipoweka wazi safu hafifu ya ulinzi ya Brazil, Nyom akimpiku Dani Alves na kumpigia pasi Matip aliyefunga kwa karibu.
Scolari aliwaashiria wachezaji wake, nao wakamjibu kwa njia ya pekee wanayojua, Marcelo kumpigia Neymar pasi ambaye alikimbia na kuwapiga chenga mabeki 2 wa Cameroon na kufunga bao lake la 35 katika mechi 52 za kimataifa.
Scolari alimwondoa Paulinho na kumweka Fernandinho wakati wa mapumziko .
Kiungo huyo wa Manchester City alichangia nipe nikupe iliyozaa bao lake Fred .
Fernandinho alifunga bao la nne na kuonyesha kuwa kuwepo kwake kulichangia ushindi huo.
Katika hatua nyingine, Uholanzi ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi B kufuatia ushindi wa mabao 2-0 katika mechi yao ya mwisho ya makundi.
Mabao ya Uholanzi yaliyofungwa na Leroy Fern na Memphis Depay yaliyowapa ushindi dhidi ya Chile katika mechi ngumu iliyochezewa jijini Sao Paulo.
Mechi hiyo ilikosa msisimko na kuishia sufuri bin suifuri kufikia muda wa mapumziko ,Lakini Fer alifunga kwa kichwa katika dakika ya 77, kabla ya Depay kufunga katika dakika ya mwisho.Timu zote mbili zilikuwa tayari zimefuzu kwa raundi ya pili baada ya kushinda mechi zao za kwanza dhidi ya Uhispania na Australia.
Huenda Chile wakachuana na Brazil katika mechi za muondoano, huku upande wa Luiz Van Gaal ukitarajia kuchuana na aidha Mexico au Croatia.
Uholanzi ilikuwa bila mshambulizi Robin Van Persie ambaye alikuwa anatumikia marufuku baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.
Chile nayo ilimpumzisha kiungo cha kati Arturo Vidal ambaye kukosekana kwake kuliadhiri mchezo, kwani ilichukua muda kabla ya walinda lango kuugusa mpira.
Mshambulizi wa Barcelona Alexis Sanchez alionekana kutaka kufunga bao la kwanza kwa Chile kwa weledi wake na pasi ambazo ziliwahangaisha mabeki wa Uholanzi kwa muda.
Arjen Robben alikuwa karibu kuendeleza rekodi yake ya kufunga bao katika kila mechi baada ya mkwaju wake kukosa lango.
Ilikuwa hadi dakika ya 65 wakati mlindalango Jasper Cillessen alipolazimika kuokoa mkwaju wa Sanchez uliopigiwa karibu na lango.
Hilo liliwatia waholanzi motisha na kumfanya Robben kupiga mkwaju uliomlenga Claudio Bravo katika lango la Chile baada ya kuwapiga chenga mabeki kabla ya Depay kuokoa kutoka kwa mlindalango kwa kuondoa katika maeneo ya hatari.
Kufutia ushindi huo Uholanzi wanatuchana na mshindi wa pili katika kundi A yaani Mexico.
Huku Chile ikiratbiwa kuvaana na mshindi wa kundi A yaani Brazil katika mechi za maondoano .
BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment