Nje: Franck Ribery (kushoto) hataenda Brazil, huku kocha wake Didier Deschamps (kulia) akitazama mechi.
NYOTA wa Ufaransa, Franck Ribery atakosa fainali za kombe la dunia baada ya kushindwa kupona majeruhi yake ya mgongo.
Ribery pamoja na kiungo wa Lyon Clement Grenier wameondolewa rasmi katika kikosi cha Ufaransa kutokana na majeruhi.
Winga wa Bayern Munich, Ribery amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya mgongo na amekuwa akifanya mazoezi peke yake mpaka leo hii alipojiunga na wenzake mazoezini.
Ribery aliyeichezea Ufaransa mechi 80 ni mchezaji muhimu kwa Deschamps na kumkosa katika fainali za kombe la dunia ni pengo kubwa mno.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
No comments:
Post a Comment