Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 9 April 2014

NYUMBA 300 ZILIZOBOLEWA ZALETA WAWEKEZAJI WA KIMATAIFA

Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha

JIJI la Arusha limefanikiwa kuvunja nyumba zaidi ya 300 katika oparesheni maalumu ya kusafisha  jiji huku pia likiweza kuweka mikakati mbalimbali ya kuendelea kuboresha sehemu ambazo zimebomolewa nyumba hizo  huku pia Viongozi nao wakidai kuwa kuanzia kubomolewa kwa nyumba hizo kumeanza kuongeza idadi ya wawekezaji wenye nia ya kuwekza katika maeneo hayo.
Aidha nyumba hizo zilibomolewa siku chache zilizopita ambapo pia zoezi hilo liliweza kwenda sanjarai na ukamataji wa bidhaa ambazo zilikuwa zinauzwa nje bila mipangilio.
Hayo yamelelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela wakati akiongea na viongozi wa Majiji mbalimbali hapa nchini wakati akielezea mpango wa kuboresha jiji la Arusha
Alisema kuwa hapoa wali nyumba zilizobomelewa zilikuwa  katikati ya Jiji na zilikuwa zinalipa kodi ndogo sana ukilinganisha na hadhi yenyewe ya Jiji la Arusha hali ambayo ilisababisha waweze kuchukua hatua hiyo.
Mongela alisema kuwa kabla ya hapo walilazimika kuburutwa mahakani ambapo wenye nyumba hzio walidia kuwa Jiji limewaonea na hivyo hawapaswi kuondolewa katika nyumba hizo.
“Hawa walituburuza mahakamani na kudai kuwa tunawaonea sasa sisi tulishinda katika kesi hiyo na tuliweza kubomoa nyumba hizo ambazo walikuwa wanalipa kiasi cha kati ya elfu sita mpaka kumi kama kodi wakati kwenye majumba mengine watu wanalipa mpaka kiasi cha Mamilioni kwa ajili ya nyumba za biashara na nyumba za kuishi”aliongeza Mongela
 Hata hivyo Mkurugenzi mtendaji wa Jiji Juma Iddi alisema kuwa kwa sasa kuna mpango wa kuweza kuendeleza maeneo hayia mbayo yalikuwa kwanza na ujenzo holela lakini pia yalikuwa hayaingizi faida kubwa kwa Jiji
Iddi alisema kuwa toka nyumbha hizo kubomolewa Jiji la Arusha limekuwa katika taswira tofauti sana kwani kwa sasa hata wawezekaji nao wameanza kujitokeza tofauti na hapo awali ambapo kulikuwa na nyumba hizo
“Hapo awali tulikuwa hatufanikiwi kwa lolote hata kodi yao kwetu ilikuwa ni ndogo sana lakini kwa sasa tumeweza kubomoa na sisi tutawekeza kwenye majengo makubwa yenye hadhi zake na wala sio yale”aliongeza Iddi.
Pia alisema kuwa mbali na kuwekeza majengo yenye hadhi ya Jiji na kimataifa kwenye maeneo ambayo nyumba hizo zimebomolewa lakini pia wanampango endelevu wa kuhakikisha kuwa nyumba za Jiji la Arusha zinajengwa kwenye hadhi ambayo inakubalika na wala sio ujenzi holela.

No comments:

Post a Comment