Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 12 April 2014

MKAPA AIASA AFRIKA MASHARIKI


Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akiwasha mshumaa
Arusha. Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amewataka wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kuacha kuoneana haya kwenye vikao vyao, badala yake waulizane yanayotokea kwenye nchi zao ili kuiepusha jumuiya na mauaji mengine ya kimbari kama ilivyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.
Aidha, Mkapa alisema kwamba nchi jirani za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Kimataifa hazikufanya ya kutosha kuzuia mauaji hayo na kwamba zinastahili kubeba lawama.
Mkapa alisema hayo jijini Arusha jana alipokuwa akizungumza kwenye maadhimisho ya mauaji ya kimbari ya Rwanda yaliyoandaliwa kwa pamoja baina ya Sekretarieti ya EAC na Ubalozi wa Rwanda nchini.
“Mungu apishilie mbali. Lakini kama jumuiya, lazima tujenge uwezo wa kukabili na kushughulikia matukio mabaya kama mauaji ya kimbari katika ukanda wetu wa EAC kwa kuimarisha vyombo vyetu na uwezo wa ndani,” alisema Mkapa.
Alikuwa akijibu swali la mwandishi wa gazeti hili aliyetaka maoni yake kuhusu hali tete inayoelezwa kuwapo nchini Burundi ikidaiwa kuchochewa na madai kuwa wanaomzunguka Rais Pierre Nkurunzinza wanamsukuma abadilishe Katiba ili agombee awamu nyingine.
Katiba hiyo ya Burundi iliyopatikana baada ya mazungumzo ya amani yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa miaka ya tisini iliweka ukomo wa nafasi ya urais kuwa wa awamu mbili za miaka mitano mitano.
Rais Nkurunzinza aliyeingia madarakani kupitia uchaguzi wa kidemokrasia anakamilisha awamu yake ya pili ya uongozi mwakani baada ya kuongoza taifa hilo kwa miaka 10.
EAC, Afrika na Jumuiya ya Kimataifa
Kuhusu mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Mkapa alisema nchi jirani zikiwamo wanachama wa EAC, Afrika na dunia kwa ujumla hazikufanya vya kutosha kuingilia kati ili kudhibiti mauaji ya Rwanda na zinastahili kubeba dhamana kwa kukiri hilo na kukubali lawama.
“Kwa siku 100 watu zaidi ya milioni moja waliuawa ikiwa ni wastani wa watu 10,000 kwa siku. Roho hizi zingeokolewa iwapo sisi majirani na Jumuiya ya Kimataifa tungetimiza wajibu wa kuhakikisha majirani zetu wanakuwa salama,” alisema Mkapa
Alitoa mfano jinsi alivyoshindwa kujibu swali la mtu aliyemtaja kuwa ni mkubwa aliyemhoji kwanini nchi za EAC hazikuonyesha juhudi za dhati na dhahiri kushughulikia amani nchini Kenya baada ya machafuko kuibuka mwaka 2007 kutokana na mvutano uliohusu matokeo ya uchaguzi Mkuu nchini humo.
“Mtakumbuka mimi, Graca Michel na Koffi Annan tuliteuliwa kutafuta suluhu na amani nchini Kenya. Mtu mmoja mkubwa alijitokeza na kunihoji kwanini hakuna juhudi za dhati za kushughulikia suala hilo miongoni mwa nchi za EAC. Sikuweza kujibu swali hilo,” alisema Mkapa.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment