Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 11 April 2014

NDESAMBURO: SOKO LA MITUMBA KUREJEA KIBORLONI

Philemon Ndesamburo, Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema)

Moshi. Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo amewahakikishia wananchi na wafanyabiashara wa Moshi na vitongoji vyake kwamba soko la mitumba litarejeshwa katika eneo la Kiborloni.
Ndesamburo alisema kurejeshwa kwa soko hilo kutoka eneo la muda la Uwanja wa Kumbukumbu ya Mfalme George (Memorial) ni ahadi ya Chadema waliyoitoa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, alitoa kauli hiyo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kiborloni, ambayo ni moja ya ngome za Chadema.
Ndesamburo alisema baada Chadema ya kupata ridhaa ya kuongoza halmashauri, azimio la kwanza walilopitisha ni kurejesha soko hilo lakini mkurugenzi wa wakati huo alikataa kutekeleza azimio hilo.
Katika hatua nyingine, madiwani watatu, PeterKimaro wa Rau, Dk Charles Mmbando wa Soweto na Ovena Kowero wa viti maalumu, wamesema hawajawahi kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Naibu Meya.
Nafasi hiyo imeachwa wazi baada ya aliyekuwa akiishikilia, Vicent Rimoy ambaye pia alikuwa Diwani wa Kiborloni, kufariki dunia.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment